What a mess at Mkapa Stadium!

What a mess at Mkapa Stadium!

Mario Kejob

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
441
Reaction score
536
Tatizo la wapenzi na mashabiki wa Simba kutoweza kuingia uwanjani kutokana na malfunction ya mfumo mpya wa ulipiaji wa tickets kwenye uwanja huo limejirudia tena leo na kuwafanya mashabiki wengi kurudi nyumbani bila kuangalia mchezo wa Simba na Biashara- Mara mubashara.

Kwa mara ya mwisho tatizo hili lilijitokeza siku ya Simba Day ambapo mashabiki wengi wa Simba walishindwa kuingia uwanjani hapo na hivyo kushindwa kuujaza uwanja huo kinyume na ilivyo tarajiwa.

Kama tatizo ni technical glitch ambayo ilishindwa kutatuliwa kwa muda wote huo, imefika wakati sasa wa kuwa na plan B ready available yanapotokea matatizo kama hayo iwe ni glitch au power outage ya kuuza manual tickets ili washabiki wahudhurie pambano hilo na sio kulikosa kabisa. Ikumbukwe kuwa washabiki wanatoka mbali kuja kuangalia mapambano hayo na wakiwa wametumia muda na pesa zao hatimae kuambulia patupu.

Wahusika wajipange suala hili lisijirudie tena kwani linavikosesha vilabu mapato na hivyo kuwa- discourage washabiki hao kuhudhuria mapambano mengine yanayokuja kutokana na usumbufu wanaoupata. Yaelekea mfumo huo haukufanyiwa majaribio ya kutosha.

You owe an apology to the Simba fans and other soccer lovers who couldn't attend the game for reasons mentioned above.
 
Hawa jamaa wanaanzisha mifumo bila kujipanga ni kama mwendokasi mpaka leo mashine hazifanyi kazi
 
Back
Top Bottom