Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 4,039
- 2,840
Hivi karibuni TCRA imesisitiza kutokuwapa mawasiliano wanaotumia namba za Simu ambazo hazijasajiliwa tena kwa kutumia vitambulisho halali vya wateja. hii ina maanisha hakuna MTZ anayetumia Simu sasa hivi bila kusajiliwa.Umezuka utapeli mjini wa kupora watu pesa baada ya kuwasiliana na Tapeli. Matapeli wakishapora pesa hunyanganya pia simu ya Victim wao na kutoweka nayo hata kama ni ya Mchina. Wanaotapeliwa hawana jinsi ya kuwapata Wezi hao zaidi ya Kutrace namba za Simu. Polisi wanaweza kuwasaidia wanyonge hawa kwa kufuatilia mawasiliiano na za CCTV Benki au Hotel kubwa. Naomba kuwasilisha wanaJamii ili tuwasaidie wale wanaopoteza mali zao kwa njia ya Kutapeliwa na Wezi wanaotumia mitandao ya simu kuwapata wa kuwaibia hapa Mjini na kwingineko. Yupo Mstaafu ametapeliwa MILION 80 anataka kukodi FBI wamsaidie kupata wezi wake. Huu ni Ulimwengu wa Science na Technolojia na Tz kwa hili hatuhitaji FBI au CIA kufuatilia.