The Finest bana, mada kama hii kwa wikiendi ngumu kidogo, lakini kwa kuwa ni MUHIMU SANA tuijadili.
Kama alivyosema MR. Rocky hapo juu, tunatumia nguvu za ziada katika kuweka mikakati kabla na ndani ya uchumba. Hiyo ya kabla ya uchumba sio mbaya, kwani ni matayarisho yako to be Husband au Wife. Lakini ndani ya uchumba tunapoteza muda na pengine pesa. Kipindi cha uchumba kinadanganya. Mwanamume anajaribu kuficha umasikini wake, ataazima gari, atakopa ili wikiendi atoke na bibi. Mwanamke anaficha kasoro zake. Tunajidanganya na/au kudanganyana. Tunapotaka kufunga ndoa tunapoteza pesa nyingi sana matayarisho na siku ya arusi. Tunawakamu marafiki na familia zetu kwa michango mpaka zipatikane milioni 10 (Mikakati yetu ya kwanza ni fahari - Mwaka huu wanitambue: Send-off.kitchen party, mlo wa mchana, hall la usiku, chai ya bibi arusi, chai ya bwana arusi...siku tau au saba za arusi). Pesa hizo zingefaa kuanzia maisha.
Mkisha kuoana ndipo matambara mabovu yanafichuka: Kumbe mume hahehohe, sms zinaingia na kutoka kama mvua, kila mmoja anadai uhuru wake, ma-ex wanawasumbueni na balaa kama hizo. Kinachonishangaza ni kwa nini wazazi wetu walioozeshwa kwa kuchaguliwa wake/waume wameishi ndani ya ndoa mpaka kuona wajukuu na vitukuu, wakati sisi tuliochaguana, kukbaliana, kupanga strategies, baada ya miaka michache pengine miezi, tunawachana. Ile kauli ya "Pamoja kwa shida na raha, kwa uzima na ugonjwa mpaka kifo kitapotutenganisha", tumeigeuza kuwa "Pamoja kwa raha na uzima mpaka nitakaposhindwa kukuvumilia au mpaka talaka itapotutenganisha".
Kwa mawazo yangu, ndoa kama pingu za maisha, strategies zake kuu zipangwe mkiwa ndani ya ndoa, hasa strategy ya kudumisha mapenzi na ndoa yenu ili kudumu katika asasi hii hii adhimu.