..ina maana ukirudisha ndio inakuwa imetoka kesi hakuna au?
Akishalipa inakuwaje? ndio swali lililopo. Kuiba na kukopa ni vitu tofauti na mahakama zipo. Nani uliemsikia akaiba halafu akarudisha?
Tuwache unazi kama kuna wizi umefanyika kwenye hizo account basi huu wizi ni wandani ukishirikisha watu wa nje, hawezi kukurupuka tu mtu wa nje kwenda kuchota benki? wenye bank walikuwa wapi? wamelala?
Kuazia sasa, wale wezi wa fedha zetu pale Benki Kuu ya Tanzania wamezuiwa kusafiri na karibu wote hadi mchana walikuwa wamesalimisha pasipoti zao kwa jamaa wa usalama wa taifa.
Ninasema wote, ingawa wapo wawili watatu hivi wanaonekana kukwepa kwamba wao hawahusiki, ingawa wanatajwa tajwa sana. Yasemekana wamehojiwa, lakini wanashindwa kubanwa moja kwa moja na wizi huo wa kutisha wa fedha kwa barabara zetu, dawa zetu, elimu yetu na kila kitu chetu.
Miongoni mwa watu hao ambao wazungu wanasema bado wako at larger ni Jeetu Patel na yule muiran anayejifanya sana kuwa mwanaCCM wa damu na swahiba wa Kikwete.. si yule jamaa wa kule Unyamwezini. Yaani hamumjui had nimtaje...haaaaa huyo huyo. naye bado jamaa wa usalama nasikia na wanamuogopa kwa kuwa ni right hand man wa mkuu wa kaya.
Lakini kwa sasa acha wakome. Nasikia wengine wanatamba, hasa Maregezi kuwa hana wasiwasi atarejesha hizo blini 16 alizokwiba. Anasema alichofanya aliziweka benki kwenye fixed account sasa akawa anakula riba, sasa wakizitaka anazo. Anasema amesharejesha 10,000,000,000.
Habari hizi kama ni za kweli inabidi JK apewe pongezi kwani tunaona shughuli zake. Ahsante JK.
Nadhani mikopo inadondokea kwenye makubaliano ya kesi za madai na nijuavyo mimi ukilipa hakuna kesi unless wanasheria wetu humu watufafanulie zaidi.
Nachelea kusema kwamba vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kuwashughulikia hawa majahili vinachukua muda mwingi saana kuwakamata! Kwa nini hawa tunaowashuku wasikamatwe wakatupwa lupango huku upelelezi ukiendelea? Kukaa kwao uraiani ni kuwapa mwanya wa kuvuruga ushahidi.
Kwanza napenda kuipa JF pongezi kwamba sasa ina Msemaji bnafsi wa JK hapa ambate ni ndugu Dar Es Salaam .Hili ni jambo jema na tulitumie vyema kupata majibu ya maswali yetu kwa JK.Ndugu Dar nakjuomba pia umpelekee salaam za malalamiko yetu .Anatuharibia Nchi kwa kutaka sifa .Sisi sifa pekee tunayo itaka ni Tanzania kumeremeta kama dhahabu zetu na mbga zetu wanavyo zitumia vibaya waache tuwe kama Mbuga zetu na madini yetu.waache kugusa jungu kuu yaani BOT nk .
Kuna namna moja tu mtu aliyeiba, akija na pesa au kitu alichoiba nakusema ndugu nilikuibia naomba unisamehe. Kama wamefika na pesa hizo na kuomba msamaha tujulishwe maana tulioibiwa ni sisi watanzania wote. Haki ya kuwasemehe ni sisi. Hivyo tunaomba tueleweshwe kama wanaomba msamaha au wanarudisha kwa kiburi wakisema pesa hiyo ni kitu gani kwangu kama huyo aliyelipa billion 10. Hayo ni majivuno na kuendelea kutuzarau.
Jamani accounts za Import Support ni mikopo ambayo inakuwa na repayment schedule. Kama mkopaji anakiuka mpangilio wa malipo basi kwenye contract kutakuwa na clause ya hatua ya kuchuliwa. Kmfn. kuuza mali ya mkopaji kufilisi etc.Hii hufanyika kisheria kama kupitia court broker and so on.Hawa jamaa watakuwa wamekiuka malipo kwa muda mrefu sana hivyo watu wa kuhusiswa kimahakama au kinidhamu ni mabenki/benki kuu yaani watumishi.Jambo la kuzingatiwa hapa ni kucharge proper interest rates for the whole period and if provision is there any penalities.
Nasikitika kwa watu kuanza kutoa pongezi na misifa wakati hata uthibitisho wa hii habari haujafanyika. Ndugu Dar es Salaam kwanza unatakiwa kuelewa ishu BOT kwa sasa pale ambayo ina watuhumiwa tayari ni EPA na si import support. Hiyo EPA ni wizi mtupu waliofanya hao jamaa maana the idea ilikuwa ni kununua madeni ya nje ya serikali na kampuni yako kulipwa madafu. Hao wezi walifungua kampuni hewa na kufaidika na mpango huo. Hivyo wamiliki wa makumpuni hayo, their BOT inside connections,RA, Benja na probably muungwana in short wote ni wezi!!!!!!!!!!!!!!!
Ushauri wa bure: Dar huwezi kumconvince mtu yeyote mwenye akili timamu na mpambanuaji wa mambo kwamba JK is serious in fighting corruption.
"Jamani wapi Balali tumemmiss kinoma au ndio tumeshamsahau baada ya richmond na Lowasa??????"
hii NI DHARAU TENA YA HALI YA JU.KWANZA MI NASHAURI WAKISHAMALIZ KURUDISHA HAYO MAHELA YETU UFANYIKE TENA UKAGUZI KUJA KAMA KWELI WAMERUDISHA NA HABARI ZITOKE KAMA MWANZO KUONYESHA KAMPUNI ZILIZOTUIBIA NA NGAPI ZIMERUDISHA NA HATIMAYE HAWA WTU WANA CHA KUJIBU KWA PILATO BWANO.Kuna namna moja tu mtu aliyeiba, akija na pesa au kitu alichoiba nakusema ndugu nilikuibia naomba unisamehe. Kama wamefika na pesa hizo na kuomba msamaha tujulishwe maana tulioibiwa ni sisi watanzania wote. Haki ya kuwasemehe ni sisi. Hivyo tunaomba tueleweshwe kama wanaomba msamaha au wanarudisha kwa kiburi wakisema pesa hiyo ni kitu gani kwangu kama huyo aliyelipa billion 10. Hayo ni majivuno na kuendelea kutuzarau.