Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim, Lipumba amesema, kitendo cha uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuzuia matokeo ya uchaguzi wa Baraza la vijana la chama hicho (Bavicha) na kuuahirisha uchaguzi wake, kinaleta tafsiri kwamba mtu waliyekuwa wanamtaka hakushinda.
Juzi Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, alisitisha kutotangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Bavicha na kuahirisha uchaguzi wake kwa muda wa MIEZI SITA, jambo ambalo limepingwa na Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.
Alisema kwa kawaida uchaguzi unapofanyika, matokeo lazima yatangazwe na si kuahirisha kutangazwa kwa matokeo kama walivyofanya Chadema.
Kama umeruhusu uchaguzi ufanyike na ukafanyika na kura kuhesabiwa, hapo huna sababu ya kutoyatangaza matokeo, ukifanya kinyume maana yake ni kwamba unataka kufinyanga demokrasia na italeta tafsiri kwamba yule uliyekuwa unamtaka ashinde, hakushinda alisema Profesa Lipumba.
Alisema hata katika chama chake, kuna matatizo lakini, hakidiriki kuficha matokeo ya uchaguzi na badala yake wanatangazwa na wasioridhika kukata rufaa.
Profesa Lipumba alisema ingawa hana uhakika wa taratibu za uchaguzi ndani ya Chadema, lakini katika mambo ya msingi kama hilo, chama kinapaswa kujikita katika kuheshimu na kusimamia katiba na kanuni za uchaguzi za chama.
Alisema wale wote wanaotuhumu matumizi ya fedha na kampeni chafu wanapaswa kuthibitisha hilo kwa ushahidi uliowazi, ili uongozi wa chama uweze kuwashughulikia wahusika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na katiba ya chama husika.
Tangu kuanza kwa maandalizi ya uchaguzi wa Chadema matukio, kumejitokeza matukio kadhaa yanayoambatana na vurugu za wafuasiwa wa Mwenyekiti wa sasa wa Chadema Freeman Mbowe na Naibu katibu mkuu wake, Kabwe.