Wezi wa BoT wazuiwa kusafiri nje

Wezi wa BoT wazuiwa kusafiri nje

..ina maana ukirudisha ndio inakuwa imetoka kesi hakuna au?

SIDHANI KAMA WATZ TUTAKUWA TUMETENDEWA HAKI. Hawa mafisadi wanatakiwa wafikishwe kwa Pilato na tusikie wako Segerea kwa wizi wa mali za umma. Msije mkaniambia hamna evidence ya kuwapeleka mahakamani tafadhali. Msinifanye niamaini ule utetezi wa fisadi Karamagi kwamba ilikuwa hakuna uwezekano wa kuvunja mkataba na Richmond kwa vile wangetupeleka mahakamani na Serikali ingepata hasara.
 
Akishalipa inakuwaje? ndio swali lililopo. Kuiba na kukopa ni vitu tofauti na mahakama zipo. Nani uliemsikia akaiba halafu akarudisha?
Tuwache unazi kama kuna wizi umefanyika kwenye hizo account basi huu wizi ni wandani ukishirikisha watu wa nje, hawezi kukurupuka tu mtu wa nje kwenda kuchota benki? wenye bank walikuwa wapi? wamelala?

Kuna namna moja tu mtu aliyeiba, akija na pesa au kitu alichoiba nakusema ndugu nilikuibia naomba unisamehe. Kama wamefika na pesa hizo na kuomba msamaha tujulishwe maana tulioibiwa ni sisi watanzania wote. Haki ya kuwasemehe ni sisi. Hivyo tunaomba tueleweshwe kama wanaomba msamaha au wanarudisha kwa kiburi wakisema pesa hiyo ni kitu gani kwangu kama huyo aliyelipa billion 10. Hayo ni majivuno na kuendelea kutuzarau.
 
Jamani accounts za Import Support ni mikopo ambayo inakuwa na repayment schedule. Kama mkopaji anakiuka mpangilio wa malipo basi kwenye contract kutakuwa na clause ya hatua ya kuchuliwa. Kmfn. kuuza mali ya mkopaji kufilisi etc.Hii hufanyika kisheria kama kupitia court broker and so on.Hawa jamaa watakuwa wamekiuka malipo kwa muda mrefu sana hivyo watu wa kuhusiswa kimahakama au kinidhamu ni mabenki/benki kuu yaani watumishi.Jambo la kuzingatiwa hapa ni kucharge proper interest rates for the whole period and if provision is there any penalities.
 
Kuazia sasa, wale wezi wa fedha zetu pale Benki Kuu ya Tanzania wamezuiwa kusafiri na karibu wote hadi mchana walikuwa wamesalimisha pasipoti zao kwa jamaa wa usalama wa taifa.

Ninasema wote, ingawa wapo wawili watatu hivi wanaonekana kukwepa kwamba wao hawahusiki, ingawa wanatajwa tajwa sana. Yasemekana wamehojiwa, lakini wanashindwa kubanwa moja kwa moja na wizi huo wa kutisha wa fedha kwa barabara zetu, dawa zetu, elimu yetu na kila kitu chetu.

Miongoni mwa watu hao ambao wazungu wanasema bado wako at larger ni Jeetu Patel na yule muiran anayejifanya sana kuwa mwanaCCM wa damu na swahiba wa Kikwete.. si yule jamaa wa kule Unyamwezini. Yaani hamumjui had nimtaje...haaaaa huyo huyo. naye bado jamaa wa usalama nasikia na wanamuogopa kwa kuwa ni right hand man wa mkuu wa kaya.

Lakini kwa sasa acha wakome. Nasikia wengine wanatamba, hasa Maregezi kuwa hana wasiwasi atarejesha hizo blini 16 alizokwiba. Anasema alichofanya aliziweka benki kwenye fixed account sasa akawa anakula riba, sasa wakizitaka anazo. Anasema amesharejesha 10,000,000,000.

siyo rahisi kiasi hicho kuwakamata hao watu kwa sababu hiyo hela haiko mikononi mwao kwa hiyo hawawezi kuirudisha. hiyo hela ilitumika kwenye kampeni ya 2005. we unafikiri zile tisheti zote za chama twawala zilitoka wapi? yaani zilivyo nyingi mpaka leo watu wanaenda nazo kanisani na kuna godown chan'gombe bado lina tisheti laki 2 za chagua kikwete.

hao watu wote waliohusika na hayo mahela wana paspoti 2 kwa hiyo kuwakilisha moja polisi si kitu cha kutisha.

ukiwa na elfu 90 unapatapaspoti mpya within one hour kwa hiyo hakuna wasiwasi wa kupata pasi hata wakitaka kuchukua kumi wataletewa.
 
I don't want to be judgemental here sababu the saga seems to be folded. Ila sioni kwa nini mwanasheria mkuu haja asign mpaka sasa msoma mashitaka na kutingisha kesi itakayosema REPUBLIC OF TANZANIA VS JITU PATEL, OR REPUBLIC OF TANZANIA VS ROSTAM AZIZ. I wanna see that, then i will praise Mh.Jakaya Kikwete on medias.

We don't want the money to be returned now, we want them to be prosecuted, then requesting maximum penalty and final freez every asset the have ( I mean everything mpaka tea spoon). That will be example not only kwa Karamangi and his crue, but kila fisadi.
 
Kwanza napenda kuipa JF pongezi kwamba sasa ina Msemaji bnafsi wa JK hapa ambate ni ndugu Dar Es Salaam .Hili ni jambo jema na tulitumie vyema kupata majibu ya maswali yetu kwa JK.Ndugu Dar nakjuomba pia umpelekee salaam za malalamiko yetu .Anatuharibia Nchi kwa kutaka sifa .Sisi sifa pekee tunayo itaka ni Tanzania kumeremeta kama dhahabu zetu na mbga zetu wanavyo zitumia vibaya waache tuwe kama Mbuga zetu na madini yetu.waache kugusa jungu kuu yaani BOT nk .
 
Habari hizi kama ni za kweli inabidi JK apewe pongezi kwani tunaona shughuli zake. Ahsante JK.

PongEzi zipi hapa wakati

ROSTAM AZIZ, E LOWASA, B MKAPA,MRAMBA, BALALI, JEETU PATEL, MGONJA, na wengine wengi mainzi bado yanawafata kwanyuma
 
Nachelea kusema kwamba vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kuwashughulikia hawa majahili vinachukua muda mwingi saana kuwakamata! Kwa nini hawa tunaowashuku wasikamatwe wakatupwa lupango huku upelelezi ukiendelea? Kukaa kwao uraiani ni kuwapa mwanya wa kuvuruga ushahidi.
 
Nadhani mikopo inadondokea kwenye makubaliano ya kesi za madai na nijuavyo mimi ukilipa hakuna kesi unless wanasheria wetu humu watufafanulie zaidi.

Dar,haya mambo siye twasubiri yawekwe hadharani,haya mambo ya kudhania kwangu siyapi nafasi. Mengi tu twayasikia lakini hatusemi kwasababu twasubiri uwazi ambao tunajua hwauwezi kutokea via JK. Tukimuuliza JK,zile zilizoenda kwenye kampeni ya CCM 2005 kupitia Kagoda farm,atajibu nini? Mbona hizi hawasisemi,au zimerudi? Dar muulize JK. Tuliambiwa tutakuwa tunapewa taarifa toka hii tume ambayo ndani yake inawatuhumiwa wa Richmond,mbona hatujaambiwa? Dar muulize JK atupe jibu.
 
Nachelea kusema kwamba vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kuwashughulikia hawa majahili vinachukua muda mwingi saana kuwakamata! Kwa nini hawa tunaowashuku wasikamatwe wakatupwa lupango huku upelelezi ukiendelea? Kukaa kwao uraiani ni kuwapa mwanya wa kuvuruga ushahidi.

Ukichunguza na kufikiria sana hapa mambo yalivyo ni kama kumtaka nyani ahukumu kesi ya ngedele......! yaani kifupi hakuna mtu msafi ambaye anaujasiri wa kuwafunga kengele wezi hata kama amepewa meno!! Kwa hiyo ndugu yangu hiyo chelewachelewa ya vyombo vya dola mi naona ni intentional ili tu kuwapa nafasi wezi kujipanga vizuri!!
 
Nasikitika kwa watu kuanza kutoa pongezi na misifa wakati hata uthibitisho wa hii habari haujafanyika. Ndugu Dar es Salaam kwanza unatakiwa kuelewa ishu BOT kwa sasa pale ambayo ina watuhumiwa tayari ni EPA na si import support. Hiyo EPA ni wizi mtupu waliofanya hao jamaa maana the idea ilikuwa ni kununua madeni ya nje ya serikali na kampuni yako kulipwa madafu. Hao wezi walifungua kampuni hewa na kufaidika na mpango huo. Hivyo wamiliki wa makumpuni hayo, their BOT inside connections,RA, Benja na probably muungwana in short wote ni wezi!!!!!!!!!!!!!!!

Ushauri wa bure: Dar huwezi kumconvince mtu yeyote mwenye akili timamu na mpambanuaji wa mambo kwamba JK is serious in fighting corruption.

"Jamani wapi Balali tumemmiss kinoma au ndio tumeshamsahau baada ya richmond na Lowasa??????"
 
Kwanza napenda kuipa JF pongezi kwamba sasa ina Msemaji bnafsi wa JK hapa ambate ni ndugu Dar Es Salaam .Hili ni jambo jema na tulitumie vyema kupata majibu ya maswali yetu kwa JK.Ndugu Dar nakjuomba pia umpelekee salaam za malalamiko yetu .Anatuharibia Nchi kwa kutaka sifa .Sisi sifa pekee tunayo itaka ni Tanzania kumeremeta kama dhahabu zetu na mbga zetu wanavyo zitumia vibaya waache tuwe kama Mbuga zetu na madini yetu.waache kugusa jungu kuu yaani BOT nk .

Napenda ufahamu ya kuwa sipo hapa kusemea JK wala yeyote yule, kama wewe upo hapa kwa kumsemea fulani, basi hayo ni yako na si yangu.

Nadhani hata wewe hizo salaam unaweza kuzifikisha kwani hujui address yake? kama huijui naomba nifahamishe nami ntakupatia.

Alie kuharibia nchi humjui? au unachuki binafsi? Mbuga zilikodishwa kwa bei ndogo awamu ipi? na hujui kuwa awamu ya JK ndio wamezirekebisha hizo bei za kutumia mbuga kuwa realistic? Madini yetu ni nani alianza kuyagawa hovyo? au huoni kuwa JK kaanza kwa kurejea mikataba yote ya zamani, muulize au mngoje Mheshimiwa Zitto Kabwe na kamati yake tuone madudu alifanya nani. Au hujui kuwa JK kaunda hiyo kamati? Na hio BoT unayoitaja si unaona JK anachofanya au hukioni?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Ukweli unabaki pale pale, hakuna awamu inayopigana na rushwa na ufisadi kama awamu ya JK. Au hukumbuki Mkapa alivyoikalia kwa miaka report ya Warioba?
 
Kuna namna moja tu mtu aliyeiba, akija na pesa au kitu alichoiba nakusema ndugu nilikuibia naomba unisamehe. Kama wamefika na pesa hizo na kuomba msamaha tujulishwe maana tulioibiwa ni sisi watanzania wote. Haki ya kuwasemehe ni sisi. Hivyo tunaomba tueleweshwe kama wanaomba msamaha au wanarudisha kwa kiburi wakisema pesa hiyo ni kitu gani kwangu kama huyo aliyelipa billion 10. Hayo ni majivuno na kuendelea kutuzarau.

Naona jibu lako umelipata hapa chini, ile ni mikopo na mwenekapufi kaifafanua vizuri.

Jamani accounts za Import Support ni mikopo ambayo inakuwa na repayment schedule. Kama mkopaji anakiuka mpangilio wa malipo basi kwenye contract kutakuwa na clause ya hatua ya kuchuliwa. Kmfn. kuuza mali ya mkopaji kufilisi etc.Hii hufanyika kisheria kama kupitia court broker and so on.Hawa jamaa watakuwa wamekiuka malipo kwa muda mrefu sana hivyo watu wa kuhusiswa kimahakama au kinidhamu ni mabenki/benki kuu yaani watumishi.Jambo la kuzingatiwa hapa ni kucharge proper interest rates for the whole period and if provision is there any penalities.
 
Wengi wanashangaza sana hasa wale wanao towa tuhuma ya kuwa pesa zimeibwa zikaenda kwenye kampeni ya JK ya 2005, hivi kama msemayo ni kweli na ushahidi mnao, kwa nini msiende mahakamani? au ndio lazima mseme tu? Au hakuna ushahidi wa kutosha?

Jee, kuna sheria inayozuia raia yeyote kwenda kushitaki?
 
Nasikitika kwa watu kuanza kutoa pongezi na misifa wakati hata uthibitisho wa hii habari haujafanyika. Ndugu Dar es Salaam kwanza unatakiwa kuelewa ishu BOT kwa sasa pale ambayo ina watuhumiwa tayari ni EPA na si import support. Hiyo EPA ni wizi mtupu waliofanya hao jamaa maana the idea ilikuwa ni kununua madeni ya nje ya serikali na kampuni yako kulipwa madafu. Hao wezi walifungua kampuni hewa na kufaidika na mpango huo. Hivyo wamiliki wa makumpuni hayo, their BOT inside connections,RA, Benja na probably muungwana in short wote ni wezi!!!!!!!!!!!!!!!

Ushauri wa bure: Dar huwezi kumconvince mtu yeyote mwenye akili timamu na mpambanuaji wa mambo kwamba JK is serious in fighting corruption.

"Jamani wapi Balali tumemmiss kinoma au ndio tumeshamsahau baada ya richmond na Lowasa??????"

Napenda kukuhakikishia kuwa sipo hapa "kumconvince" yeyote kwa chochote. Natoa maoni yangu kwa muono wangu, nawe toa yako kwa muono wako, alimradi tusijidanganye, la kweli tuliseme na tusilokuwa na uhakika nalo tuulize na tuloliona sawa ndio hilo tulitetee. Upo hao ulipo? Wezi ni wengi tu, na JK ndio yumo katika kuwasafisha na kazi yake inaonekana. Asiye na macho haambiwi tazama. Asiye na masikio haambiwi sikia.
 
Good work Dar-es-salaam, you are definately blending in now..i like the lito twist u added 'maoni yako' lol sounding like a true govt spokesperson..very nice..keep it up..at your rate of posting threads and replying to threads, you will be a senior expert member of JF real soon and people will actually take your views seriously..lol
 
napenda kuwakilisha kwa machungu kabisa wizi wa wazi wazi unaofanywa na Kampuni ya simu ya VODACOM...
Vodacom imekua na dealers wengi Tanzania nzima na katika hao dealers wengi pia wanateua sub-dealers kudeal kwa niaba yao mikoani....
Vodacom imekua inatangaza sana huduma zake kwatika radio, TVs, Newspapers, etc... kwa kipindi cha December 2007 walikua na Vouchers kibao zainazo-karibia ku-expire mitaani...kama kweli inawajali wateja wake ilishindwa nini kutangaza na kuwaambia wateja wake wawe makini wanunuapo vouchers?????
Binafsi nimekutwa na mkasa huo na kwa masikitiko nimejikuta napigwa danadana isioeleweka...mara ooh!! vouchers sio za dealer husika i.e. vouchers zinaonyesha ni za shivacom na wewe mteja unadai umenunua Alphatel!!!!
KWELI HUU NI WIZI WA WAZI WAZI KWA WALALAHOI NA PIA SIO USTAARABU KABISA...LEO HII WANASHEREHEKEA WATEJA MILION 4 LAKIN WAELEWE KUWA KUTOMRIDHISHA MTEJA 1 KWA JAMBO DOGO INAWEZA IKAWAHARIBIA HAYO MAFANIKIO WANAYOJIVUNIA!!!!
 
Watu wanaotoa sifa Kama akina Dar ni watu ambao wanadondokewa na masalia ya Ufisadi uliofanywa na unaofanywa. Haihitaji shule, bali akili timamu tu, kugundua kuwa JK hana nia ya kuwashughulikia hawa wezi ila anajikuta analizimishwa na mazingira hasa anapoangalia 2010. Uhujumu na wizi wote tunaousikia sasa pamoja na kuwa na watu wengine, pia una mkono wa JK.Kivuli chake ndo kinamfunga mikono. Anachoangalia yeye ni uchaguzi wa 2010,ili isije ikawa ngumu kwake kama Kibaki. Analazimika kufanya mazingaombwe kuwa-fool watanzania ambao wengi wetu tuna mawazo kama Dar.
 
Kuna namna moja tu mtu aliyeiba, akija na pesa au kitu alichoiba nakusema ndugu nilikuibia naomba unisamehe. Kama wamefika na pesa hizo na kuomba msamaha tujulishwe maana tulioibiwa ni sisi watanzania wote. Haki ya kuwasemehe ni sisi. Hivyo tunaomba tueleweshwe kama wanaomba msamaha au wanarudisha kwa kiburi wakisema pesa hiyo ni kitu gani kwangu kama huyo aliyelipa billion 10. Hayo ni majivuno na kuendelea kutuzarau.
hii NI DHARAU TENA YA HALI YA JU.KWANZA MI NASHAURI WAKISHAMALIZ KURUDISHA HAYO MAHELA YETU UFANYIKE TENA UKAGUZI KUJA KAMA KWELI WAMERUDISHA NA HABARI ZITOKE KAMA MWANZO KUONYESHA KAMPUNI ZILIZOTUIBIA NA NGAPI ZIMERUDISHA NA HATIMAYE HAWA WTU WANA CHA KUJIBU KWA PILATO BWANO.
 
JAMANIEE hawa watu wanacheza na wtz kwani huyo muiran wanashindwa nini kumtumia usalama wa taifa ukamkamate kama walivyofanya kwa vijana wetu wa JF?au ndio ufisadi unawatisha?na huyu mwengine mbona alishatoroka long time watampataje?JEET PATEL.KAMA KWELI WAMEANZA KURUDISHA SIE TWASHUKURU MUNGU ILA WAFUNGWE HAO NI WEZI KABISA
 
Back
Top Bottom