Wezesha kwenye M-PESA

Kwema ndugu zangu....leo nilikuwa naomba kupata elimu juu ya wezesha kwenye m-pesa hasa kwa mawakala mfano nikikopa 150,000/= marejesho yake shs ngap??. Kwa mda wa mwezi mmoja.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Hongera Mkuu.

Wezesha ni huduma inayokuwezesha wakala kupata kiasi cha pesa kutokana na matumizi yako na kukirudisha baada ya mwezi mmoja kwa riba ya 10%.

Mfano, wewe kiasi chako ni 150,000 basi ukiipata watakupa lakini utarudisha pamoja na riba ya 10% ambayo ni 15,000. Hivyo kwa ujumla utarudisha 165,000 baada ya mwezi.

Lakini, riba yao wataichukua punde tu baada ya kukuwezesha. Mfano wakikupa hiyo 150,000, kwenye account yako itaingia 135,000 baada ya kuondoa 15,000 yao ya riba.

Then, mwisho wa mwezi ndiyo utarudisha 150,000.

Karibu.
 
Asante sana....kwa elimu nzuri.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Rejesho mnachukua kwenye mtaji wake????

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kwa mfano ukipewa mkopo wa shs 150,000/= ukamaliza vizuri...ukitaka kurudia tena wanakukopesha shs ngapi????

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app

Ile ile ila me nilibahatika round ya kwanza nilipewa 150k ya pili wakanipa hiyohiyo kabla mwezi haujaisha wakaniongezea ikawa 300k ndo nipo nayo mpaka sasa
 
Ikifika siku ya kurejesha utarejesha mwenyewe process kama ulivyokua unataka kukopa ila ujue kwamba ukiwa na deni songesha hautaruhusiwa kukopa wezesha, na ukikopa wezesha hautaruhusiwa kutumia songesha
Nilimpa dogo mmoja atumie laini yangu lakini cha kushangaza kapiga matukio eti kakopa sehemu zote hizo 2 hii imekaeje au iliwezekana vipi?
 
Nilimpa dogo mmoja atumie laini yangu lakini cha kushangaza kapiga matukio eti kakopa sehemu zote hizo 2 hii imekaeje au iliwezekana vipi?

Saivi inawezekana vizuri
 
Saivi inawezekana vizuri
Daaah!! Hili nalisolve vipi maana dogo katoweka baada ya kupiga tukio la mikopo tena hela kubwa, kwingine laki 9 na chenji na pengine laki 3 na point.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…