Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
Tunaishi ili tujifunze yaani hapa Duniani tupo shuleni then ukifa unarudi nyumbani, kwahiyo unatakiwa ufanye Jambo kubwa ili hata ukirudi nyumbani (kifo) ukumbukwe milele.Natumaini hamjambo waheshimiwa.
Nimetafakari kwa muda mrefu sana, nini hasa maana ya maisha na kwanini tunaishi?
Maisha hayako fair kabisa, wako watu wasio na hatia wala ubaya, wenye roho nzuri kupitiliza na wameishia kufa katika umri mdogo tena vifo vya kikatili mno. Wapo watu wenye roho chafu kupitiliza na wanaishi miaka na miaka wakiendeleza ukatili huo.
Maisha yetu yamejaa matatizo, majanga, huzuni, presha bila kujali waliofanikiwa kifedha na ambao hawajafanikiwa pia.
Wengi wetu tunajitahidi kupambana kufanikiwa kifedha, ila hata baada ya kufanikiwa, kwanini bado kunakua na suffering na presha nyingine za maisha????
Kwa mifano hii michache huwa najiuliza, kwanini binadamu tunaishi???? What is the purpose????
Saa nyingine naishia kuamini mstari wa ni biblia ulioandika maisha ni ubatili mtupu..
Karibuni kwa maoni wadau.
Tofauti na hivyo ukifa utakumbukwa na familia yako tuu baada ya wiki moja washakusahau!! ipo mifano ya watu waliofanya Mambo makubwa hapa Duniani hao ndo waliishi.
Kuhusu ukatili, Kama nilivyoeleza hapo awali dhumuni la kuishi ni kujifunza sasa ukiwa darasani kuna wanaofaulu na wanaofeli hao wanaofanya ukatili wameshafeli
Maisha ya Duniani ni maisha mabaya kuliko maisha yeyote baada ya kifo ndo maana tumeletwa Duniani tujifunze ukifaulu utaenda kwenye level ingine ya maisha baada ya kufa ukifail inawezekana ukazaliwa Tena upya hapa Duniani Kama kiumbe tofauti yaani Kama ulikuwa unafanya ukatili unaweza ukazaliwa Tena Kama paka au mbwa au kenge!!!
Sent using Jamii Forums mobile app