hata mimi nahisi hili. Uchumi wetu unahitaji kusahihishwa au kujisahihisha kwani ulivyo sasa ni unsustainable. Swali litakuwa ni maumivu kiasi gani yatatokea ili tutoke hapa.
...Kuna mambo mengi sana yanayochangia uwepo wa hali hii, ambayo ni mbaya na itakayotupeleka pabaya zaidi ya hapa, huu ni mwanzo tu.
...Pamoja na kuwa na baadhi ya sera ambazo ni nzuri na hazisimamiwi au kutekelezwa, kwa kuwa watu wakubwa wanataka kutolipia gharama au wanapenda bure, tumeshindwa kuweka sera nyingine za maksudi ambazo zingeleta nafuu kubwa kwa uchumi wetu. Mathalani, kupunguza utegemezi na ununuzi wa bidhaa kadhaa toka nje ambazo kuna uwezo uliopo au unaoweza kujengwa wa kuzizalisha nchini. Ziko nyingi, unaweza kuzitambua.
...Kuna kansa kubwa ya kutowajibika, kutumia akili, na kufanya kazi yenye tija na inayoleta maendeleo kwa taifa na kunufaisha wananchi. Watu hawafikirii kuendeleza miundombinu; bahati nzuri tunaijua. Hawafikirii kuendeleza raslimali watu; ambayo kwa dunia ya leo ndio tegemeo kuu la nchi yeyote. Huwezi kuwa na uchumi mzuri kama watu wako hawana lishe, elimu hitajika ya kujikwamua kimaendeleo, afya yao ni mgogoro na hawajatulia kuweza kuzalisha mali. Kila siku wanahangaika kutafuta chakula, kwa kufanya hili, kuliacha na kufanya lile na kutopata faida yeyote.
...Nchi yeyote yenye kuhitaji kujikwamua kwenye umaskini, lazima iwe na viapaumbele vikuu vichache kwa wakati na mtazamo unaolenga kulikwamua taifa unaotekelezeka na wenye kusimamiwa, na sio maneno matupu yasiyo na mantinki kiutekelezaji. Mathalani, umeamua kupunguza umaskini, je?, ni mambo gani yanayowaletea umaskini watu wako? Ni elimu? Ukosefu wa ardhi? Kutokuwepo viwanda? Ugumu wa kupata mikopo; na sio mitaji, kwa maana tunayo mingi, kilichobaki ni kujua namna ya kuifanya iweze kutumika. Au, ni ukosefu wa chakula? Je, miundombinu ndio kikwazo? Maana, tumeona jinsi ukosefu wa umeme na barabara mbovu jijini Dar zinavyokwamisha shughuli za uzalishaji, biashara na maendeleo.
...Sasa, hivi vitu vyote vinahitaji uongozi makini, usio na ubinafsi au ulafi na unaopenda utaifa wake kwa vitendo. Kama kiongozi, unahitaji kufahamu matatizo ya watu wako, kujua au na kutafiti nini cha kufanya, kwa wakati gani, kwa kuwatumia kina nani na kwa gharama gani. Kazi kubwa ya kiongozi ni kusimamia na kufuatilia matokeo ya mwisho. Wajibu wake mkuu ni kuona mambo yanaenda sawa, kama ilivyotegemewa.
...Tatizo kuu la uchumu huu ni matumizi makubwa, yanayohusisha fedha za kigeni. Uzalishaji mdogo wa ndani na uagizaji mkubwa wa mali toka nje. Hivyo, hata kufanyike nini, shillingi itashuka thamani kila siku. Majuzi, sera ya fedha imetumika kupunguza makali ya kushuka thamani shillingi. Hata hivyo, hii haitafua dafu, kwani mhalifu ni sera ya matumizi na mapato. Matumizi makubwa kuliko mapato. Hatari zaidi ni hela chafu kusafishiwa kwenye uchumi huu ulio hoi; kunakuwa na ongezeko la matumizi ambayo hayatokani na mapato ya uzalishaji katika uchumi huu.
...Watu wamelala, wanahitaji kuamka na kutekeleza majukumu yao; tatizo ni kama wataamka mapema vya kutosha.