Injili ya Yesu Kristu haishii kifo tu pale msalabani Kalvari. Alifufuka siku ya tatu, akapaa mbinguni na yu mkono wa kuume wa Baba akituombea.
Maisha ya Mkristu siyo tu kuacha dhambi (mfano wa mauti), bali mtu huyo anapaswa kuendelea kutenda mema, akiwaongoza wengine nao waje kwa Kristu waonje uzuri wa neema, waone jinsi Bwana alivyo mwema.