da irritant boy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2013
- 402
- 444
Ilikuwa ni mwaka 2017 nikiwa naishi mkoa wa Morogoro wezi waliiba laptop tatu , mbili mpya na moja ya kwangu ya mda mrefu
Nikiwa mkoa mwingine nilipigiwa simu kuwa dirisha la chumbani kwangu limetobolewa sikuwaza kabisa kuwa naweza kuwa nimeibiwa kitu nilihisi ni wale jamaa wa kuiba simu dirishan, na pia nilitumiwa picha za tundu lile na baada ya kuliona nilijiaminisha kuwa computer haziwez kuwa zimeibiwa kutokana na udogo wa tundu lile
basi nilirejea siku iliyofuata nakukuta nimeibiwa laptop zangu, na kwa namna nilivoziweka na umbali kutoka dirishan vilinifanya nizid kuchanganyikiwa zaidi, sikuwa na namna zaid ya kwenda kuripot polisi na nikapewa mpelelezi, upelelezi uliendelea kwa takribani wiki mbili bila mafanikio,
cha kuumiza zaid ule upelelezi nilikuwa nikitoa pesa zangu mfukoni kwa mambo madogo madogo, kuna siku mpelelezi aliniambia kuna genge la wezi wa computer limekamatwa na store yao ipo chalinze itabid nigharamie tuende nae huko ili nikatambue kama naweza kupata computer zangu, nilihangaika na upelelezi bila ya kuzaa matunda. hapo zishapita zaid ya siku 34 baada ya tukio
MUNGU nisamehe sasa nikashauriwa niangalie upande wa pili kwa WATAALAM,
kilichokuwa kinanifanya nihangaike namna ile ilikuwa kati ya zile computer zilizoibiwa mbili niliagizwa na ma lecturers wa chuo kikubwa hapo mjini Morogoro, na walinipatia 1.6m, na hapo nilikuwa nshaanza kuingia nao mgogoro ila niliwaeleza japo haikuwa rahisi kuelewa na kuvuta subira ila walinielewa na nilikuwa nikiwapa updates
mtu alienishaur kufanya hivi alikuwa ni mama mwenye nyumba wangu, na alinipatia namba ya bibi mmoja ambae alinielekeza namna ya kufika kwake, na kwel siku iliyofuata nilianza safar kuelelea sehem moja inaitwa kiloka, nilifika pale na kumuelezea bibi hali halisi, bibi akasema nimechelewa sana kama ni computer zitakuwa zimefika mbali sana ila wahusika naweza kuwapata,
bhas haikuwa kazi ngumu kwan kuna dawa alinipa nikapake pale kwenye tundu la dirisha , na nyingine alinipa nikaweke kwenye maji na kunyunyiza kila kona ya nyumba na mlangoni pia nakumbuka aliniuliza kama kuna kitu chochote ambacho nimebaki nacho ambacho kilikuwa kimegusana na moja ya zile computer, nashukuru mungu nilikuwa na cd ya antivirus ambayo niliitumia kwemye zile pc mbili mpya zilizoibiwa ukiachana na ya kwangu ambayo sikuitumia ile cd,
ikabid niulizie atanichaj shingap kwa kazi yake akasema hawez kusema maana kuna kuweza na kushindwa ilinikatisha tamaa japo nilikuwa na iman legevu, nilimuaga na akaniambia baada ya kutumia zile dawa kesho yake ni rud na hiyo cd
nilirejea nyumbani na kufanya kila kitu nilichoelekezwa na kwakwel ule usiku kwangu ulikuwa usiku mrefu sana kwan nilikuwa nikiota ndoto za kutisha ya kwanza niliota kitu cha ajabu kinakwarua dirisha mpaka nikastuka kuchungulia dirisha, sikuona kitu chochote na kulikuwa kumetulia sanA hapo ikiwa ni kama saa nane usiku, baada ya kama dakika 30 nilipitiwa na usingizi safari hii nikaota kama mtu ananyonga kitasa kwa nguvu sebuleni, na vishindo kama anaondoka, nikashtuka tena hapa ikiwa ni saa 10 na nusu , dah usingizi haukuja tena
asubuh baada ya jua kutoka nilimpigia simu yule bibi, na akapokea akiwa na furaha sana na kuniambia niende asubuh ile ile kwan matokeo yamekuwa mazuri, na pia alinisisitizia ili kazi ikamilike niende na ile CD nlosema ntampelekea, kweli nikajiandaa na kuanza safar kuelekea kwa bibi, kweli nilifika na kusalimiana na bibi kisha akaniambia tusipoteze mida simama tangulia kwenye kile chumba akinionesha chumba ambacho kilikuwa jiran na kilionekana kuwa na pazia tuu bila ya mlango,
kwenye kile chumba alichukua kitambaa cheupe na kupaka dawa fulan kwa mtindo wa madoa madoa mengi yaliyo kwenye mistari na kukining'iniza ukutan kama kakibandika hivi, kisha akachanganya nyingine ya unga nakuniambia ninywe, aiseee ilikuwa chungu ila ndio hivo lazima ninywe hapo nisijue nn kinakuja na uoga ulianza kunipata, hasa baada ya bibi kuziba kidirsha kilichokuwa kinaingiza mwanga ndan ya chumba kile
kisha akaniambia nitazame pale kwenye kitambaa kwa umakini, nilikodolea macho kile kitambaa kwa dakika kama nane nkaanza kuona kizungu na kama nataka kuzimia ila nlijitahid kukazia macho, mawenge yalizid na kile kitambaa kikaanza kuwa cheusi kabisa na yale madoa yakapotea kwa mbaali nkaanza kuona kama watu watatu wanasogelea makazi yangu ila sura nilikuwa sizioni vema kutokana na mawenge, baada ya kusogea mmoja alitoa funguo na kufungua kitasa kama vile ni muhusika, wote wakaingia ndani na kuanza kukagua ndio wakachukua laptop zangu wakaweka kwenye beg kisha kama wakaanza kujadiriana kwa dakika kadhaa ndipo wakatoka nje wakafunga vizur kisha wakazunguka dirishan, na kuanza kutoboa dirisha kama ushahidi na hapa ndipo kwa shida nliweza kutambua sura zao kasoro mmoja aliyekuwa mweusi sana kwa sura
machozi yalianza kunitoka na nguvu zikaniisha na hapo nkaona giza na kuanza kuhema kwa nguvu, yule bibi alifungua lile dirisha na mwanga ule ukanifanya faham zangu zirud,,,,,,, nilipatwa na hasir na uchungu kwa pamoja kwan sura ya mtu niliemuona ni mtu wa karibu kabisa na mm na huwa namwachia makazi yangu anafanya ufuska wake nikiwa mjini moro na ni mtu ambae dah, nilimuamini sana kwan kila kitu, na mambo yangu aliyajua hadi mipango yangu, yan nikisema kila kitu nimemaanisha.
na siku naondoka kabla ya tukio niliondoka na funguo yangu na hapo kat hatukua tukionana ila tulichat na hata baada ya tukio alikuwa mtu wangu wa karibu kunishauri nisikate tamaa, ila hii issue ya kwenda kiloka nilimficha kwani mama mwenye nyumba alinishaur nisimwambie mtu mwingine.
bibi akaniambia jikaze ww mtoto wa kiume, nadham ushawaona wezi wako sasa turahisishe kujua hivo vitu viko wapi, alichukua ile cd kisha akachanganya na madawa yake kisha akaichoma moto ikawaka na kuanza kutoa moshi, aliongea maneno nisiyoyaelewa na kisha kuniambia mali nilizoibiwa haziko pamoja na hazipo ila hii moja nayoiona itaelekeza nyingine zilipo kupitia hao hao wezi wako,
uzuri ni kwamba wez wangu niliwatambua wawili kasoro mmoja kwa sura, na bibi aliniuliza nkamwambia nawajua wawili mmoja nimeshindwa kumjua, akasema kati ya hao uliowatambua achana na huyo rafiki yako wa karibu aliye na mali yako moja ni huyu mwngine. mwisho akaniuliza unataka tufanyaje hapo sasa maana nasikiliza kauli yako ndo ya mwisho.
nikamwambia kwa hapo bibi yangu inatosha kwani umeshanitatulia tatizo langu,bibi akanigeukia kisha akasema kwani wewe peke yako unataka kufanya nn, nkamuelekeza nachotaka kufanya akanielewa akasema ila yeye atakuwa amefanya kazi nusu nimlipe kiasi chochote ntachoona kinafaa kwa kazi yake, bas kwa kua nilikua na pesa kwenye simu nikaomba nimtumie kwa tigo pesa akasema hapana pesa nayotakiwa kutoa ni inayoshikika na kuna sehem natakiwa kuiweka mm mwenyewe nilietatuliwa tatizo, basi ikabid nisogee centre ya pale pale kiloka nikatoa 200k kwa wakala na kisha nikarejea na kufanya malipo na kisha kuanza kuelekea mjini
njia nzima nlijawa sana na mawazo na ukizingatia nilikuwa naendesha usafiri wa piki piki, lakini nilifika maeneo ya bigwa na nikawaza kwann nisitekeleze kile ambacho nilinena kwa bibi kule kuwa ndicho nitakachokifanya nkaona hapana, nilichonena kwa bibi ni kuwa nitakwenda moja kwa moja kwa yule aliye na mali yangu kwa kumshtukiza kisha nimuambie issue yao waliyonifanyia na kisha nimpigie rafiki yangu wa karibu nkiwa hapo kwa jamaa kisha aje nae nimueleze kisha wanieleze wamepeleka wap computer zangu.
akili nyingine ikaja kwamba wanaweza wakanibadirikia na au mambo yakaenda kombo bila usaidizi wowote, bhas akili ya haraka ikaja nikapaki chombo njia panda ya dar ya zamani pale bigwa, kisha nikatafuta namba ya yule mpelelezi niliepewa kituoni, nikampigia na kumuelekeza kuwa nawajua wezi wangu aliniuliza umewajuaje nkamuelekeza hali hali akasema serikali haimini katika uchawi, nkamwambia ndo maana nimekupigia ili unisaidie kama mdogo wako tukawakamate wale jamaa, nkamwambia posho ipo asijali, bhas nikampanga kila kitu, akanambia nimpitie yupo kota, bhas nikafanya hivo ila baada ya kukutana nae akataka tutumie gar yake piki piki yangu niiache pale kota,
nikakubariana nae na safar ya kwanza ilikuwa kwenda kwa jamaa wangu wa karibu, nikamtext nkawambia uko wap ndungu yangu kuna issue nataka nkuagize upeleke sehem, akanambia alipo bhas tukaenda na poti, bhas kufika pale pot akanambia nenda ukaongee nae kisha mm nakuja kwa mguu mpaka hapo mlipo, bhas nkaenda kwa jamaa angu na nkamwambia bana ofisin kuna laptop ya mteja inabid uipeleke kwa mteja nakupa namba, akasema poa twende zetu basi ukanipe hiyo machine, kabla hata hatujaanza hatua poti akamshika jamaa kiutan kabisa kama wanajuana akamwambia uko chini ya ulinzi na akatoa pingu akamvisha, tukaenda kwemye gar eneo hilo raia hawakuwepo wengi hvo hakukua na shuhuda,
jamaaa alianza kulalamika kwamba kafanya nn yeye hana kosa, bhas poti akamsachi akachukua simu akaniuliza kama nalijua jina la mtuhumiwa 2 nichukue ile simu nimtext kumuuliza jamaa yupo wapi, jamaa akajibu yupo geto kwake, bhas moja kwa moja safar ya kwenda geto kwa mtuhumiwa wa pili ikaanza mtuhumiwa wa pili alikuwa anaishi maeneo ya mtaa wa vibandani , tulikwenda mpaka mlangoni poti akaniambia shuka kaingie mm nakuja nyuma, nkatii maagizo nkaenda nkasukuma mlango ulkuwa haujafungwa, la haula nilichokiona sikuamini jamaa alikuwa na computer yangu anaangalia movie, kibaya hata windows alikuwa hajabadirisha ila alikuwa kaipiga stika kwa nyuma ya kioo. jaamaa alishtuka sana na hapo poti akaingia akampiga jamaa mkwala mzito kwamba anaenda kuozea jela, bhas nkakunja ile laptop na chaja yake, yan wez hawakuwa na huruma masikini waliniibia hadi chaja na hata kwenye maelezo yangu polisi skukumbuka kama zilikuwa na chaja mpaka hapa nlipoiona moja
poti bwana akanambia ntoe kamba kwenye moja ya viatu vya jamaa nkafanya hivo akamfunga ile kamba mikononi na kutoka nae nje hapa palikuwa na mashahid walioona tukio lile ,
bhas hapa ikawa imebakia bado mtuhumiwa mmoja ambae mm sikuwa na mtambua
wale jamaa walikuwa wanaongea maneno meng ila mm ilikuwa ni hasira tuu imejaa kifuani, safar ya kuelekea kituoni ikaanza poti akasema ss nyie naenda kuwafunga mpaka mtie adabu, ebhana eh bhas wale jamaa walianza kuropoka asee kuwa ile computer moja mpya huyu jamaa yangu wa karibu alimpa (mtuhumiwa namba 1) alimpatia mshikaj wake mwanachuo amuuzie kwa wanafunzi wenzie na bado hajapata mteja, kiukwel huyu jamaa alikuwa si mwizi na alikuwa anaogopa san swala la kupelekwa kituoni, baada ya hapo tukaanza kwenda kwa mshtakiwa wa tatu ambae sikuwa namfaham ila aliishi maeneo ya chamwino ccm kulingana na maelezo ya mshtakiwa namba mbili, baada ya kufika kwa mshtakiwa namba 3 yeye alisema alimpelekea computer fundi mmoja wa computer eneo la masika na huyo fund ni maarufu sana mitaa ya masika na anavuma kwa tabia za kuwaibia vifaa pia wateja wake anasema alimuuzia ile computer kwa 150,000
yani roho iliniuma sana yani computer nimenunua hela nyingi afu mtu anaenda kuuza kwa hasara namna ile ( sifa za computer ilikuwa intel corei 7, Ram 8gb, graphics card ilikuwa intel dedicated gfx 3gb, hard disk 750gb na computer ni mpya from shop), tulikwenda kwa fund na baada ya kufika moja kwa moja jamaa akaanza kusema oh mm sina makosa na computer niliiuza sijui kwa mwalimu mmoja, dah ebhana tulikwenda kwa yule mwalimu alikuwa anaishi kihonda mm na poti siti ya mbele watuhumiwa wetu nyuma.
baada ya kufika kwa mwalimu poti na fund walienda na kuongea nae kiisha akaleta ile computer ikiwa bado inamuonekano wa upyaaa, kisha poti akamuachia namba akamwambia aje kituoni kesho yake mwalimu hakuwa mbishi kwani alioneshwa na kitambulisho japo haitoshi kumuachia polisi mali yako kwan lazima pia awe na warranty ya kufanya hivo lakin ndio hivo.
safar ikawa sasa kwenda kwa mwanafunzi ambae alipewa computer mpya na mtumiwa 1 ambapo mwanafunzi nae alikuwa akiishi kwenye nyumba za mzee ayubu vibandan kule tulikomchukua mtuhumiwa 2, fundi aliachwa na aliambiwa kesho alipot kituo cha polisi, kwend tulifika kwa mwanafunzi kisha tukachukua ile computer na sasa mali zangu zikawa zimekamilika bila ya kasoro yoyote.
nikajua bhana poti atawaachia wale jamaa la hasha, mm aliniacha nyumban kwangu kisha akasema ngoja awapeleke jamaa wakapumzike lockup kwan watakuwa wamechoka na mizunguko, khee akawasukuma ndani kisha akarud, tuliongea akanambia hapa kilichobaki tuwajambishe jamaa kwa sabab kesi ilikuwa bado haijafungwa na kwel tukaanza kwa wazaz wa watuhumiwa , ebhana hii siku niliiona ndefu sana ila nilikuwa nafuraha, nilimuachia poti kuzungumza kwenye meeting na wazaz ebhana walijiingiza mtego.
wakakubaliana kutoa 250k kila mzazi ndio watoto wao waachiwe, na kesi iishe kiukwel mm nilikuwa tuu naomba yaishe ila poti akakasimamia ukucha, baaada ya mambo kukamilika tulikwenda kota nkachukua piki piki yangu tukaagana na poti. usiku huu ulikuwa wa furaha sana kwangu nilianza kuwaza kama wakishindwa kulipa na jamaa wakaenda jela mm ntajilaumu kwan mateso ya jela hata kama ulimpeleka mtu kwa chuki inafika wakat unaanza kujuta na kumuonea huruma.
bhasi usiku ule ukapita na kweli hela ilitolewa siku ya kesho yake yan naweza kusema sijui dawa zilikuwa zinafanya kazi wazazi hata hawakubisha hata chembe, ilitolewa 750,000 nkapewa mm poti nikamkatia 250,000 nikabakia na 500k
========MWISHO=======
*jamaa walitolewa ila mshikaji wangu yule wa karibu alihama siku hizi yupo iringa,
*yule bb nilimpigia kumshukuru kwa kunifanikishoa jambo langu.
*ni miaka mi 3 ss imepita na sina mawasiliano na bibi tena na hata namba nilipoteza.
*poti yupo ni rafiki yangu na huwa nna mpa madili ya hapa na pale
* nilikabidhi laptop kwa wahusika japo ilinipunguzia legacy yangu
*sijui yalishaje ya mwalimu na yule fundi.
note:
**sio kila mtu unaweza kumuanini, rafiki yangu kumbe alichongesha funguo ya kitasa changu
**uchawi upo ni ukwel japo kuna matapeli siku hizi
**pia mnisamehe kwa uandishi wangu kwani naweza kuwa nimechanganya mafaili kulingana na hii story ni ndefu sana na kuandika uvivu
TUKUMBUKE KUEPUKA KUSHIKANA MIKONO, TUNAWE KWA MAJI YANAYOTIRIRIKA NA SABUNI, KUVAA BARAKOA NA TUMIA SANITIZER KWAN TUNASHIKA SEH3M NA VITU VINGI
Sent using Jamii Forums mobile app