Wezi wavunja Kanisa wala Mikate ya Sakramenti na wanywa Divai katika Kanisa la ACK Kenya

Wezi wavunja Kanisa wala Mikate ya Sakramenti na wanywa Divai katika Kanisa la ACK Kenya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Taharuki imetanda miongoni mwa waumini wa Kanisa la Anglikana (ACK) St. Matthew’s Mutithi lililopo Kirinyaga nchini Kenya, baada ya watu wasiojulikana kuvunja na kuiba mali ya kanisa, huku wakinywa divai ya madhabahuni na kula mikate ya sakramenti.

1748330632961.png
Tukio hilo la kusikitisha liliripotiwa na wanakwaya wa kanisa hilo waliogundua kuwa kibodi ya muziki ilikuwa haipo. Makamu mwenyekiti wa kanisa hilo, Eliud Githaka, alithibitisha taarifa hiyo na kueleza kuwa waligundua pia vitu vingine muhimu vimeibiwa.

Inadaiwa kuwa wizi huo ulifanyika wakati mlinzi wa usiku akiwa kazini, lakini hakugundua lolote hadi kesho yake. “Tunadhani alikuwa amelala, kwani hakuonyesha dalili zozote za kufahamu kuwa kanisa limevunjwa,” walisema baadhi ya wakazi kwa masikitiko.
 
Daudi pia alifanya kama hivyo. Ni njaa hiyo sioni Kama kuna dhambi hapo Kama hawajaiba chochote
 
Back
Top Bottom