Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
WhatsApp imeanza kuongeza udhibiti mpya wa wazazi kwa akaunti za vijana (teens). Kipengele hiki kinahusu kuwapa wazazi uwezo wa kuweka mipaka fulani bila kuwapa uwezo wa kusoma ujumbe binafsi wa mtoto.
๐ Wazazi wataweza kudhibiti nini?
๐ค Picha ya profile: mzazi anaweza kuweka nani anayeruhusiwa kuiona.
๐ฅ Kuongezwa kwenye Groups: mzazi anaweza kuweka mipaka kuhusu nani anaweza kumuongeza kijana kwenye group.
๐ข Channels: matumizi ya Channels yanaweza kudhibitiwa.
๐ข Status: mzazi anaweza kudhibiti nani kijana anaweza kuona Status za wengine na nani anaweza kuona Status yake.
๐ค Meta AI: mzazi anaweza kuchagua kiwango cha maudhui kinacho ruhusiwa kwenye Meta AI, ikiwemo chaguo kali zaidi la โLimited Content.โ
๐ Taarifa za Groups: mzazi anaweza kupata notification kijana akijiunga au kuondoka kwenye group, au group inapoongezeka kufikia ukubwa fulani.
Setting hiyo inalindwa na PIN ya mzazi. Hivyo, kijana akitaka kubadilisha baadhi ya vikwazo vilivyowekwa, atahitaji idhini ya mzazi kupitia PIN hiyo.
๐ Je, mzazi ataweza kusoma chats?
Hapana. WhatsApp inasema ujumbe na simu bado zinalindwa na end-to-end encryption. Kwa hiyo parental controls hizi hazimaanishi mzazi anapata uwezo wa kusoma mazungumzo binafsi ya kijana.