Dunia Mwalukasa
New Member
- Aug 26, 2022
- 4
- 2
Wewe ni mshindi amka na Tumaini jipya
Umaskini unaweza kukunyima vingi, lakini usikubali kujishushia thamani yako kwa sababu ya umaskini. Usione umechakaa, thamani yako iko palepale.
Fanya kuiboost. Uchakavu wa noti hauondoi thamani yake. Kumbuka maskini ni tajiri asiyekuwa na pesa na utajiri ni kukinai ulichonacho. Sijui naeleweka Mungu wangu? Nasema hivi unyonge ukizidi unaweza nyongwa na haki yako usiipate.
Ukiipata utadhani hisani. Kuna vitu ukiacha kuvijali na vyenyewe vinaacha kukuumiza. Koma kuujali umaskini, kataa kuitwa maskini kwa moyo wako wote, akili zako zote na nguvu zako zote unapoanza siku mpya. Ubichi na ukakasi wa ndizi ni hatua za kuelekea kwenye utamu. Umaskini ni hatua za awali kuelekea kwenywe utajiri. Ongeza hatua!
Ukimaliza kupanga mipango yako iweke kwa maombi maana mpangaji mkuu sio wewe, ni Mungu! Ohooo! Mwamvuli hauzuii mvua isinyeshe bali huzuia kichwa chako kisinyeshewe. Imani yako kwa Mungu inaweza isizuie matatizo kutokea ila itazuia matatizo hayo kukujeruhi. Utakula sumu lakini hautakufa.
Ndio maana wazee wa zamani wakasema unapopiga goti kuomba mvua, ujue unaomba pia matope. Kikubwa mtangulize Mungu kwa kila jambo. Haya maisha danadana ni nyingi.
Kama washenzi walimroga Mtume Muhammad na kumuua Yesu watoto wa Mungu, wewe ni nani hadi uwe salama?
Uchawi haukumdhuri Mtume Mohammad na Yesu alishinda kifo kwa sababu walimtegemea Mungu.
Dunia Mwalukasa
0759474686
duniamwalukasa@gmail.com

Upvote
1