...this hurts, ila the finest tayari umeshalijibu swali hili uliposema; "wengi sana wako katika hali kama hii lakini hawasemi kwa kuhofia wakiacha ndoa zao jamii itawaelewa vibaya"
...kwa mtazamo na maoni yangu, hali hii pia inachangiwa na tabia iliyoota mizizi kwenye jamii zetu za kibantu kwamba
mtoto wa kike akishaolewa, haki zake zote zinahamishiwa kwa mumewe, chochote kinachomtokea huko ni "majaaliwa" yake, sana sana ataambiwa avumilie...
hivi, mwanamke anazaliwa hapa duniani aje kuozeshwa, kuzalishwa, na kumnyenyekea mumewe tu?
kama una mtoto wa kike,---binti--- hapo nyumbani na unampenda, jiulize utamteteaje mwanao kwenye hali kama hii...
Mkuu, hapo nilipokuza, kukozesha na kupigia mstari, ninakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa, lakini udhalilishaji wa wanawake si tabia ya wabantu tu. Hata sisi wabantu tumeanza kubadilika. Wengine wanaona kama mabadiliko haya ni kuwalea vibaya wasichana, pale mama anapomwambia mwanawe m/mke arejee nyumbani, au anpomkemea mume kwa kumwambia "huyu ana kwao, hukumwokota jaani".
Udhalilishaji wa wanawake upo ulimwenguni pote miongoni mwa races zote - Waafrika weusi na weupe, waarabu, wahindi, wachina, wazungu wa mabara yote, na response ya wanawake wengi inakuwa kama hii ya Angela. Ni juzi tu rafiki yangu mzungu alinisikitikia mateso anayopata toka kwa mume wake - wivu, gubu, kisago - na bado anabakia kwa kisingizio cha watoto lakini ukweli ni kuwa anafikiri iko siku mume atabadilika.
Imefikia wakati, kwa takwimu nilizonazo za nchi moja ya Ulaya, wastani wa wanawake watano kwa mwezi huuliwa na waume au ex-wao, ukiwachia mbali ya maelfu wanaojulikana na wasiojulikana rasmi kesi zao; ukilinganisha na 1/45 ya wanawake wanaoua waume zao pale maji yanapowafika shingoni. Imefika wakati pia wanaume/wanawake wanavishwa vilinzi (GPRS) ili kuwakinga mahasimu zao wasiwasogelee.
Tatizo lipo kwenye mfumo dume, toka majumbani hadi serikalini. Angalau kwa nchi zinazoendelea wanajaribu kulipunguza. Mfano ni EU ambapo wamo wanaandaa sheria ya kuwasakama wanaume watesaji na wauwaji. Hata hivyo mitaani, bado mke akiteswa inaonekana kama ni stahiki yake.
Ninachowashauri wasichana wasimame wenyewao kujilinda na hii hali. Mkisubiri huruma ya mume, serikali na familia zetu, mtaendelea kuteswa. Ikiwa sula ni la watoto, watoto si wako peke yako. Na ikiwa ni tamaa ya kumbadilisha mume siku moja, kumbuka kuwa walishishashindwa wazazi wake kumbadilisha. AMKENI