Whatsssssss!!!!!!!!!????

WIVU MBAYA NA NI NOMA!
Mwanamke mmoja alikuwa akimhisi mume wake anatembea na houseGirl, siku moja usiku akamhamisha chumba houseGirl kwa
siri bila mumewe kujua ili amtege!
AkaJichomeka chumbani kwa yule dada akazima taa na kujifanya amelala, mara akasikia mtu anaingia chumban na kumparamia! mapenz moto moto yakaanza
Jamaa kapiga goli la kwanza la pili. Yule mama akasema kumbe kwa housegirl unafanya vizuri hivi akaruka ili awashe taa, enheeeh! leo nimekukamata, ile kuwasha taa ili amuumbue akakuta ni mwanae[emoji86][emoji87][emoji125][emoji125][emoji125]
 
SHERIA 13 ZA MPIRA WA MIGUU WAKATI
TUKIWA WATOTO.
1. Dogo mnene lazima awe Golikipa.
2. Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze.
3. Penati itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.
4. Mechi itaisha kama kila mchezaji atakua amechoka.
5. Hakuna free kick, kitu kama icho hakipo kwenye mechi zetu.
6. Hakuna Refa, mchezaji anaweza kuzunguka na mpira ata nyuma ya goli.
7. Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako ni mdogo kuliko watu wote uwanjani.
8. Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka, au kutungua mpira endapo utanasa kwenye mti uku wakisubiria mchezaji aitwe kwao na wao wapate nafasi.
9. Mwenye mpira akikasirika, mechi ndo
itakua imefika mwisho.
10. Inaruhusiwa kubadili golikipa kama penati ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea yule wa mwanzo.
11. Yule mtaalam wa soka huwa hakosi namba ata siku moja.
12. Mwenye mpira huwa hatolewi ata akicheza vibaya.[emoji460][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Mume akamwambia mke wake,"Fumba macho
yako tufanye maombi" akaanza kwa Kimombo,
"... Lord I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray 4 Joy, I pray 4 Love, I pray 4 Hope, I pray 4 GLORY, I pray 4 Faith,I pray 4...."
Mke akadakia, "Unadhani mimi sina ee" akaanza
I pray 4 Geofrey,I pray 4 Temu,I pray 4 Rweyemamu, I pray 4 Masawe,I pray 4 Benson,I pray 4 Edwin, I pray 4 Swai,I pray kwa wote niliowasahau!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
MUME:::Hello My Wife?
MKE:::Hello My Husband!
MUME:::How are you?
MKE:::Fine,
MUME:::Baby Leo nitachelewa kurudi nyumbani,
MKE:::Nishajua uko kwa malaya zako,Wewe ni mzinzi sana sijui ilikuaje ukanioa nakuchukia sana,Kwanza sikupendi nakuchukia Sura yenyewe kama Zombi,
MUME:::Nipo Benki hapa Wife kuna foleni kidogo,
MKE:::Haaa!!! Ulijiaje kama sina pesa mume
wangu, njoo na laki 2 mume wangu nadaiwa na Mama Juma hela ya Madera na Vitenge niliyokopa wiki iliyopita nakupenda sana My
Husband kuliko hata roho yangu,Wewe ndiyo
Handsome wangu kuliko yoyote duniani na
Pia nakutengea maji ya moto iliuje kuoga
na hii baridi My sweet, Alafu pitia kwa John Unichukulie Chips, Mayai, Kuku wa Kuchoma nakupenda sana My husband wangu,
MUME:::Ni Benki ya Kuchangia Damu,
MKE:::Nyooo!!! Na tena wambie wakutoe yote ninavyokuchukia yaani Sikupendi basi tu.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
USWAZI noma!!
Mama KIDAWA Ni Mjamzito, Hawezi Kumpa Mumewe Penzi. Akamwonea Huruma Kwa KIU Aliyo Nayo.
Akampa elfu 5 Akamwambia Akatulize Kiu
Kwa ASHURA. Jamaa Kufika ASHURA Akamtolea Nje, eti hela ndogo.
Mama KIDAWA Akaja Juu Akamwambia Mumewe,
"Usikonde! Nenda Kwa MAGE, ni mtu Wangu
Ila Huyu ASHURA Atanikoma, Yeye Akiwa Na MIMBA Mumewe nampaga
Bure, Leo Hii Anajifanya Mjanja[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa: Hello mrembo, samahani, una mpenzi?
Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye."
Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8
"Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa
maana Mungu ni upendo."
Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na wewe
unamaanisha hayo maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana,
kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake."
Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba we ni mkweli na mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe."
Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu?
Wasichana mbona wako wengi tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote."
Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi kwangu umependa kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila."
Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata sio
mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
Binti: Nikisema nimekukubalia itakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua maandiko kiasi hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapo ifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."
Binti: Wowwww! Naona unampenda sana Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini."
Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza,
yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo."
Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali. Mpaka hapo nakupenda tayari!!
Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"[emoji120]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bado unasema Kiswahili ni lugha nyepesi eti
kwa kuwa tunaelewana tu!!!?Tazama.......
KIINGEREZA--------------KISWAHILI
Device--------------------Kitumi
Photocopier-------------Kinukuzi...
Duplicating Machine --Kirudufu
Resistor------------------kikinzani
Power Saw---------------Msumeno oto
Sensor--------------------Kisimbuzi
Lap Top------------------Kipakatalishi
ICU------------------------Kisadaruki
Microwave---------------Tanuri ya miyale
Memory Card-----------Kadi sakima
SIM card-----------------Kadiwia/mkamimo
Scratch card------------Kadi hela
Business card----------Kadikazi
Identity card---- --------Kitambulisho
ATM---------- ------------Kiotomotela
Nutrients ----- ----------Virutubisho
Starch---------- ---------Nisha
Stigma--------- ----------Ntwe
Nectar--------------------Mbochi
Humus--------------------Mboji
Germ cell----------------Celizazi
Femur--------------------Fupaja
Green house------------Kivungulio
Esophagus--------------Umio
Sunflower---------------Alizeti
Weevil-------------------Fukusi/dumuzi
Distillation---------------Ukenekaji
Evaporation------------Mvukizo
Dissolve ----------------Uyeyushaji
Stagnant----------------Tuame
Synthesis---------------Uoanishaji
Monitor-----------Muwazi
Processor---------------Kichakato
Computer Virus--------Mtaliga
Floppy Disk-------------Diski tepetevu
Mouse-------------------Kipanya/kisakura
Slot-----------------------Upenyu
Flash Disk--------------Diski mweko
Scanner-----------------Mdaki
Keyboard---------------Kicharazio
Force of Gravity-------Kani ya mvutano
Certificate--------------Astashahada
Diploma----------------Stashahada
Degree-----------------Shahada
Masters----------------Uzamili
Phd---------------------Uzamivu
Sausage---------------Soseji
Kebab------------------Mshakiki
Crisps------------------Kaukau
Chips-------------------Vibanzi
Juice--------------------Sharubati
Password--------------Nywila
Zebra Crossing-------Kivuko milia
[emoji117]sijaambulia hata moja[emoji23][emoji23]
 
Jamaa alianza kujisifu sana
kazini kwake;
Jemsi: Wiki ijayo nafanya mtihani, ni miezi sita sasa nafanya masomo ya jioni, nimejua mengi sana, we unamjua David Livingstone?
Devi: Hapana simjui
Jemsi: Huyo ndie mzungu wa kwanza kuliona Ziwa Victoria, ungekuwa unasoma masomo ya
jioni ungemjua huyu.
Jemsi akawa kero kazini kwa maswali yake.
Jemsi: We unamjua Graham Bell?
Devi: Hapana simjui
Jemsi: Huyo ndie alikuwa mtu wa kwanza kutengeneza simu, ungekuwa unaenda
kuchukua masomo ya jioni ungemjua.
Siku moja Devi akamwita Jemsi;
Devi: Jemsi unamjua Hasani Makolokocho?
Jemsi: Hapana
Devi: Huyo ndie mchepuko wa mkeo kwa miezi
sita sasa, ungekuwa huendi kuchukua masomo ya jioni ungemjua[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkaanga chipsi alikuwa anakaanga chips, akapasua yai la kwanza halikuwa na kitu, yai la pili halikuwa na kitu pia, yai la tatu hivo hivo, jamaa akasema "shenzi! ina maana na kuku hawa leo wametumia Kondom?![emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi
akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.
MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23]
Mume: utanitambua leo kumbe kuna watu wananiibia!!
 
Binti: Hallo mpenzi, mambo!
Jamaa: Poa baby!
Binti: Uko wapi?
Jamaa: Mimi niko town napata lunch.
Binti: Wow! Unarudi saa ngapi? Nina njaa dear, nataka uniletee msosi.
Jamaa: Narudi baada ya nusu saa, Nikuletee nini?
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne yakaangwe pembeni, baga, piza ya samaki waweke mayonaize, coka take away ya baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa chupa kubwa ya Kilimanjaro.
Jamaa: Umesahau viti, meza, leseni, masufuria, sahani na vijiko.
Binti: Kwa nini dear?
Jamaa: Naona hutaki kula, unataka kufungua hoteli??[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Demu mkaliiii alikaa na mzee kwenye daladala siti ya nyuma, mzee kavaa viatu vinatema kishenzi demu kashindwa kuvumilia na kuropoka, "wee mzee ni VIATU vyako vinanuka au?" Mzee akamjibu kwa upole, "Hapana hebu angalia PICHU yako labda iko upande mjukuu wangu!"
Yule demu kimyaaaa![emoji12][emoji13]
 
Mume anamuuliza mkewe: wewe kutwa nzima unacheki kipindi cha mapishi kwa Tv lakini kupika kwenyewe hujui..
Mke akamjibu: wewe mbona usiku kucha unaangalia movie za ngono lakini huwezi duuuuh!, nilishawahi kukuulizaa??? Zaidi ya mimi kutoka nje kwenda ku du na wenzako tuheshimiane bwana!. jamaa akafa hapohapo.!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wiki iliyopita Ray alienda kwa daktari wa saikolojia ya mahusiano kumuona daktari katika harakati za kutaka kuimarisha ndoa yake. Ray akaanza kuuliza cha kufanya
Ray: Dokta, nataka nimshike mke wangu sehemu ambayo itamfanya achanganyikiwe
Daktari: Ni rahisi sana, njoo na mkeo, tutamfanyia upasuaji wa kichwa, tutafunua kichwa chake kisha utagusa ubongo wake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii imetokea huko ujerumani ambapo daktari mmoja wa vichaa mwenye hospitali yake binafsi alikuwa anasafiri na vichaa wake watatu wenye nafuu katika ndege ndogo toka mji mmoja kwenda mji mwingine.
Wakiwa hewani wagonjwa wawili walikuwa wanacheza cheza na kupiga kelele ndani ya ndege kwa nyuma wakati mmoja ametulia kimya akiwa ameshika gazeti. Kelele zilikuwa
zinasumbua kiasi fulandi ndipo Yule mgonjwa
aliyekuwa kimya akaenda kwa daktari mbele katika chumba cha kuongozea ndege na kuzungumza na daktari wao
Mgonjwa: Samahani dokta, nilikuwa nafikiri kama tungewapa mipira wachezee ili wapunguze kelele
Daktari: Ni sawa haina tatizo, wazo zuri sana
Yule mgonjwa akarudi nyuma kwa wenzie
kisha baada ya kama dakika kumi hivi kule nyuma kulikuwa kimya kabisa. Daktari akafurahishwa mno na ubunifu wa yule mgonjwa mmoja na kuona kuwa maendeleo yake ni mazuri.
Daktari akataka kuwapa pongezi kwa kukaa kimya, akamuita yule mgonjwa aliyetoa wazo na kumuuliza
Daktari: aisee! Wazo lako ni zuri sana, waambie wenzio kuwa tukifika nitawapa zawadi kwa utulivu wa leo
Mgonjwa: nilipata wazo zuri zaidi ya lile, nilipowapa mpira nikawafungulia mlango wakachezee barazani.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkewe Ray alikamatwa katika supamaketi moja Mlimani siti akiiba matunda.Kisha akapelekwa mahakama ya kisutu na
mahojiano yake na hakimu yalikuwa hivi:
Hakimu: Umeiba nini?
Mke wa Ray: Nimeiba mfuko wa machungwa
Hakimu: Ulikuwa na machungwa mangapi?
Mke wa Ray: ulikuwa na machungwa manne
Hakimu: Basi nakuhukumu ufungwe jela kwa muda wa siku nne.
Kabla Yule hakimu hajagonga nyundo yake kumaliza kesi Ray (mumewe) akasimama na kumuomba hakimu kama anaweza kupewa ruhusa ya kuzungumza. Hakimu akamruhusu kisha Ray akasema “Pia aliiba na mfuko wa mchele”
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…