Wewe ni Wewe!

Wewe ni Wewe!

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
🫵Wewe ni wewe katika maisha ni wewe ukilia ni wewe ukifurahi ni wewe ukibakwaa ni wewe maana kila kitu kipo juu yako ni wewe.

🫵Ukiwa bora ni wewe ukishindia dagaa ni wewe jikubali katika haya maisha ni wewe acha kudandia mtumbwi ambao sio wako wewe.

🫵Naongea na wewe maana unaiga maisha yana wenyewe kila kitu unachokifanya kina kuhusu wewe.

🫵Ukisemwa achana nao fanya mambo yako wewe maana ukifanikiwa unafanikiwa wewe mwenyewe na ukiumwa unaumwa mwenyewe sio yule ila ni wewe.

🫵Hujanielewa au hujanipata bado wewe ulimwengu wako wewe na siku utakao vua mwili ni wewe sio nyoka wala sio ng'ombe wewe yaaani ni wewe.

🫵Au niongeze sauti hujanielewaaaa wewee, vuta mibangi na unapo kunywa pombe unaye haribikiwa ni wewe angalia usizime ukapasuliwa mayai wewe maana kuna vijana wa hovyo nakwambia wewe.

🫵Ukifanywa vibaya aibu sio ya yule wala sio ya huyu ni yako wewee.

🫵Hii post mjanja ananielewa wewe usipo nielewa wewe ila ata nielewa yule itamfikia na atapata habari wewe.

🫵Mwili ni wako wewe na roho yako wewe ukiamka kiroho ukipata mafanikio na utambuzi unajiongoza wewe.

🫵Naongea na wewe kiakili ukinifikiria kama na rap sawa ila nakupa ujumbe uliokuwa bora ili ujiongoze wewe.

🫵Jitafute wewe ili usiwe mtumwa wa fikra wewe au unaimani ya injili ili usafiri ktk imani ya akili wewe.

🫵Ukiwa maskini ni wewe na ukiwa tajiri ni wewe au unafikiri yule akija atakupa utajiri bila ya kujiajili wewe.

🫵Nakuandikia ujumbe wewe ila uongo dhambi nakupenda sana wewe maana mimi ni mwalimu wako wewe ni wa upendo sana kuliko mwalimu wako wa hesabu wewe.

🫵Ukinichukia ni chukie tuu wewe ila nakupenda wewe kwa kukuandikia masomo mbalimbali ili ujikomboe na kujielewa wewe.

🫵Nikutakie mafanikio mema na familia yako kiujumla na ongeza juhudi ili mwanao afate nyayo zako wewe.

BY
DR CHAZZ
 
🫵Wewe ni wewe katika maisha ni wewe ukilia ni wewe ukifurahi ni wewe ukibakwaa ni wewe maana kila kitu kipo juu yako ni wewe.

🫵Ukiwa bora ni wewe ukishindia dagaa ni wewe jikubali katika haya maisha ni wewe acha kudandia mtumbwi ambao sio wako wewe...
Maaamaeee Manyanza
 
Juzi kuna jamaa yangu kanambia ukifikwa na majanga usije nifata kwa msaada. Nilimuuliza kwani toka nimezaliwa mpaka hapa nilipo kuna msaada wowote alio toa juu yangu?.
 
Juzi kuna jamaa yangu kanambia ukifikwa na majanga usije nifata kwa msaada. Nilimuuliza kwani toka nimezaliwa mpaka hapa nilipo kuna msaada wowote alio toa juu yangu?.
🤣🤣🤣
Kwani yeye ni nani huyo jamaa yako???
Halafu Wapuuzi kama hao Mimi ndio huwa nawamaindi kinoma yaani
 
Back
Top Bottom