Anselmo John
New Member
- Jul 8, 2019
- 1
- 0
Bila kujali kiwango cha Elimu yako, mali na pesa zako au idadi ya watu wanaokuzunguka. Kuna nyakati unaweza kuzipitia na kujiona wewe ni mtu wa kufeli zaidi kuliko wote duniani. Sio wewe pekee, bali kila mtu unaemuona, anaweza kupita katika nyakati hizo pia; Na katika uhalisia, asilimia kubwa ya binadamu wote tumewahi kupitia nyakati kama hizo katika maisha yetu.
Ukiwa kijana mtafutaji na unaependa mabadiliko chanya katika maisha yako, Maisha yatakuzawadia mambo makubwa mawili; MAFANIKIO AU KUFELI, na wakati mwingine unaweza kupewa vyote viwili kwa pamoja. Ni vigumu sana kukutana na mtu aliyefanikiwa pasipo kufeli hata mara moja au bila kuonja matokeo ya kufeli katika mipango au malengo yake. Asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa leo, walipitia hatua ya kufeli kwa kiwango kikubwa sana, na kutokana na kufeli kwao, walijifunza na kuwa imara zaidi na ndio maana tumeweza kushuhudia mafanikio yao leo.
Kama umepambana vya kutosha, umeweka juhudi za kutosha lakini bado unaambulia kufeli basi hauna budi KUSIMAMA IMARA ZAIDI na sio kukata tamaa. Ni kipindi cha muda tu unachopitia ili uweze kufikia ushindi mkubwa unaokusubiri. Siku ya leo nimekuandalia baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kuyakumbuka pale unapohisi kufeli katika mipango na malengo yako;
Haijalishi unapitia changamoto gani zinazokupelekea kufeli, haupaswi kuhisi uko peke yako au kudhani hakuna mtu anaeweza kukusaidia. Jaribu kuangalia watu wanaoweza kukusaidia katika ushauri na kukupa mwanga katika jambo linalokwamisha maendeleo yako. Kama ni matatizo binafsi ya kifamilia, basi jaribu kuzungumza na wazazi au wanafamilia wenzako ili uweze kutatua changamoto zilizopo nk. Usijaribu kabisa kufikiria kwamba umebaki peke yako katika kila tatizo au changamoto inayokunyima kusonga mbele, wala usije kuona aibu kuzungumza kwa kuogopa labda watakucheka na kukudharau kutokana na kufeli kwako.
Kitendo cha kufeli huzaa Fursa nyingi sana ambazo ni vigumu sana kuonekana kwa sababu asilimia kubwa ya wanaofeli hukata tamaa mapema na kuishia njiani katika kutimiza malengo/mipango yao. Fumbua macho na akili yako na utazame Fursa zilizojificha katika kufeli kwako. Bila shaka umewahi kumsikia “Jack Ma”, Mwanzilishi wa Alibaba Group, mjasiriamali na mmoja wa matajiri wakubwa nchini china.
Jack alifeli na kukataliwa mara nyingi sana katika maisha yake, lakini mwisho aliweza kutumia Fursa zilizojificha kupitia kufeli kwake na kutengeneza Fursa nyingi sana katika sekta ya Teknolojia. Na mpaka sasa ni miongoni mwa wafabiashara wakubwa sana duniani. Kama Jack aliweza kufanya hivyo, Kwanini mimi na wewe Tushindwe?
Kuna ukomo katika kufeli kwako, hauwezi kufeli milele katika maisha yako. Ukiwa mtu wa kutokata tamaa mapema, mtu wa kuongeza juhudi zaidi katika kila unachokifanya, basi hali ya kufeli itazidi kupungua kadri unavyozidi kuongeza juhudi za kukabiliana na vikwazo vyako. Amini na weka akilini mwako kwamba, “Hali ya Kufeli HAITADUMU MILELE.” Jifunze kutoka kwa mtoto mdogo anaejifunza kutembea. Je, akiacha kujifunza kwa sababu ya kuanguka mara nyingi, atafanikiwa kutemebea? Bila shaka jibu ni HAPANA. Unapaswa kuongeza juhudi na kusimama tena kila mara unapofeli; Na hii ndio moja ya njia kuu za kuishinda hali ya kufeli.
Kila mara unapofeli, weka ahadi ya kutorudia tena makosa yaliyosababisha ufeli na kushindwa kusonga mbele. Weka nia ya kujifunza na kutorudia tena kupita katika njia iliyokupeleka nje ya malengo/mipango yako. Kubali kwamba ulifeli, jifunze na songa mbele zaidi ukiwa na tahadhari ya kutorudia tena makosa uliyoyafanya.
Elimu uliyoipata leo ikakusaidie kila mara unapopitia hali ya kufeli. Kamwe usiruhusu Fikra hasi zikuambie kwamba, hapo ndio mwisho wako. Hata barabara ina miinuko, mabonde na mteremko. Basi hata katika safari ya kutimiza ndoto na malengo yako ni hivyo hivyo; Utakutana na changamoto mbalimbali zinazoweza kukupelekea kufeli na kuona huwezi tena kusonga mbele.
Anselmo John.
www.anselmojohn.com

- HAUKO PEKEE YAKO, ZUNGUMZA NA WATU.

- FURSA NYINGI ‘HUZALIWA’ PALE UNAPOFELI MARA NYINGI.
Kitendo cha kufeli huzaa Fursa nyingi sana ambazo ni vigumu sana kuonekana kwa sababu asilimia kubwa ya wanaofeli hukata tamaa mapema na kuishia njiani katika kutimiza malengo/mipango yao. Fumbua macho na akili yako na utazame Fursa zilizojificha katika kufeli kwako. Bila shaka umewahi kumsikia “Jack Ma”, Mwanzilishi wa Alibaba Group, mjasiriamali na mmoja wa matajiri wakubwa nchini china.
Jack alifeli na kukataliwa mara nyingi sana katika maisha yake, lakini mwisho aliweza kutumia Fursa zilizojificha kupitia kufeli kwake na kutengeneza Fursa nyingi sana katika sekta ya Teknolojia. Na mpaka sasa ni miongoni mwa wafabiashara wakubwa sana duniani. Kama Jack aliweza kufanya hivyo, Kwanini mimi na wewe Tushindwe?
“Tumia kufeli kwako kuzitambua Fursa zilizojificha. Fursa moja utakayoigundua, inaweza kubadili kabisa maisha yako na dunia nzima.”
- KUFELI NI HALI YA MUDA TU, HAITADUMU MILELE.
Kuna ukomo katika kufeli kwako, hauwezi kufeli milele katika maisha yako. Ukiwa mtu wa kutokata tamaa mapema, mtu wa kuongeza juhudi zaidi katika kila unachokifanya, basi hali ya kufeli itazidi kupungua kadri unavyozidi kuongeza juhudi za kukabiliana na vikwazo vyako. Amini na weka akilini mwako kwamba, “Hali ya Kufeli HAITADUMU MILELE.” Jifunze kutoka kwa mtoto mdogo anaejifunza kutembea. Je, akiacha kujifunza kwa sababu ya kuanguka mara nyingi, atafanikiwa kutemebea? Bila shaka jibu ni HAPANA. Unapaswa kuongeza juhudi na kusimama tena kila mara unapofeli; Na hii ndio moja ya njia kuu za kuishinda hali ya kufeli.
- UNAPOFELI MARA MOJA, USIRUDIE TENA MAKOSA ULIYOYAFANYA.
Kila mara unapofeli, weka ahadi ya kutorudia tena makosa yaliyosababisha ufeli na kushindwa kusonga mbele. Weka nia ya kujifunza na kutorudia tena kupita katika njia iliyokupeleka nje ya malengo/mipango yako. Kubali kwamba ulifeli, jifunze na songa mbele zaidi ukiwa na tahadhari ya kutorudia tena makosa uliyoyafanya.
Elimu uliyoipata leo ikakusaidie kila mara unapopitia hali ya kufeli. Kamwe usiruhusu Fikra hasi zikuambie kwamba, hapo ndio mwisho wako. Hata barabara ina miinuko, mabonde na mteremko. Basi hata katika safari ya kutimiza ndoto na malengo yako ni hivyo hivyo; Utakutana na changamoto mbalimbali zinazoweza kukupelekea kufeli na kuona huwezi tena kusonga mbele.
Ulikuwa nami Rafiki na Mwalimu wako,Jifunze kusimama imara bila kutetereka, “Wewe sio mtu wa kufeli siku zote; Ni hali ya muda tu, inapita na haitadumu milele.”
Anselmo John.
www.anselmojohn.com