Kama badiliko kwa sisi wanaume liwe ni kubeba mimba tuu basi
itakuwa kasheshe, kwasababu uanamke siyo kuwa na uterus tuu.
Ni mambo mengi sana yanayofanikisha kuwa mwanamke, Kuanzia
ubongo,maumbule n.k.
Kwa mfano ubongo wa mwanamke uko mahiri kufanya vitu vingi
kwa wakati mmoja sasa kama sisi kitu kidogo tuu kama kuongea
kwenye simu ni lazima tupunguze sauti za tv au redio kwasababu
hatuwezi ku-process mambo mengi kwa wakati mmoja ndo tutaweza
kudeal complex task kama kubeba mimba? Usione tuu wanavyo
pendeza, hawa ni complex design, everything about a woman is a
miracle.
Hebu fikiria mjibaba anabeba mimba wakati waist to hip ratio yake
ni 1:1 sasa atawezaje kutembea akiwa na mimba? Maungo ya
mwanamke ni mapana kwenye nyonga ili mtoto aweze kukaa vizuri
wakati yeye mwenyewe aweze kufanya shughuli zake za kawaida,
kama kutembea, kukaa n.k.
Wewe KakaJambazi naona hutupendi sasa hilo hilo la kuwatokea
wanawake linatutosha hayo makopleksiti mengine ya kubeba mimba
waachie hao wenyewe.