Whatsssssss!!!!!!!!!????

Whatsssssss!!!!!!!!!????

Mchungaji kamfuata pedeshee mmoja maarufu kwa kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu, huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia kwa kujenga eneo la choo!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kuna watu wawili walienda railway station wakakuta train ndio inaondoka wakaanza kuikimbiza mmoja akafankiwa kuipata "alieachwa akawa anacheka", watu wakamuliza unacheka nini wakati umeachwa? akasema yule aliepanda alikuwa ananisindikiza mimi"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
*_" Hakuna jambo baya kama kwenda kwenye harusi ukakuta shati lako ndo uniform ya wahudumu, unasimamishwa na mwenyekiti wa kamati na anakufokea kabisa kwanini huhudumii watu? watu wakiishiwa vinywaji halafu wewe umekaa wanakutazama kwa hasira._* [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndani ya daladala,
DEMU: samahani kaka naomba unipakate,
JAMAA: usijali njoo tu,
DEMU: haya,
JAMAA: inaonekana ww ni sekretari..?,
DEMU: ndio kwa nn,
JAMAA: vidole vyako laini kweli,
DEMU: na ww ni fundi magari?
JAMAA: ndio, kwa nini?
DEMU: hapa nilipokaa naona nainuliwa na kitu kama jeki!! [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahaaaaa..!!
Jamaa ww balaa,
Fundi ananyanyua tairi kwa jeki.
Nimecheka sana.
 
Jamaa mmoja wakati amemsimamisha dada mmoja na wakati akimtongoza bahati mbaya/nzuri naniliu yeke ndani ya zipu si ikasimama.
Jamaa alichoamua baada ya

hapo ni kuitoa nje na kuiambia "haya tongoza wewe mwenyewe na haraka zako" [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yalaaaaahh .
Daaah..!!!
Ngoja hii thridi niipe jina la JPM lager.
Hatari sana hii.
 
Mbongo kaenda hospitali kumuona daktari

Mhudumu: babu kumuona dakari ni 20000 unalipia hapa.

Babu: sina

Mhudumu: lazima ulipie

Babu : usijari ntaziba macho .
 
Jamaa alikua anaumwa jino mkewe akamuelekeza aende kung'oa hospitali ya bei nafuu jino moja wanang'oa kwa shilingi moja.

Jamaa kafika hosptiali wakamng'oa jino ila wakamchaji shilingi 32 kwa kung'oa jino moja.
Karudi nyumbani kwa huzuni kamwambia mkewe kua bei imepanda, mkewe kamwambia umeibiwa Mme wang , jamaa karudi hosptali kwa jazba wakagoma kumrudishia chenji ya shilingi 31
Kuona hivyo akaamua wamng'oe meno mengine 31 kufidia ela yake isiende bure.
Kurudi nyumbani anamwambia mkewe, wale jamaa wapumbavu sana waligoma kunipa ela yangu ikabidi ning'oe meno yote ili pesa yangu isiende bure

Wanaume hatupendagi ujinga[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom