What is your favorite food?

What is your favorite food?

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Mi napenda sana!

1.Ndizi nyama
2.Ugali na nyama choma.
 
Ugali wa muhogo na Samaki(SATO) wa kupika.
Ugali wa muhogo na nyama iliyobanikwa na kupikwa.
Ugali wa muhogo na mboga mboga.
Ugali wa muhogo na mlenda, nyama kavu.
Ugali wa muhogo na dagaa wakukaanga afu wakapikwa.
Wali nyama
Wali maharagwe.
 
Mzee mimi napenda sana mandi...naweza kula ata sio size yangu
 
Ugali wa muhogo na Samaki(SATO) wa kupika.
Ugali wa muhogo na nyama iliyobanikwa na kupikwa.
Ugali wa muhogo na mboga mboga.
Ugali wa muhogo na mlenda, nyama kavu.
Ugali wa muhogo na dagaa wakukaanga afu wakapikwa.
Wali nyama
Wali maharagwe.
Ugali wa muhogo kwa ambaye hajawahi ni kazi sana,nilikuwa sijawahi but baadaye nikazoea kumbe wa ukweli sana
 
Ugali, mchunga wa nazi, na kipande cha papa kilichochomwa.

Kama pua zako ni sensitive umeula - LOL.

Tanga line mpooo?
 
Mchunga ni nini?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Kama upo Toronto bibie Farkhina, mchunga ni dandoline. Yale majani yanajiootea wakati wa Spring kwenye lawns na yana maua ya manjano. Kwa Tanzania (na pwani yote) haya ni majani yanajiotea yenyewe lakini ukiyachuma (kama dandoline) yanatoa utomvu mweupe. Ni majani machungu sana lakini yakipikwa vizuri (hasa na nazi) utayapenda.

Wagosi/wandee wa kaya saidieni hapa tuwajuze watu hii delicacy. Mkuu Jerrymsigwa mtu akipikiwa vizuri hii kitu na kuila basi amekwishaoa - LOL.
 
Tupikie basi siku moja tuje kula lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
samaki tilapia ugali and greens za aina yoyote
 
Back
Top Bottom