What is the purpose of life? Kwanini tunaishi?

Tunaishi ili tujifunze yaani hapa Duniani tupo shuleni then ukifa unarudi nyumbani, kwahiyo unatakiwa ufanye Jambo kubwa ili hata ukirudi nyumbani (kifo) ukumbukwe milele.

Tofauti na hivyo ukifa utakumbukwa na familia yako tuu baada ya wiki moja washakusahau!! ipo mifano ya watu waliofanya Mambo makubwa hapa Duniani hao ndo waliishi.

Kuhusu ukatili, Kama nilivyoeleza hapo awali dhumuni la kuishi ni kujifunza sasa ukiwa darasani kuna wanaofaulu na wanaofeli hao wanaofanya ukatili wameshafeli

Maisha ya Duniani ni maisha mabaya kuliko maisha yeyote baada ya kifo ndo maana tumeletwa Duniani tujifunze ukifaulu utaenda kwenye level ingine ya maisha baada ya kufa ukifail inawezekana ukazaliwa Tena upya hapa Duniani Kama kiumbe tofauti yaani Kama ulikuwa unafanya ukatili unaweza ukazaliwa Tena Kama paka au mbwa au kenge!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maishq siyqelewi kabisa,hata hiyo akili tuliyopewa mwisho wa siku what for??sijui ujenge,uwe na afya njema mwisho wa siku vyote hivyo vina faida gani??

Tunaishi ili iweje,bado sijawahi pata hili jibu.
 
Dini zinajibu vizuri hoja hii kama wengine walivyokwishasema.

Iwapo mtu hana imani katika dini ni bora ainjoi tu kuishi, bila kutafuta sababu.
 
Hata sijui labda tupo ili kuonyeshana ufundi!.. mfano anachokifanya sahivi huko marekani dada yetu..😂
 
Mhubirib12:13

Baada ya hayo yote yaliyokwisha semwa bado kuna hili linalotakiwa: Mche Mungu, na uzishike amri zake; kwa sababu hilo ndilo jukumu aliloumbiwa binadamu.
 
Hakuna zawadi kubwa na ya pekee aliyopewa mwanadamu kama kifo.

Kifo kimetufanya tuwe na uwezo wa kupambana na mazingira yetu na kuja na gunduzi nyingi zisizo na kifani.
Kifo kimemfanya binadamu agundue namna ya kuugawa muda wake kwani hatimaye kuna ukomo wa kuishi.

Kupitia kifo mimi najua kabisa siwezi kuishi zaidi ya miaka 120, hivyo basi ndani ya muda huo napaswa kufanya mambo fulani kabla sijaondoka.

Hebu fikiri, najua ni ngumu sana akili ya mwanadamu kufikiria muda usio na ukomo(infinity), je, ungeishi hata miaka bilioni 300, ungekuwa unafanya nini?

Tusitishane!! najua kifo kinatisha hasa pale kinapowachukuwa wapendwa wetu lakini bado ni zawadi kubwa ambayo tumepewa ila hatuitaki.

Baadhi ya dini zimekuwa zikitaja kifo kana kwamba ni adhabu, mara zote kukumbushana kuhusu kaburi, hakuna sababu ya kufanya hivyo kwani kifo kamwe haitakuwa itokee kukwepwa na mwanadamu.

Tujifunze namna ya kukiangalia kifo kwa upande wa pili na kamwe hutaona kama kifo ni adhabu.
 
Umeongelea kifo vizuri sana mkuu...na yote uliyoyasema ni kweli... ila haijajibu hoja kwanini tunaishi... je tunaishi ili tu tufe??? Kama ndivyo, si ni bora tusingekuwepo kabisa tangu mwanzo?? Food for thought
 
Mhubirib12:13

Baada ya hayo yote yaliyokwisha semwa bado kuna hili linalotakiwa: Mche Mungu, na uzishike amri zake; kwa sababu hilo ndilo jukumu aliloumbiwa binadamu.
Hii ni kwa imani ya kikristu.. na wakristu hawafiki zaidi ya 30% ya population ya dunia. Je, hawa wengine 70% wasioamini ukristu ina maana wao hawana purpose ya kuishi??
 
We live in oder to eat.
 
The purpose of our existence

Acts 17:26-28
[26] From one human being he created all races on earth and made them live throughout the whole earth. He himself fixed beforehand the exact times and the limits of the places where they would live.

[27] He did this so that they would look for him, and perhaps find him as they felt about for him. Yet God is actually not far from any one of us;

Grow in wisdom and you'll find the purpose
 
Mungu aliiumba bustani ya Edeni yenye matunda mengi, matunda hukomaa na kuiva hivyo akamuumba Adam ili aitunze kwa kuyala matunda yaliyokomaa, matunda yalimzidi Adam bustani ikaanza kuchafuka kwa matunda yanayooza hivyo Mungu akamuumba Eva(Hawa) ili amsaidie Adamu kuitunza bustani, hata hivyo walizidiwa na kwakua walielekezwa wazae watoto ili walaji wa matunda wawe wengi na kuweza kudhibiti wingi wa matunda kuoza na hilo lilifanikiwa kuifanya bustani ya Edeni kuwa safi na kupendeza, hivyo ni wazi tunaishi ili tule na kumshukuru Mungu vinginevyo dunia ingekuwa chafu kwa matunda yaliyooza.
 
Ukisikiza sana motivational speakers waweza fikiri kusudi la maisha yako ni kua Rais, au waziri au daktari au kuinua wajasiliamali, kutetea wanyonge, mwanaharakati wa jinsia na haki za watoto etc! Brother and Sister kusudi la maisha yako ni ndani ya Kristo, linatekelezwa ndani ya na kupitia kanisa lako la mahali. Mengine hayo ni “carrier” tu na unaweza badili wakati wowote! Bado una nafasi ya kujipata utambulisho wako na kusudi la kuishi kwako ndani ya Kristo. Anza kufuatilia kwa karibu Kainosmedia kabla hujafukuza upepo maisha yote!

- Kainos Creation -
 
Uvivu katika study ya maandiko unafanya kukosa kuona kua maandiko yote yanazungumza mambo yale yale kwa lugha tu tofauti sababu ya gepu la wakati kati ya kizazi na kizazi inayopelekea gepu la utamaduni unaozalisha gepu la lugha na matumizi ya maneno! Ukiona Injili mbili au tatu, ukiona wokovu wa aina tofauti kwa mataifa tofauti, ukiona badiliko la mpango wa Mungu au kusudi lake katika vizazi tofauti basi ujue umekumbwa na hio hali. Maandiko yamejaa “synonyms”. Shauri na kusudi la Mungu ni moja kwa mataifa yote na vizazi vyote. Tuanzie hapo kwanza!

- Kainos Creation -
 
Kwanini uwe na siku nyingine zaidi duniani?
Kuwa na hela zaidi? Nyumba zaidi? Kuoa au kuolewa? Hakuna kati ya haya yenye umuhimu wa milele! Paulo alitupa ufahamu juu ya kusudi la maisha na kuishi.. “bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu. Nami nikitumaini hayo, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, ili mpate kuendelea na kufurahi katika imani;” Fil 1:24-25. Si kwa ajili yako binafsi bali kwa ajili ya wengine. Ina umuhimu wa milele!
Injili ya Kristo. Kwa nini unataka kuishi siku moja zaidi?

Kainos Creation
 

Bado haujajibu hoja, why are we here, what's the purpose.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…