Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu salaam,
Tuna wazazi na walezi wa aina tofauti kwenye jamii, kuna wale wanaokwenda na wakati na wale ambao kidogo ka ukoloni kapo wakiamini njia zilizotumika miaka 47 kwake zitafanya kazi katika kizazi hiki.
Matumizi ya digitali yakua kadri siku zinavyosonga, si tu kwa watu wazima kwani hata watoto wanatumia digitali kwenye masomo yao na hata michezo. Sasa kuna wazazi ambao katika ulimwengu huu nyumbani kwake ni marufuku mtoto kumiliki na kutumia simu mpaka atakapofika chuo ikionekana huu ndio umri 'sahihi' au kwa wengine ni mpaka pale atakapokuwa na uwezo wa kujinunulia mwenyewe simu.
Kuna wazazi wengine siyo simu tu, hata TV nyumbani kwake ni marufuku, kwa kisingizio kuwa 'zinaharibu watoto', au 'siku hizi hakuna maadili', nk, unakuta TV inakaa chumbani kwa wazazi waangalie wenyewe, msiwafanyie watoto jamani 😁😁.
Nikwambie tu, kama wewe ni mzazi huyu jua tu kwamba mtoto wako anatumia simu kama hana akili nzuri, tena inawezekana anajua kutumia simu kuliko wewe, na wengine wanamiliki kabisa simu, ametoa wapi nani kamnunulia, hiyo inaweza kuwa topic ya wakati mwingine (ntawapa story sehemu ya comment mambo yasiwe mengi hapa, jinsi mzee wetu alivyokuwa mkoloni kwenye suala la TV na simu, na kama hilo lilituzuia kutumia vifaa hivyo).
Badala ya kumzuia, ambayo huwezi na unamnyima mtoto njia nyingine ya kujifunza na kukuza ubunifu, mwongoze kwenye matumizi mazuri ya simu, mueleze hatari anazoweza kukutana nazo kwenye mitandao hii na jinsi anavyoweza kutumia vizuri.
Apps nyingi zina matoleo ya watoto, muwekee hizo atumie na mara kwa mara fanya mazungumzo naye ya kirafiki ujue anafanya nini mtandaoni na vipi unaweza kumsaidia kuboresha zaidi matumizi yake.
Tukiwa tumeweka kalam chini kama Robert Heriel Mtibeli, tuambie, wewe ni mzazi wa aina gani, unamwongoza mtoto kwenye matumizi mazuri na kuhimiza matumizi ya digitali salama au team mafuruku mpaka mpaka mtoto awe na 'akili', pia tuambie kwanini?