Whatsssssss!!!!!!!!!????

Mume Alipomuoa Mke Wake Kwenye Simu Akamsave "Honey My Life."
Baada Ya Mwaka 1 Akabadilisha Akaandika "My Wife."
Baada Ya Miaka 2 Akaandika "Home."
Baada Ya Miaka 5 Akaandika "Wrong Number."
Baada Ya Miaka 10 Akaandika "Hitler."
Baada Ya Miaka 15 Akaandika "Taliban."
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
HEKAYA ZA ABUNUASI[emoji23][emoji23]
Abunuasi Alinunua Punda Ila Hakuwa Na Sufuria Kubwa La Kumnyweshea Maji Ikabidi Aende Kuazima Kwa Jirani Na Akapewa Baada Ya Siku 3 Akalirudisha Kwa Mwenyewe Huku Akiwa Ameweka Sufuria Nyingine Ndogo Ndani Yake,
Abunuasi Akamwambia Yule Jirani Wakati Anaichukua Ile Sufuria Ilikuwa Na Mimba Kwahiyo Imezaa Yule Jirani Akashangaa Na Kufurahi Kusikia Sufuria Imezaa,
Siku Nyingine Abunuasi Akaenda Kuazima Yule Jirani Akampa Akijua Itarudi Imezaa Lakini Siku Nyingi Zikapita Bila Sufuria Kurudishwa Ndipo Alipoamua Kumfata Abunuasi Akamwambia "Samahani Jirani Ile Sufuria Imefariki Wakati Inajifungua."
Jirani "Haiwezekani Sufuria Haiwezi Kufa."
Abunuasi "Kila Kinachozaa Pia Hufa."
Yule Jirani Alirudi Kwake Bila Sufuria.
 
Kuna Wanafunzi Flani Walikuwa Na Mitihani Jumatatu Asubuhi Ila Jana Yake Jumapili Walikesha Club Walikunywa Pombe Balaa Mpaka Jumatatu Wakachelewa Kwenye Mtihani Wakaamua Kumfata Mwalimu Na Kumwambia Walikuwa Kwenye Harusi Ivyo Wabadilishiwe Siku Ya Kufanya Mtihani Mwalimu Akakubali Na Akawaambia Mtihani Ni Kesho Yake,
Ilipofika Kesho Kila Mtu Akawekwa Kwenye Chumba Cha Peke Yake Halafu Maswali Yaliuliza Hivi:-
1.Bwana Harusi Anaitwa Nani?
2.Bibi Harusi Ni Mrefu Au Mfupi?
3.Bwana Harusi Ni Mweupe Au Mweusi?
4.Ukumbi Unaitwaje?
5.Ukumbini Mlitoka Saa Ngapi?
[emoji12][emoji13][emoji13][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwalimu Aliingia Darasani Akasema Anaejijua Mjinga Asimame
Zuzu Akasimama, Mwalimu Akamuuliza "Kwahiyo Wewe Ndo Mjinga?"
Zuzu"Nimeona Nikusaidie Maana Ulikuwa Peke Yako."
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Baba Alikuwa Anakula Na Mwanae,
Mtoto: Baba Hivi Mende Wanaliwa?
Baba: We Ndo Maswali Gani Hayo Wakati Wa Kula Ebu Nyamaza.
(baada Ya Kula)
Baba: Eeeh Ulikuwa Unauliza Nini?
Mtoto: Nilimwona Mende Kwenye Mchuzi Wako Basi Ushamaliza Kula[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa Alienda Kwa Dokta:-
Dokta: Una Tatizo Gani Mgonjwa?
Jamaa: La Macho.
Dokta: Vipi Huoni?
Jamaa: Naona Vitu Vyote Kasoro Kimoja Tu.
Dokta: Kitu Gani Icho?
Jamaa: WIVU..Yaani Sionagi Wivu Kabisa.[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzazi Alimpeleka Mwanae Kumuandikisha Na Chuo,
Akakutana Na Mlinzi Ikawa Hivi:-
MZAZI: Hiki Chuo Kinafundisha Eeeeh?
MLINZI: Eeeh Ni Kizuri Kwasababu Mimi Nimemaliza Hapa Na Kupata Kazi Hapa Hapa.[emoji23][emoji23]
 
Majambazi Flani Walikamata Gari Wakaanza Kusachi Watu Wakakuta Hawana Hela,
Wakasema Kila Mtu Ataadhibiwa Kutokana Na Shati Au Tshirt Aliyovaa,
Kuna Mmoja Alivaa Jezi Ya Rooney Akapigwa Fimbo 10 Kwakua Jezi Ilikuwa Imeandikwa Namba 10 Mgongoni,
Mwingine Akala 50 Kwasababu Alivaa Shati Imeandikwa 50 Cent Sasa Kwa Pembeni Kulikuwa Na Jamaa Analia Balaaaa Kumuangalia Vizuri Kumbe Amevaa Tshirt Ya Uchaguzi Imeandikwa "LOWASSA 2015" [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Traffic Flani Mlevi Aliona Gari Linakuja Kwa Kasi Akalisimamisha,
Alikuwa Mwanamke Anaendesha,
Yule Mwanamke Akapaki Pembeni Akaona Kupitia Side Mirror Traffic Anakuja Huku Akiyumbayumba Akajua Yuko Chakari,
Traffic Akafika Akamwambia " Mama Lete Leseni Yako"
Yule Mama Akajisachi Kwenye Pochi Akatoa Kioo Kidogo Cha Kujitazamia Kisha Akampa Yule Traffic Akakichukua Akakiangalia Kiasi Kisha Akamwambia " Si Ungesema Tu Kama Ni Traffic Mwenzangu Haya Nenda." [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa Flani Aliingia Kwa Kinyozi Na Mtoto,
Akasema Anyolewe Nywele Na Ndevu Alipomaliza Akasema Na Mtoto Naye Anyolewe,
Wakati Mtoto Ananyolewa Yeye Akaaga Anaenda Kumnunulia Mtoto Juisi,
Masaa 3 Yakapita Bila Jamaa Kutokea Kinyozi Akamwambia Dogo "Vipi Baba Ako Amekusahau?"
Mtoto"Yule Sio Baba Angu Alinikuta Njiani Akaniambia Tuingie Hapa Tunyolewe Bure." [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa:Baby Nataka Nikununulie Zawadi Nzuri Sana Unaona Lile Vogue Pale?
Demu🙁kwa Kudakia)
Heeee Baby Kweeli Unataka Kuninulia Gari Zuri Vileee?
Asante Sana.
Jamaa:Hamna, Kuna Rangi Ya Kucha Inafanana Rangi Na Lile Gari Ndo Nataka Nikununulie. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwalimu Alikuwa Anawauliza Wanafunzi Kazi Za Baba Zao Ndipo Akafika Kwa Jose
MWALIMU: Eeeh Jose Tuambie Baba Yako Anafanya Kazi Gani?
JOSE: Mimi Baba Yangu Ni Mtu Mkubwa Na Anaheshimika Katika Nchi.
MWALIMU: Inaonekana Baba Yako Ana Cheo Kikubwa?
JOSE: Hata Raisi Anainamisha Kichwa Akiwa Naye.
MWALIMU: Sasa Anafanya Kazi Gani?
JOSE: KINYOZI.[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa Flani Alikuwa Amechoka Kufanya Kazi Akaamua Afanye Kituko Ili Aambiwe Akapumzike Nyumbani,
Jamaa Akapanda Juu Ya Dari Akajining'iniza Kama Taa
Bosi Alipomuona Akashangaa Na Kumuuliza "Unafanya Nini Uko Juu?"
Jamaa"Mimi Ni Taa Namulika Ofisi."
Bosi"Haha Inaonekana Kazi Inakupa Stress Nenda Nyumbani Ukapumzike"
Jamaa Akashuka Na Kuanza Kuondoka Rafiki Yake Pale Ofisini Naye Akainuka Na Akamfuata Nyuma
Bosi Akashangaa Na Kumuuliza Rafiki Yake "Na Wewe Unaenda Wapi?"
Rafiki"Sasa Nitafanyaje Kazi Kwenye Giza Bosi"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Demu Flani Alipigiwa Simu Na Namba Ngeni
Namba Ngeni: Halooo Mrembo
Vipi Una Boi Friend?
Mrembo: Ndio Ninae Kwani We Nani?
Namba Ngeni: Ni Mimi Baba Yako Kumbe Una Boi Friend Eeeeeeh Nikirudi Utakoma...
*Baada Ya Dakika Tano Namba Ngeni Ikampigia
Namba Ngeni: Haloo Mrembo Una Boi Friend?
Mrembo: Hapana Sina Kwani We Nani?
Namba Ngeni: Ni Mimi Boi Friend Wako Kumbe Umenisaliti?
Mrembo:Hapana Nilijua Ni Baba Yangu.
Namba Ngeni: Ni Mimi Baba Yako Kumbe Ni Kweli Subiri Nirudi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa Kaweka Sahani Yake Ya Chakula Mezani Ile Anataka Kula Tu Anasikia Mlango Unagongwa Akaficha Chakula Chini Ya Meza Akaenda Kufungua Mlango,
Mgeni: Vipi Mbona Pale Kwenye Meza Panatoka Moshi?
Jamaa: Ahaaaa Mipanya Ya Humu Ndani Inakera Sana Yenyewe Kila Saa Inavuta Bangi Tu. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwalimu: Mwaka 1961 Ni Tukio Gani Lilitokea Tanzania?
Mwanafunzi: Tanzania Ilipata Uhuru Wake.
Mwalimu: Na 1964
Mwanafunzi: Tanzania Ilitimiza Miaka 3 Baada Ya Kupata Uhuru.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Zuzu Alienda Kuposa,
Akaambiwa Mahari Ni Milioni 2 Akashtuka Kwa Mshangao Na Kusema " Yani Mahari Ni Milioni 2 Wakati Pale Jirani Nimeambiwa Ni Laki 2 Na Binti Ana Mimba Kabisa."
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siku Moja Watoa Damu Salama Walienda Kutoa Damu Shule Moja. Baada Ya Maelekezo Muhimu Na Kabla Ya Zoezi La Utoaji Damu Madaktari Wakatoa Nafasi Ya Maswali Na Majibu.
Mazungumzo Yalikuwa Kama Ifuatavyo:
Mwanafunzi: Nyie Wanasayansi Mnasema Binadamu Ametokana Na Nyani?
Daktari: Ndio
Mwanafunzi: Kwanini Msiende Kutoa Damu Kwa Nyani Wapatikanao Mbuga Ya Serengeti, Mikumi, Katavi N.K.
Daktari Akakosa Jibu.
Wanafunzi Wakashangilia Huku Madaktari Wakirudi Bila Damu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
JAMAA: Baby Let Me Be The First Kukuwish..HAPPY BIRTHDAY.
DEMU: Thank You Baby Same To U. [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…