It can hardly be possible for a man to sit comfortably when he is broke. Wakati mwingine baada ya mitego na mirija yote ya hela kukwama na grafu ya kipato kuanza kuelekea chini, humlazimu mwanaume kutulia na kutafakari njia anazopitia katika utafutaji wake. Utulivu wake hulenga kuweka mikakati mipya pasipo kumshirikisha mke (hasa wale wake ambao hukwaza kwa dhihaka katika suala ambalo mume alitarajia kupewa moyo na mawazo mbadala ya utafutaji wanaposhirikishwa). Ukimya wa mume huweza kutafsiriwa na mkewe kuwa yupo comfortable... Hakuna mwanaume anaweza kuwa comfortable wakati anajua ada ya watoto, kodi na bills mbalimbali zinahitajika.
Lakini kubwa kuliko ni kuwa ni wakati huohuo mwanaume anapokuwa broke anaweza kuimarika katika mahusiano kwa mkewe iwapo atakuwa mfariji na mwenye kuibua fikra za kujikwamua; wakati upande wa pili anaweza kupoteza hisia kabisa kwa mke mbwatukakaji na mwenye dharau kwake kiasi ambacho hata maisha yakirejea katika ubora wake, thamani ya mke huyo haiwezi kuwapo tena kamwe akilini mwa mwanaume.