Wewe ungefanyaje???

Mtalingolo

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
2,181
Reaction score
410
Ni muda mfupi tangu uoe. Sikumoja uliporudi kutoka kazin ukamkuta mwanaume ambaye mkeo amekutambulisha kuwa walisoma darasa moja hivyo ni kama kaka yake. Ikawa mara kwa mara unaporudi unamkuta mwanaume huyo kwenye chumba chenu mlichopanga akipiga stori na mkeo.

Sikumoja kunajamaa akakutonya kuwa yule mwanaume na mkeo ni wapenzi wa siku nyingi. Ulipomuuliza mkeo kuhusiana na tuhuma hzo anakwambia kuwa ni kweli alikuwa mpenz wake na ndie mwanaume wake wakwanza aliemtoa usichana ila ni muda mrefu wameachana, wamebaki kama kaka na dada.

JE UNGEKUWA WEWE UNGEFANYAJE?
 
Hapo kuna cha kufanyaje tena?

Wasichana mara nyingi huwa hawawi na mahusiano ya karibu na watu waliowatoa usichana.
 
Hiyo scenario yako hujaiweka vizuri...

Haina uhalisia.. Anyway,kwa hili kila mtu ana majibu yake..
 
Hapo hakuna cha kufanya zaidi ya kuwaambia kwaheri endelezeni libeneke tu nawaachia chumba nachukua vitu vya kuanzia maisha najikataaa tu!
 
naondoka,naenda pale kwa mangi,nagonga konyagi mzinga mmoja,nikishapata steam ntapata lakufanya.
 
Ina uhalisia mimi nilishaona live wakati nimepanga kuna jamaa alikuwa amezaa na mtu kabla ya kuolewa na mumewe alikuwa anamkuta yule jamaa kila siku ndani na wakati mwingine anawakuta wanasindikizana. Jamaa alikuwa ni mvumilivu sana

Hiyo scenario yako hujaiweka vizuri...

Haina uhalisia.. Anyway,kwa hili kila mtu ana majibu yake..
 
wao wana msemo wanasema...''awali ni awali hakuna awali mbovu''.....
 
Ina uhalisia mimi nilishaona live wakati nimepanga kuna jamaa alikuwa amezaa na mtu kabla ya kuolewa na mumewe alikuwa anamkuta yule jamaa kila siku ndani na wakati mwingine anawakuta wanasindikizana. Jamaa alikuwa ni mvumilivu sana

Tulipanga nyumba moja nini? Kiukweli inauma jamani...
 
duh hapo inatakiwa busara ya hali ya juu
 
usipoua unaweza ukalia kama mtoto mdogo. Matokeo yake utaonekana *****.cha msingi ni ku face stuation with sorber mind.

Inakuwaje hyo sorber mind mkuu? Ila busara kweli inahitajika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…