hii ni shule ya msingi.. mi nilikuwa mchora ramani wa darasa
sijawahi ingia kipindi cha hesabu kuanzia darasa la tatu mpaka la saba, hata walimu wa hilo somo hawakuwa wakinifahamu, ia nilikuwa mkimbiza upepo mzuri enzi za umitashumta, namba mbili au moja ndio zilikuwa namba zangu..nilikuwa mtoro siku zingine nashinda mtoni asubuhi na mapema katika begi la shule kuna karai, na mafuta ya kula, nikifika mtoni siulizi natafuta mtumbwi wowote uwe mzima ama m bovu naanza kukagua nyavu za wavuvi moja baada ya nyingine na nikikuta samaki sitoi kistaarabu ntachelewa, napitisha wembe, ilikuwa kujulikana siku mtumbwi ulipobiduliwa na kiboko na kunifanya nirudi home uchi,
vichongeo nilikuwa navyo zaidi ya mia tatu home
nilikuwa na mikebe ya wenzangu kama hamsini
nilikuwa na funguo zinazofungua shule nzima mpaka nyumba za walimu, kwa walimu sikuwa nachukua chochote zaidi ya vitabu na tukikuta msosi tunakamua tunasepa
nilikuwa mpole sana kiasi ukiletewa kesi yangu kama ni mwalimu lazma unisamehe
nilikuwa pia mkorofi nakudunda na ukienda kunishtaki unachapwa wewe
pia ule mchezo wa kuweka vioo chini kuchungulia chupi zao nilikuwa nao