WhatsApp: Jumamosi ijayo kuwa siku ya mwisho ya watumiaji kukubali masharti mapya

Wanadanga eti masharti haya mapya hayawahusu watumiaji waliopo Ulaya lakini sote tunaendelea kukumbushwa kuhusu mabadiliko hayo.

Kimsingi binafsi nimelazimika kufuta hata Facebook kwenye simu yangu mara baada ya IOS 14.5.1 kuanza kutumika kwasababu Facebook walitaka kunilazimisha kukubali wanifuatilie wanavyotaka.

Facebook imepoteza muelekeo kwa namna ambavyo wanatumia taarifa za wateja wao kwa manufaa yao bila kujali haki za msingi za kulinda taarifa husika
Nasubiri muda ufike tu naondoka whatsapp
 
Acha upumbavu wewe....privacy ni jambo la msingi. Hata chumbani kwako penyewe unafunga wakati unajua huna cha kuibiwa .
 
Kwanini wamexempt Ulaya, hawa jamàa sio watu poa.
 
Tofauti yetu nn sisi hatujakataa au nn shida ,kwamba wezetu ulaya na ujeruman wao waendelee na mambo yao kawaida ila sisi hapana.kazi wamekosa Facebook!

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Mi sina account ya FACEBOOK, kuna tatizo gani hapo

Haijalishi bado taarifa watazipeleka kwa kampuni ya Facebook inayohusika kuziuza hizo taarifa kwa makampuni mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…