Whats wrong with Kanye?

Hivi nini kinaendelea?
ni mental issues au kuna mengine?

nimeona kuna watu wanahusisha na Illuminati....
nimeona clip ya DMX....

Kanye West ana tatizo gani hasa?

Paulo Sergio De Souz Nyani Ngabu
BAK

Inawezekana kabisa kuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiakili na hata ya kihisia.

Kwa vile tu yeye ni nyota wa muziki, hiyo haimaanishi kwamba yuko tofauti sana na wengine.

Na yeye mwisho wa siku ni binadamu tu kama tulivyo binadamu wengine.

Halafu, kwa watu observant kama mimi, hilo la yeye kuwa 'volatile' hajalianza leo.

Tokea zamani yuko hivyo ila sasa ndo naona hiyo 'volatility' yake imeshika kasi.

Unakumbuka 2009 alipomvamia Taylor Swift na kumnyang'anya kipaza sauti na kuanza kutiririka kuhusu nani alistahili kushinda hiyo tuzo aliyoshinda Taylor?

Hiyo ilikuwa ni moja ya dalili alizozionyesha hadharani.


Kwa hiyo mimi naamini kabisa kuwa huenda ana matatizo ya akili na kihisia ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi muafaka.

Kuhusu Illuminati, mi nadhani hizo ni hekaya za Abunuasi tu.
 


Mimi nilimtazama live siku ile kuhusu Katrina...nilicheka sana siku ile...
kweli jamaa ana namna ya ku snap hivi....analipuka ghafla....
 
Huyu jamaa ujambazi aliofanyiwa mkewe kule Paris inasemekana umemuathiri sana kiakili. Halafu pia inadaiwa tangu ujambazi ule utokee hawajapata muda wa kukaa pamoja kama mke na mume kuzungumzia yaliyotokea Paris. Hivyo pamoja na usongo wa mkewe kuibiwa ving'aro vya thamani inasemekana jamaa halali pia sijui kama ni kwa kukosa usingizi au msongo wa mawazo na kuona marafiki zake hasa Jayz na mkewe wamemtenga.

Hivi nini kinaendelea?
ni mental issues au kuna mengine?

nimeona kuna watu wanahusisha na Illuminati....
nimeona clip ya DMX....

Kanye West ana tatizo gani hasa?

Paulo Sergio De Souz Nyani Ngabu
BAK
 
Mimi nilimtazama live siku ile kuhusu Katrina...nilicheka sana siku ile...
kweli jamaa ana namna ya ku snap hivi....analipuka ghafla....

Oh yeah...miaka 11 iliyopita.

Tayari hata hapo alikuwa keshaanza kuonyesha 'volatility' yake.


Halafu baadaye alikuja kumwomba radhi rais Bush.

 
Ngabu unajua wi hiyo hiyo ndo Time walimuweka kwenye cover?
halafu ndo akamshambulia Bush...dah
 
Namwonea huruma sana sana . ..duh
 
Ndo maana nasema kuna strong possibility kuwa jamaa ana matatizo ya kiakili na kihisia.

Wanasema wau wote ambao unaweza kuwaita 'creative genius'
au wanaofanya kazi zinazo wataka kuwa 'creative sana' ni rahisi kwao kupata magonjwa ya akili..

nimesoma sehemu leo jamaa huko hospitali anazungumza habari za kuingia studio still..hadi mkewe
hataki watoto wamsogelee
 
Reactions: MC7

Yeah...kuna taarifa kuwa Kimmy yuko concerned sana na hali ya watoto wao.
 
Oh yeah...miaka 11 iliyopita.

Tayari hata hapo alikuwa keshaanza kuonyesha 'volatility' yake.


Halafu baadaye alikuja kumwomba radhi rais Bush.

Tehehehe kama, Nimevutiwa sana na pozi la mtangazaji, hasa pale baada ya kusema "George Bush doesn't care about black people"
 
Reactions: MC7
Kanye ni mfano tu wa wasanii ambao wako under MK-Ultra mind control na hata hii skit ya yeye kuloose it hamna lolote waliona kwnye show kawaumbua wakubwa zake wakaona bora waseme kua ni kichaa in the mean time huko hospitali hatujui wanamfanya nn. Nakumbuka maneno ya Dave chapelle aliposema kua there is something wrong with hollywood. Kila msanii ana njia yake ya kudeal na his own deamons....mfano britney alijinyoa nywele,Kanye amerant kwnye stage badala ya kuperform. He just needs prayers.
 

Dave nae bangi sana....
 
Huyu mgosi simuelewagi kabisaaaaaa.... Jay z alimkurupua tu. Na hakupenda kuwa hapa alipo sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…