Whatsssssss!!!!!!!!!????

ofa hadi kanisani, jamaa kamzimia mrembo kanisani mara ikafika saa ya kutoa sadaka eti akamwambia " dont worry i"will pay for you"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uhali gani mteja wangu?
Leo tunapeana discount kwa wanunuzi wote wa kuku. Tuna kila aina za KUKU kama vile:_
1. KUKUwaza
2. KUKUpenda
3. KUKUmiss
4. KUKUona
5. KUKUalika
6. KUKUbeep
7. KUKUsuta
8. KUKUtia
9. KUKUpigia
10. KUKUjali
11. KUKUlamba
12. KUKUngoja
13. KUKUtukana
14. KUKUsifu
15. KUKUsalimu
16. KUKUoa
17. KUKUtumia Sms
18. KUKUtamani
19. KUKUfuata

Niambie unahitaji kuku gani mteja wangu?[emoji12][emoji13]
 
Najua vitu vitano (5) kuhusu wewe!!
1. Unasoma hii msg
2. Wewe ni mtu
3. Huwezi kutamka neno "P" bila kufumbua mdomo
4. Umejaribu kuona kama utaweza
6. Unacheka[emoji16]
7. Uso wako unafuraha, na umeiruka No. 5
8. Umeangalia kama kuna No.5 kweli umeiruka
9. Unaendelea kutabasamu kwasababu nakupatia
10. Umeipenda hii msg[emoji23][emoji23][emoji23], Utaiiba[emoji12]
 
DOGO ASIYEPENDA SHULE ALISHUHUDIA MWIZI AKIIBA KWAO USIKU WAKATI MWIZI ANAONDOKA DOGO AKAMDAKA MGUU AKAMWAMBIA KAMA HUCHUKUI NA BEGI LANGU LA SHULE NAPIGA KELELE[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtoto Ziro aligoma kwenda shule, Alipoulizwa kwanini huendi shule?
Akajibu, huko shule Walimu hawana uhakika na wanachokisema,
Maana juzi walisema 5+2=7,
Jana 4+3=7,
Leo 6+1=7,
Kesho huenda watasema 7+0=7,
Sasa huo sio ubabaishaji wa akili?[emoji12]
 
Kipofu kampiga mtu mpaka kamuua, akafikishwa mahakamani;
HAKIMU: Kwanini umefanya ukatili namna hii
KIPOFU: Mheshimiwa marehemu alisema mwenyewe,'Ukinipiga utaona', kwa vile nilikuwa na hamu kubwa ya kuweza kuona, nikajitahidi kumpiga sana ILI nipone, bahati mbaya kafariki[emoji13][emoji13][emoji13]
 
Mke: Hivi mume wangu nikifa utaowa tena?
Mume: Ndio ntaoa
Mke: Ukioa huyo mwanamke ataishi humu?
Mume: Ndio ndani
Mke: Huyo mwanamke atalala kwenye kitanda hiki?
Mume: Ndiyo kitanda kitadumu sana hiki,
Mke: Vipi atavaa hadi nguo zangu?
Mme: Hilo sina uhakika kwani yeye ni mnene kidogo[emoji12]
 
Mume alichelewa kurudi nyumbani kwake kama kawaida yake, alipofika akapitiliza mpaka chumbani alipofika akagusa kitandani kwenye shuka ndipo alipogusa miguu minne badala ya miwili aliyozoea siku zote, akatoka taratibu aliporudi alirudi na rungu akawatandika miguuni kwa hasira akatoka mpaka sebuleni kutuliza hasira..
Hapo ndipo alipomkuta mkewe kalala...!!
Mke akamwambia: Mume wangu chumbani nimepisha wazazi wako walale wamekuja leo kutusalimia[emoji15]
 
Amakweli Uvivu kipaji hebu wasikie hawa.....
MTOTO: Baba naomba hiyo glass.
BABA: Njoo uchukue mwenyewe.
MTOTO: Baba bwana naomba.
BABA: Halafu we mtoto ntakuja kukupiga.
MTOTO: Basi ukija kunipiga njoo na hiyo glass.![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Babu Mmoja alikuwa anakunywa Uji Mgahawani, Mara akaingia Mzungu na Kuagiza Soda aina ya FANTA, Yule Mzungu Alipomaliza Kunywa alisikika akisema;
"THIS FANTA IS VERY FANTASTIC."
Yule Mzee nae Kuonyesha Nayeye anajua Kizungu, alipomaliza Uji wake tu akasema;
"THIS UJI IS VERY UJISTIC"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Jamaa wa3 walikodisha hoteli ya ghorofa 60, wao wakapata ghorofa ya mwisho kabisa, wakapanda kwa lift na asubuhi wakashuka kwa lift, jioni walivyorudi wakakuta umeme umekatika wakakubaliana wapande ngazi kwa stori,
wa1 apige za kutisha kuanzia ghorofa 1-20,
wa2 kuchekesha kuanzia 21-40,
wa3 kuhuzunisha kuanzia 41-60,
wakapanda walivyofika ya 59 yule wa3 akasema hii ndo ya kuhuzunisha zaidi, TUMESAHAU KUCHUKUA FUNGUO PALE RECEIPTION!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DIRECT TRANSLATION FROM SWAHILI TO ENGLISH..
1)Wacha mchezo - leave sport
2) wewe ni kiboko yao - you are their hippopotamus
3)nasikia kizunguzungu - am hearing english english
4)mahindi yameota - maize are dreaming...
5)usinivute - don't smoke me
6)acha kulia lia wewe - stop to right right you
7)maisha ni rahis sana - life is very president
8) Amezimia - he has jobnhundreded
9)Amejikakamua - he has brother sugarcaned himself
10) ana kimbelembele sana - he has a lot of front front
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
JANA HAPA HOME
JENERETA LILIWASHWA...!!!
ACHA TUHANGAIKE KULIKUNA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna jamaa hapa ananiuliza kwanini stand haikufungwa na Yanga nimemjibu
Stand ifungwe halafu mabasi yapark wapi[emoji16][emoji12]
 
Teacher: Nitajie biashara iliyo fell kwasababu ya uzembe
Mwanafunzi: Changudoa akipata mimba
Teacher: Toka nje upesiiiiiii
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna siku nilikuwa kwenye Dar Express naenda Moshi, pembeni yangu alikaa mzee mmoja, tulipofika kibaha nikanunua chokleti mbili nikaanza kula, yule Mzee akawa ananiangalia sana akaniuliza "kijana unajua kula chokleti sana meno yataoza?"
Nikafikiria nimjibu nini nikakosa, basi nikaamua kumwambia " *unajua babu yangu aliishi miaka 140?*" akaniuliza "babu yako alikuwa anakulaga chokleti?" nikamjibu kwa kifupi ALIKUWA HAFUATILIAGI MAISHA YA WATU akaamua kuahama siti akaenda kukaa mbele na dereva[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni heri ukae bar ukiwa unawaza kanisani kuliko kukaa kanisani ukiwa unawaza bar[emoji13]
 
Rais wa Marekani Baraka Obama ni MWEUSI
Mcheza tenesi number moja wakike duniani Serena Wiliam ni MWEUSI
Bondia ghali zaidi Duniania Floyd Mywether ni MWEUSI
Gwiji mkuu wa Soka Duniani Pele ni MWEUSI
Kiffi Anan ni MWEUSI
Mwanamziki tajiri zaidi duniani Dk. Dree ni MWEUSI
sasa wewe mwanamke unaejichubua unataka nini?[emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…