What's your morning ritual? / Nini ni ibada yako ya asubuhi?

kali linux

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,192
Reaction score
5,685
Hello bosses and roses...

Kuna mambo madogo madogo ambayo watu huwa tunajisahau lkn yana umuhimu sana kwa masaa 24 yatakayofuata.

Mfano mtu unaamka tu asbh hapo hapo unapiga mswaki na kutafuta usafiri uelekee kituo chako cha kazi lkn ukifuatilia ikifika saa tano asbh tyr ushaanza kuchoka na kuchukia siku yote iliobaki. Hapo utaanza kuhesabu masaa yaliobaki ili urudi kwako ambapo huko nako labda hukutandika kitanda asbh (kama ni bachela) au sebule ni chafu ipo kwenye mvurugano tu, au hata uwanja wa nje hujafagia. Ukirudi huko napo lazima uwe bored tu na asbh yake circle inajirudia.

Morning ritual au Ibada ya asbh sio lazima iwe ni sala, ni mambo kadhaa ambayo lazima uyafanye asbh, hii ukiifuata itakujengra discpline bila hata kujijua au kutumia nguvu kubwa sana. Vile vile unaweza kufanya siku yako iwe nzuri.

Mfano mdg tu ni kutandika kitanda chako na kufagia uwanja au kusafisha chumba au/na sebule yako.

Kwenye Taoism kitendo cha kufanya usafi asubuhi kina maana kubwa sana kiroho, sababu inakupa sense ya kusafisha takataka zote moyoni, rohoni na akilini. Ndo maana utaona monks wengi hufagia uwanja lkn kwa hisia sana sababu muda huo yupo deep kwenye meditation anasafisha akili yake, moyo wake na roho yake (kuondoa chuki, hofu zisizo na lazima, etc....)

Binafsi siwezi kuanza siku bila meditation, push up 200, sit ups 200, usafi kisha kusoma angalau page 10 za kitabu (hard copy). Baada ya hapo ndipo nitashika simu au computer, lkn kabla ya hapo hata akipiga simu nani siwezi kupokea mpaka nimalize morning ritual yangu. Nimefanya hivyo kwa mwaka na nusu sasa na ninahisi utofauti sana ukilinganisha na kpnd cha nyuma ambapo nikiamka tu ni kuoga kisha kazini.

So, what is your morning ritual?
 
We uko sawa na mimi tofauti kidogo sana !Namuomba Mungu aisimamie siku iende vyema.
 
Asubuhi ukiamka kabla ya chochote Anza kwa kuomba ukiwa peku huku unatembea ndani chumbani, unaninenea maneno mazuri...

Mf: Unajibariki miguu yako, unajiambia wewe ni mmiliki wa ardhi na na vyote...

Unajitamkia kuwa Mungu ulisema utabariki niingiapo na nitokapo...

Ulisema utabariki kazi ya mikono yangu...

Unashukuru..

Asante Mungu kwa kuwa ushanibariki ..

Yote kwa jina la YESU
 
Alisema atabariki kazi ya miguu yako🤔🤔
 
Yaani squarts 200? Unapiga reps ngapi kwa sets ngapi?
 
Nisikilizeni vizuri! Hakuna kitu muhimu kama kusali kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu uamkapo asubuhi kabla ya kufanya jambo lolote!

Omba baraka na ulinzi wa Mungu katika kila jambo unalokwenda kufanya. Pia omba juu ya wote utakaokutana nao na kushirikiana.

Usiku kabla ya kulala sharti umshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote alokutendea mchana kutwa. Omba ulinzi wa Mungu kwako, familia na wote uwapendao.

Furahia jambo hili kila siku bila kukosa na utakuwa na maisha bora sana.


We uko sawa na mimi tofauti kidogo sana !Namuomba Mungu aisimamie siku iende vyema.

Nadhani tuko wengi hapa

usiache kupokea simu asubuhi

sometime kupokea kwako simu kunaweza kuwa zaid ya ibada kwako au kwa mwingine


Vip gorofaaa lako limeishapigwaaa rangiii....?
 
Amen 🙏🙏
 
Yaani squarts 200? Unapiga reps ngapi kwa sets ngapi?
Sio squats, nimesema sit ups 200 na push ups 200.

Vyote huwa naenda set ya 20 20 kwa kuchanganya, yaan 20 pushups kisha 20 situps, hio ni kwa upper body. Ila round 10 za mwanzo naenda speed sana.

Kwa lower body sana sana nafanya lunges round 5 za 20, 3 times a week minimum.

Fanya hvo kila asubuhi kisha piga cold shower utasikia raha siku nzima
 
Amen
 
Yote hayo ni part ya meditation kama nilivosema hapo juu
 
Ngoja niichukue hii, ujue nilivosoma sit ups nikajua kama squarts kumbe ni ile ya kukaa na kusimama. Haidhuru mgongo?
 
Baada ya kuamka asubuhi ni sala kwanza, kutandika kitanda kisha kupiga bafu na kusepa, maandalizi ya mavazi na vitu vingine vya kazi huwa navifanya kabla la kulala ila kupunguza vipengele asubuhi

Sijajua unaishi wapi mkuu ila itakuwa ama unaamka asubuhi sana, huishi mbali na eneo lako la kazi/umejiajiri ili kuweza kufanya vyote hivyo asubuhi

Si wengine tunaskip vipengele vingi hivyo asubuhi maana usafiri wenyewe ni mtihani, hivyo lazima ukapambanie usafiri vinginevyo kuchelewa job itakuwa ni daily
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…