Whatsssssss!!!!!!!!!????

Zuzu mmoja alinunua gazeti alipofika nyumbani tu akaenda kuliweka ndani ya friji, mama ake aliyekuwa amekaa sebuleni akashangaa akamuuliza "mbona umeweka gazeti ndani ya friji?"
zuzu akajibu" wameandika lina habari motomoto acha zipoe kiasi ndo nizisome."[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtu na mkewe walizozana wakiwa Moshi.
MKE: mbona tangu tufike hapa moshi unaniita MOSHILING?
MUME: " hee wewe mwanamke upendweje mbona tukiwa dar nakuita DARLING.[emoji12][emoji13][emoji23][emoji23]
 
Jamaa wawili walikuwa wanacheza karata porini. Mara wakapita wakulima,wakasikia sauti inasema, "weka jembe chini". Wakaweka majembe yao chini. "Weka kisu, wakaweka visu chini, "naomba kopa, wakaangaliana hawana kopa"..
"kama huna kopa weka mavi chini, ikabidi mmoja anye palepale". Mara wakasikia " kama huna mavi lamba, ikabidi yule ambaye hajanya alambe ya mwenzake.... Mara wakasikia "GAME OVER", Wakashtuka "daaah kumbe ulikuwa mchezo." [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DEMU: Mambo beby
JAMAA: Poa beby
DEME: Nimekumiss, naomba Tshs50,000 niende salon kutengeneza nywele.
JAMAA: Umeunganishwa na huduma ya voicemail, bonyeza 2 kuacha ujumbe au bonyeza 1 kujitoa [emoji12][emoji13][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uongo mwingine ni ishu.
Jamaa: unasoma?
Demu: sisomi vipi wewe unasoma?
Jamaa: ndio nipo kidato cha 4 jangwani.
Demu: jamani hiyo si shule ya wasichana?
Jamaa: aha sorry nimechanganya nipo kisutu.
Demu: mwee mbona nayo ya wasichana?.
Jamaa: nilikuwa nakutania tu nachukua masterz i.f.m.
Demu: mmh ina mana i.f.m imeanza kutoa masterz?.
Jamaa: ishia zako demu mwenyewe unauliza maswali kama tupo uhamiaji?
NA KWA TAARIFA YAKO NACHUKUA DIGRII YA UDAKTARI C.B.E.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna msichana mmoja katoka kijijini,akawa anafanya mapenzi na mvulana wa mjini,sasa yule mvulana kabla hajaanza chochote akaenda kuvaa mpira a.k.a condom. Sasa alivyorudi yule msichana nyumbani akachukua simu akapiga "MAGE NIMEPATA MVULANA NINILIU YAKE HATA HAIJAFUNGULIWA MPYAA. [emoji12][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Kinyozi mmoja alifungua saluni gorofa ya juu,baada ya kuona wateja hamna akaamua aamishe saluni gorofa ya chini akaandika bonge la bango linalosema "YULE KINYOZI ALIYEKUWA ANANYOA JUU SASA ANANYOA CHINI.."[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mama mjamzito alikuwa na tumbo kubwa alipoenda hospitali akaambiwa atazaa mapacha 3,
watoto mle tumboni wakaanza kujadili:-
MTOTO WA 1: mimi nikitoka nataka kuwa fundi umeme kuna giza sana humu ndani.
MTOT WA 2: mimi nikitoka nataka kuwa fundi bomba kuna unyevunyevu sana humu.
MTOTO WA 3: mimi nataka kuwa mwanajeshi na yule nyoka anayeingiaga humu ndani nnamkatakata mapanga [emoji23][emoji23][emoji23]
 
OMARI: mke wangu ananidharau sana.
SHABANI: kwanini?
OMARI: anasema eti hajawai ona mwanaume mjinga kama mimi.
SHABANI: huyo mwanamke hajaona wajinga nini? Ngoja nimuite yule dereva wa bodaboda ndo ujue duniani kuna wajinga(shabani akamuita dereva wa bodaboda)
SHABANI: oya hebu chukua hizi sh.500 nenda pale kwangu kaangalie kama nipo.
DEREVA: sawa bro (dereva wa bodaboda akaondoka).
SHABANI: unaona omari sasa yule ndo mjinga mke wako hajaona kitu.
OMARI: Ahaaa!! Kweli yule jamaa ni mjinga ningekuwa mimi ningechukua pesa halafu ningekupigia simu kama upo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mmasai kaenda kusimama nje ya kanisa na kondoo wake.
Pasta alipomuona akamwambia"yeroo si uingie kanisani,mbona unakaa nje?"
masai akajibu"unadhani mi mjinga eeeh si naskia simba wa yudah yuko ndani."[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mlevi flani alikuwa anapita akamuona mchungaji anabatiza watu mtoni.
Akaamua kujiunga ilipofika zamu yake mchungaji akamzamisha kwenye maji mara ya kwanza na kumuuliza "umempata yesu??"
MLEVI: "hapana"
MCHUNGAJI: akamzamisha mara ya 2 kisha akamtoa na kumuuliza"umempata yesu sasa?"
MLEVI:"hapana"
MCHUNGAJI: akamzamisha mara 3 na kumtoa na kumuuliza tena"haya sasa umempata yesu?"
MLEVI: "hivi mchungaji una uhakika huyo yesu alizamia hapa au unanisumbua tu?
Mchungaji hoi[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mlevi mmoja alibatizwa majini. Mchungaji akasema tangu sasa hutaitwa RAHIMU utaitwa YOHANA maana umekua kiumbe kipya. Mlevi alipofika nyumbani akachukua bia akaitumbukiza kwenye ndoo ya maji akisema kuanzia sasa hutaitwa TUSKER utaitwa FANTA maana umekuwa kinywaji kipya halafu akainywa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wanafunzi wa shule waliambiwa watengeneze Tv kwa kutumia maboksi siku ya kuleta Tv wanafunzi wote wakaleta maboksi yao,kasoro mmoja yeye akaleta karatasi kubwa haijaandikwa kitu chochote.
MWALIMU: wewe vipi mbona umeleta karatasi?.
MWANAFUNZI: hamna mwalimu hii ni flat screen.!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
MHUDUMU: Karibu mteja
DOGO: Asante
MHUDUMU: Nikusaidie nini
DOGO: Chips kuku Shs ngapi?
MHUDUMU: Shs 7000
DOGO: Je kama nimekuja na kuku wangu?
MHUDUMU: [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mwalimu alimuuliza Omari darasani "ukiwa mkubwa, utataka nini?"
OMARI: Nataka niwe na pesa nyingi nioe mke mrembo, tuwe tunaogelea pamoja, niwe nikifanya mapenzi nae mara 3 kwa siku na niwe......."
MWALIMU: akamkatiza Omari, kisha akamgeukia Aisha na kumuuliza " na wewe unataka nini ukiwa mkubwa?"
AISHA: nataka niwe mke wa omari. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa mmoja alienda kwenye kibanda cha kuuza chipsi,alipofika akaagiza chipsi na mayai,yule muuzaji akamuuliza:-
MUUZAJI: hoya braza vipi nizichanganye?
Jamaa kwa kujifanya mjuaji na lugha inapanda akasema:-
JAMAA: Yeah Confuse Them.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
BABA: unamjua Julius Nyerere?
MTOTO: hapana simjui.
BABA: pumbavu sana kuwa makini na masomo yako.
MTOTO: haya,na wewe baba unamjua Hamisi Kibonyezo?
BABA: hapana simjui.
MTOTO: pumbav sana, kuwa makini na ndoa yako.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Walikuwepo walevi watatu wametoka kulewa basi wakaenda sehemu zinakopaki bajaji wakapanda yule dereva baada ya kuona wamelewa akawasha bajaji kisha akaizima akawaambia haya tumefika.
MLEVI WA 1: akasema asante
MLEVI WA 2: akatoa pesa na kulipia.
MLEVI WA 3: akampiga kofi dereva na kumwambia siku nyengine usiendeshe kwa spidi kama hii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa mmoja alipeleka gari yake gereji ili ipakwe rangi.
FUNDI: tupake rangi gani?
JAMAA: paka rangi zote isipokuwa kijani, njano, blue, nyekundu, nyeupe, machungwa, kijivu na nyinginezo. nije kuichukua lini?
FUNDI: njoo siku zote isipokuwa jumatatu, jumanne, jumatano, alhamis, ijumaa, jumamosi na jumapili na siku nyinginezo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…