Wilbert1974
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 1,632
- 481
Sina uhakika ka watoa ajira serikalini wanafahamu vyema kuhusu hii kitu nchini
PPP (Public Private Partnership) kuna hiki kiini macho ka si kiini yai inasemekana kipo hapa nchini.Inachonishangaza inakuwaje mwajiriwa wa Private anapotoka huko na kuajiriwa serikalini Public kwa kazi ile ile ambayo alikuwa anafanya huko Private; akiingia serikalini anaanza na ngazi / cheo na mishahara ya mwanzo kabisa wakati alikuwa ni mzoefu sana tu wa hiyo kazi? Na wakati mwingine unakuta alikuwa analipwa kwa mshahara wa serikali wa juu, leo kaingia serikalini jina lile lile na kazi ile ile, iweje analipwa mshahara kiduchu!? Ina maana hata hazina wanashindwa kutambua kuwa huyo ni mtu ni yule yule iweje analipwa tofauti tofauti; yaani miaka inavyosonga ndo mshahara unashuka, badala ya kupanda! Mi naona hili nalo ka nia ajabu
Sioni uPartnership wowote!Halafu wataalamu wakiamua kuvujisha ubongo brain drain nchini mnaanza kubwabwaja! Au nasi tuanze mkakati ka walimu ndo mtuelewe jamani
Ngoja na wahanga wa hii kadhia nao waje waweke mawazo yao
.