Wezi waiba mtambo wa ATM Kenya

Wezi waiba mtambo wa ATM Kenya

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Tumezoea kusikia wezi wakivamia Benki na kuchukua fedha, lakini hii iliyotokea Nairobi Kenya ni ya tofauti kutokana na njia iliyotumiwa na wezi kuiba mtambo wa ATM ukiwa na fedha ndani yake.

Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi Nairobi Kenya limemkamata mlinzi wa Benki ya Equity akihusishwa na wizi huo ambao ulitokea mwishoni mwa wiki.

Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana mpaka sasa, unaambiwa wezi walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la kuhifadhi pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani. Washukiwa hao waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kufanya tukio hilo la wizi.

Akizungumza na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumika kukata chuma.

Chanzo: BBC
 
Dah! movie zingine zitapigwa marufuku sasa. Hii mambo ya The bank Job. kutoboa ukuta wa bank bila kugundulika na ku activate mitambo ta alarm na cctv sio kazi ndogo. Ila kama wameiba tu mtambo wa ATM na hawakuingia kwenye safe kuchota mpunga, watakua wametumia jitihada kubwa mno kwa faida ndogo.

Ila habari inasema kisanduku cha kuhifadhia pesa, nafikiri wanamaanisha safe.

Zile ATM mashine hazina uwezo wa kuhifadhi pesa nyingi sana, hapo hatujaweka kigezo cha muda wizi uliotokea, ambapo unaweza kukuta pesa tayari zilishapunguzwa na wateja.

cc The bold
 
Inabidi Mkuu The bold aandae story kuhusu hili tukio la kusisimua. Hakika limefanywa kiustadi sana.

Hongera wezi wa Kenya kwa kutumia akili nyingi sana.
 
Dah! movie zingine zitapigwa marufuku sasa. Hii mambo ya The bank Job. kutoboa ukuta wa bank bila kugundulika na ku activate mitambo ta alarm na cctv sio kazi ndogo. Ila kama wameiba tu mtambo wa ATM na hawakuingia kwenye safe kuchota mpunga, watakua wametumia jitihada kubwa mno kwa faida ndogo.

Ila habari inasema kisanduku cha kuhifadhia pesa, nafikiri wanamaanisha safe.

Zile ATM mashine hazina uwezo wa kuhifadhi pesa nyingi sana, hapo hatujaweka kigezo cha muda wizi uliotokea, ambapo unaweza kukuta pesa tayari zilishapunguzwa na wateja.

cc The bold
Mkuu kwa kukadiria kiasi ambacho ATM machine moja inaweza kubeba $200,000. Sasa hapo ni kiasi gani Cha pesa kimebebwa?
 
Kwa haraka haraka hauwezi kupata jibu sahihi kwa sababu kuna vigezo vingi sana vinavyochangia idadi au thamani ya pesa inayowekwa kwenye mashine moja ya ATM.

Kutegemea na aina ya ATM mashine na muundo wake pamoja na benki husika wameziwekaje zile cassette za kutunzia pesa, ATM nyingi zina cassette nne, sasa hapo inategemea wapeprogram note za aina gani? Namaanisha denomination kwa mfano, 100, 1000 n.k Kumbuka kwa kumbukumbu zangu Kenya noti yao kubwa kabisa ni ile ya KShs 1000.
 
Kenya hakuna fursa za kumiliki ardhi kwa kilimo au ajira binafsi ndiyo maana imebaki raia wapige bongo sana kufanya wizi na utapeli wa hali ya juu. Ardhi inamilikiwa na wachache na biashara pia ni za wageni kiasi wanaishia kuwa "machinga/madalali" wa bidhaa za nje kama colgate, sabuni ya imperial n.k

Si bure raia waKenya wanalilia sana mipaka ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ifunguliwe ili wapata fursa za kilimo, ajira na biashara maana Kenya nafasi hizo zimebanwa sana matajiri wachache wa ndani na makampuni ya kigeni.
 
No one killed or injured.............CHECK
No police chase......................CHECK
No trace left behind...........CHECK
Victimless crime....................CHECK

.

Well, 'good job'
 
Kenya hakuna fursa za kumiliki ardhi kwa kilimo au ajira binafsi ndiyo maana imebaki raia wapige bongo sana kufanya wizi na utapeli wa hali ya juu. Ardhi inamilikiwa na wachache na biashara pia ni za wageni kiasi wanaishia kuwa "machinga/madalali" wa bidhaa za nje kama colgate, sabuni ya imperial n.k

Si bure raia waKenya wanalilia sana mipaka ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ifunguliwe ili wapata fursa za kilimo, ajira na biashara maana Kenya nafasi hizo zimebanwa sana matajiri wachache wa ndani na makampuni ya kigeni.

i like the bongolala experts on kenya wakiwa tanganyika. kwa hesabu ndogo watu milioni 43 wanaishi kwa hewa kulingana na huyu expert on kenyan matters. i must like you a lot!! watu wanaoishi kwa hewa can have an economy bigger than bongo the land of honey and flowing milk kulingana na wewe. unatisha!!!

tanzania beggars wamezagaa kwa nchi ya machinga kuomba kutoka kwao. bwa hahahahaa!!!

1446294_2.jpg

Kisumo, a father of six and a beggar along Kenyatta Avenue in Nakuru town, lost his lower limbs.

He told journalists that poverty drove him from Tanzania, adding that although he has knowledge in leather work, he has no capital to start a business.
Kisumo, a father of six and a beggar along Kenyatta Avenue in Nakuru town, lost his lower limbs.

Na bado nitakujazia page baada ya page hawa wamejaa hapa kenya mpaka vijijini. huyu ni sample tu!!!!
 
Kenya hakuna fursa za kumiliki ardhi kwa kilimo au ajira binafsi ndiyo maana imebaki raia wapige bongo sana kufanya wizi na utapeli wa hali ya juu. Ardhi inamilikiwa na wachache na biashara pia ni za wageni kiasi wanaishia kuwa "machinga/madalali" wa bidhaa za nje kama colgate, sabuni ya imperial n.k

Si bure raia waKenya wanalilia sana mipaka ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ifunguliwe ili wapata fursa za kilimo, ajira na biashara maana Kenya nafasi hizo zimebanwa sana matajiri wachache wa ndani na makampuni ya kigeni.

Hivi Tanzania biashara zinamilikiwa na akina nani?
 
Back
Top Bottom