Inasikitisha kuona Ghana ikiondolewa ktk dakika za mwisho. Hii si mara ya kwanza kwa timu za Africa kutolewa ktk robo fanali kombe la dunia. Ghana ndiyo time pekee ya Africa iliyoweza kubakia kabla ya kunyimwa goli na "FIFA" referee.
Swali la kujiuliza, kwanini timu za Africa hazifiki mbali ktk WC zaidi ya robo fainali? jibu, ligi zetu hazina mikiki ya nguvu kama ligi za wenzetu Ulaya, na South America. Kila mwaka tunaona timu zilezile zinawakilisha Africa. Soka ya Africa haichezwi kihalali kama za wenzetu Ulaya. Rushwa imezidi kwa mareferee, viongozi wa vilabu, National level, na viongozi wa CAF. Kila mwaka tunaona timu kubwa ndizo zinazochukuwa ubingwa. Kiukweli kabisa, Africa Chapions League inabenefit zaidi timu za West Africa na North Africa. Kila mwaka tunaona kabisa vilabu vikubwa vinapangiwa vilabu "vidogo" ktk mechi za ufunguzi ktk mechi za CAF, na Chapions League. Soka ni progress, ukicheza mechi ya kwanza, basi kuna uwezakano mzuri zaidi ktk mechi ya pili utacheza kwa uzoefu zaidi kuliko ile ya mwanzo.
CAF haina mikakati ya kuisadia Africia ktk mechi za kimataifa. Tutafute mbinu zingine zaidi za kuisadia timu za Africa, tuimarishe upinzani ktk ligi zetu za nyumbani ili tuweze kujenga wachezaji bora kama wenzetu South America na Ulaya. Is time for Africa to wake up, stop corruption in sports, and let's play fair game.