Whatsssssss!!!!!!!!!????

Kuna Ajali Ilitokea Gari Lilitumbukia Mtoni,
Kila Mtu Akawa Anafanya Jitihada Za Kuogelea Na Kutoka,
Zuzu Akafanikiwa Kutoka Mle Mtoni Na Kufika Nchi Kavu Mara Ghafla Akajitupa Tena Watu Wakamuuliza " Mbona Unarudi Tena Kwenye Maji?"
Zuzu: Naenda Kumtafuta Konda Hajanirudishia Chenchi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mama Mmoja Alikuwa Na Mwanae Akachukua Taxi Waende Sehemu Flani Wakati Wapo Njiani Wakawaona Wadada Wanajiuza, Dogo Akamuuliza Mama Yake
DOGO: Eti Mama Hawa Wanafanya Nini Hapa?
MAMA: Wanawangoja Waume Zao Waje Kuwachukua.
(Mara Dereva Taxi Akaingilia)
DEREVA: Si Umwambie Ukweli Tu Kwamba Hao Wanajiuza.
DOGO: Kwani Mama Hao Wakizaa Watoto Wao Wanakuwaje?
MAMA: Wanakuwa Madereva Taxi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbongo Flani Alienda Ulaya Akaingia Hotelini,
Akaagizia Chipsi Na Kuku Na Kwakua Kuku Wa Huko Walikuwa Laini Akawa Anatafuna Mpaka Mifupa,
Na Pembeni Yake Alikuwa Amekaa Mzungu Alikuwa Anakula Wali Na Samaki Na Alikuwa Akimshangaa Sana Na Mara Akamwambia
MZUNGU: Kama Unaweza Kula Hadi Mifupa Sasa Mbwa Wenu Mnawalisha Nini Afrika??
Mbongo Akajibu Kwa Dharau,
MBONGO: Weell, We Give Them A Plateful Of Rice And Fish. [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtoto Flani Tangu Azaliwe Alikuwa Hawezi Kuongea,
Siku Moja Akaita Bibi Kesho Yake Bibi Akafa,
Siku Iliyofata Akaita Babu
Kesho Yake Babu Akafa
Nyumba Nzima Ikajaa Hofu Nani Anafuata
Mara Akaita Baba,
Baba Akawa Na Huzuni Akaenda Kazini Akawaaga Wenzake Aliporudi Nyumbani Akaambiwa Housi Boi Kafa[emoji13][emoji13][emoji13]
 
Baba Mmoja Bahili Sana Alirudi Nyumbani Akaanza Kuwapiga Bakora Watoto Wake,
Watoto: Baba Mbona Unatuchapa Tumefanyaje?
Baba: Nyie Mna Matumizi Mabovu Sana Haiwezekani Mko Watatu Halafu Mnafungulia Feni Namba 4
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwanafunzi Flani Aliingia Na Chabo Kwenye Mtihani
Bahati Mbaya Msimamizi Akamkata Nayo,
Msimamizi: Hiki Nini?
Mwanafunzi: Hata Aliyetengeneza Computer Alijua Hard Disk Uwa Inajaa Akatengeneza External[emoji15].
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Baunsa Flani Mwenye Mizaha Aliingia Bar Akamkuta Jamaa Ameshika Tama Huku Akiwa Amemimina Bia Kwenye Glasi Akachukua Glasi Akainywa Bia Yote
Jamaa AkasemaπŸ˜€aaah Sijui Nina Mkosi Gani?.
Baunsa:Nilikuwa Nakutania Tu Kaka Nitakununulia Nyingine.
Jamaa:Hapana Leo Asubui Nimeenda Kazini Bosi Akanifukuza Kazi Nikatoka Nje Nikakuta Gari Langu Limeibiwa Nikarudi Nyumbani Nikakuta Mke Wangu Ameondoka Ndo Nikaja Hapa Nimenunua Bia Nikaweka Sumu Halafu Umekuja Kunipokonya Kwa Ubabe.[emoji12][emoji13][emoji13]
 
MKE: Mume Wangu Mbona Ulisema Ukiingia Mwaka Mpya Utaacha Kunywa Pombe Na Utakuwa Mtu Mpya?
MUME: Ni Kweeli Lakini Sio Kama Sijabadilika Lakini Tatizo Na Huyu Mtu Mpya Anapenda Pombe [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna Mmachinga Alikuwa Anafanya Biashara Ya Kofia Siku Moja Wakati Anarudi Alipita Karibu Na Pori Na Kwakua Alikua Amechoka Sana Akaamua Apumzike Chini Ya Mti Mkubwa Wa Kivuli Na Huku Akiwa Ameweka Kiroba Cha Kofia Pembeni Na Mara Akapitiwa Na Usingizi Ghafla Alishtushwa Na Kelele Za Ajabu Alipoamka Akaona Nyani Wengi Wakiwa Wamevaa Kofia Zake Akasikitika Huku Akijishika Kichwa Mara Nyani Nao Wakamuiga Akashusha Mikono Nyani Nao Wakashusha Jamaa Akagundua Wanamuiga Akachukua Kofia Yake Akaitupa Chini Na Nyani Wote Wakatupa Kofia Zao Jamaa Akazikusanya Akaondoka Nazo.
Baada Ya Miaka 50 Jamaa Akawa Mzee Na Mjukuu Wake Naye Akawa Mmachinga Siku Moja Naye Wakati Anarudi Akapita Kwenye Pori Na Kwakua Alikuwa Amechoka Akaamua Kupumzika Kwenye Mti Akiwa Ameweka Furushi La Kofia Akapitiwa Na Usingizi Akashtushwa Na Kelele Na Kukuta Nyani Wengi Wamevaa Kofia Na Kwakua Alisikia Stori Ya Babu Yake Akatupa Kofia Chini Ila Hakuna Nyani Aliyetupa Ndipo Nyani Mmoja Akamwambia" We Zuzu Unafikiri Babu Unaye Peke Yako" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
>>> Katika Safari Kulikuwako Mzungu, Mchina, Mmasai Na Mchaga.
Wakiwa Safarini Ikatokea Dhoruba Kali Mpaka Meli Ikataka Kuzama Ikalazimika Kila Mtu Atupe Mizigo Yake:
Akaanza Mzungu Akatupa Computer
MZUNGU: Zipo Nyingi Kwetu.
Akafata Mchina Akatupa Mabox Ya Simu
MCHINA: Zipo Nyingi Kwetu.
Akaja Mmasai Akatupa Ng'ombe
MMASAI: Watazaliana Wengine.
Alipofika Mchaga Akaona Kila Kitu Kina Thamani Akaamua Amtupe Mmasai Na Kusema:
MCHAGA: Hawa Wapo Wengi Sana Kule Kwetu Monduli. [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna Jamaa Flani Alikuwa Anaishi Na Mama Yake, Mdogo Wake Pamoja Na Mbwa Aliyempenda Sana.
Siku Moja Jamaa Alisafiri Akakaa Kama Mwezi Halafu Akarudi Alipofika Nyumbani Mdogo Wake Akamkimbilia
DOGO: Kaka Mbwa Wako Amekufa Juzi.
Jamaa Akasikitika Sana Na Hasa Jinsi Alivyofikishiwa Taarifa,
JAMAA: Daah Usingesema Ivyo Unatakiwa Angalau Uanze Kusema Mbwa Wako Alikuwa Juu Ya Paa Halafu Akadondoka Nakuwa Nimejiandaa Kisaikolojia.
DOGO: Sawa Kaka Nitajirekebisha.
JAMAA: Na Mama Yuko Wapi?
DOGO: Alikuwa Juu Ya Paa.
[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kulikuwa Na Mazishi Mwanamke Alifariki.
Wakati Wabebaji Wanalitoa Jeneza Nje Kutokea Ndani Wakaligongesha Ukutani,
Mara Wakasikia Sauti Ndani Walipofungua Wakakuta Yule Mwanamke Yuko Hai.
Yule Mwanamke Akaishi Miaka 5 Na Akafa Tena,
Siku Ya Mazishi Wakati Wanatoa Jeneza Nje Mume Wake Akafoka Kwa Sauti "Jamani Taratibu Msije Mkaligongesha Tena." [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
bure kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…