What is really behind GNLD, Forever Living product na Sungreen?

Niwemugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
902
Reaction score
462
Hivi kwa nini hawa wauzaji wa dawa za virutubisho kama GNLD, Forever Living product na sasa hivi kuna hawa wapya wanajiita Sungreen wanapotoa matangazo yao hawawi wawazi mfano utasikia wanakukaribisha sijui kwenye mkutano wa kimataifa utafanyikia Ubungo Plaza ama sijui Millenium Tower lakini wanaishia kusema kwamba ni mkutano wa kuvumbua vipaji na kutengeneza nafasi za kupata pesa ukiwa holday ama ukiwa umekaa kwenye kochi nyumbani.

Swali langu la leo ni hili, hivi hawa jamaa ni wababaishaji kiasi kwamba inabidi wawaite watu kwa lobbying maana wanaamini kuwa wakisema kwamba ni issue za product zao hawataenda, ama hawa jamaa ni kikundi cha watu wanatoa sumu kwa waTanzania wenzetu.Yaani in short nashindwa kuelewa kwa nini wanashindwa kuandika with confidence kwamba ndugu mteja tunakukaribisha kwenye kikao cha product za GNLD, Forever Living product au Sungreen kitakachofanyika Millenium Tower siku ya tarehe 17/08/2013? Kwa nini wanashindwa kuwa wawazi ina maana wanachokifanya siyo halali ama ni ujinga wao tu.Na wote hakuna mwenye akili hata mmoja yaani ukijiunga huko utafikiri waasi wa M23 hakuna anaetaka kuwa muwazi kwenye matangazo yao SHIDA NI NINI HASA
 
goshhh, hii thread nimeipenda, japo nakiri kuona na kukutana na ajira nyingi kutokana na hizi kampuni za kimataifa za kimachinga, lakini huduma zao na uhakika bado ni swala la kubahatisha tu. kwasababu wanachokifanya ni kutoa mawakala wanaojua ku-rapu tu na wakati mwingine wanakuwa kama ze comedy, na hawaachi kuomba radhi wateja wao hasa kwenye mabasi kila siku kwa kujua kwamba baadhi wanakereka na makelele. binafsi nadhani ndio soko huria lenyewe. dah! nashawishika kuhisi kuwa haya makampuni nadhani yanawaibia watanzania, sana tu.kuanzia kodi, n.k. hawa mawakala wao wanalazimisha sana kuuza vitu vyao kuna wakati unajikuta unanunua tu kwa kumuonea huruma muuzaji kwa jinsi alivyo-rapu wakati akitangaza.
 
sio siri wanaboa maana hata wanachokifanya sikioni daaaah nimewahi kutumia dawa zao wizi mtupuuuu
 
sio siri wanaboa maana hata wanachokifanya sikioni daaaah nimewahi kutumia dawa zao wizi mtupuuuu
pole wewe, binafsi huwa siwaamini kwa jinsi navyoelewa dawa na magonjwa mbalimbali,mawakala hawa wanakatabia kakulazimisha ugonjwa na dawa hata kama wanajua haitibu, ukichunguza baadhi ya chupa zao zimeandikwa ki-china.na mawakala wanaelimu ya std seven tu hadi from two. wanatumia mikwara ya kiingereza kama kusema kampuni lakimataifa-forever sijui nini ili kutidshia watu. funny how! hizi kampuni hazina wataalamu wanaoweza kufafanua matumizi sahihi ya dawa na aina ya ugonjwa. zaidi ya kubwabwaja kwa sauti na kulazimishia tu dawa na ugonjwa wowote. kimsingi mtu aliyewahi kufanya kazi hii anaweza kuwa mganga wa kienyeji akitaka, kwakuwa anajua namna ya kuwadanganya watu. ni bora kwenda hospitali, angalau utaweza kupata tiba sahihi japo hospitali nyingi siku hizi zipo kimauzo zaidi kuliko huduma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…