Roulette
Kwenye thread ya mwaka juzi nilisema nampango wa kusoma vitabu 12, hebu ngoja nione kama vilifika. Kwa kawaida napenda sana adventure books .
1.
the time machine-ni fiction, ni kitabu kizuri kinachojaribu kuelezea evolution kwenye mtazamo wa use and misuse. Kinaelezea jinsi wasionacho wanaweza wageuka walionacho. Ni kizuri sana japo cha zamani.
2.
king Solomon mines- hiki wengi mnakijua, macumazahn!.
3.
The hobbit- niliona kusubiri movies kuta ni frustrate nikaamua nipige kitabu yaishe.
4.
The game of thrones (the song of ice and fire)- ni series ya vitabu vitano, ni kizuri sana hasa sehemu za tyrion (wengi mtakuwa mmeona series yake)
5.
Animal farm- kitabu cha George orwell- kipo kwa mtindo wa kuchekesha ila kina maana pan asana, kinaelezea jinsi watu wanaweza struggle pamoja na baadae kusalitiana baada ya mafanikio. Kizuri sana viongozi wa upinzani wakisoma.
6.
Dune- hii ni series inahusu space adventure,ecology, science fictions na politics . ni kama vitabu 18 vingine kaandika baba(frank albert) na vingine mtoto wake.kuna watu cunning sana humo. Nimesoma vitabu kama 10.
Baada ya kusoma sana vya adventure nikajiuliza, Napata faida gani?. Nikaamua kubadilisha vitabu. Nikaanza kusoma social psychology (napenda psychology)
7.
Blink the power of thinking without thinking- kitabu cha malcom gladwell. Anaeleza jinsi ambavyo binadamu tunafanya maamumuzi bila kuwa aware kwanini tunaamua vile. Mfano bongo star search huwa wanatafuta mwanamuziki lakini unaweza kuta wakachagua mtu kutokana na uzuri, confidence au swagga bila wao kujua.
8.
Outliers- kitabu gladwell. Ni boonge la kitabu!. Anajaribu kujibu swali kwanini wengine hufanikiwa na wengine hushindwa. Anajibu why bill gate, why steve jobs, why Rockefeller why jews? Etc. mjasiriamali au kwa mzazi anaemtakia mema mwanae inabidi kusoma hiki kitabu.
9.
The tipping point- cha gladwell. – anajaribu kujibu. How and when epidemics occurs?.
10.
Predictably irrational- bonge la kitabu! . kinaeleza jinsi ambavyo tuko irrational katika decision making na mbaya zaida irrationality yetu ni predictable. Pia anazungumza jinsi makampuni yanatumia hiyo fursa kutuexploit. Kama wewe ni employer au mtu wa marketing inabidi usome hiki kitabu.
11.
Confessions of economic hitman-hiki ni kitabu serious sana kati ya nilivyosoma mwaka huu. Ni dizaini yakina snowden na assange. Jamaa anaeleza jinsi WB na IMF zinasaidia mabeberu kutuexploit. Ukisoma hiki kitabu kila ukisikia WB utakuwa unahuzunika. Zamani nilikuwa nadhani USAID ni shirika la misaada humo ndo nikajua na kirefu chake!. Ningependa wabunge kabla ya kuingia bungeni iwe sharti kukisoma.
12.
Nilivyoenda kuzimu na kurudi tena duniani- ni kitabu cha P. kaskasi. Kinazungumzia uchawi na habari za kuzimu. Nimesoma part one natafuta part two.
13. Yeremia, Ayubu na Ezekia navyo si ni vitabu!?.
Saa hizi nasoma BRIEF HISTORY OF TIME cha Stephen Hawking