When one tells you,he didn't love you...uwiiiiiiiiiii

Sweetdada yaani huna haja ya kutamani kufa ,
Furahi maisha haya mafupi sana hutakiwi kuishi kwa shida na mawazo
Kwanza huyo alokwambia hivyo kakuepushia mengi sana ingawa kwa akili za kawaida utaona kama amekunyanyasa kisaikolojia
Iko siku utamshukuru kwa hili..
Cha msingi jipe moyo na mshukuru mungu kwa kila jambo
Utampata utakayempenda kwa dhati
 
DA kuna sehemu umesema wewe ni chombo cha haja. Kama ulisoma vizuri ile sredi, utaona kuwa kwa wanawake wenye shepu kama yako wanaume ni wengi sana. Wenyewe mnasema ukiniachia tu nimedakwa........Sasa basi huwezi jua kama mwenzio naye ni kama wewe, manake kuna wanawake ambao kwa kweli kwao wanaume ni wachache sana na hao ndio wengi. All being said sweetdada we komaa tu, kwanza wewe sweet bwana, tulia wapo washkaji watakupenda tu.
 
watu wa namna hyo wachomwe moto au kupigwa mawe hadharan......shen.....zy zao
 

Nilijua tu lazima uninukuu.
DW si na mimi nimemshauri hivyo au? Hiyo red.
 
mie hapa sielewi.... hii thread ni mwendelezo wa ile ya anajifanya bab kubwa? kama ndio basi si zingeunganishwa tu? au ndio ile ya kuongeza threads per day?
 
Mtetezi wako yu hai na hatimaye atasimama kukutetea, Mungu ni mwenye haki na hata kuacha kamwe!! Mungu anajua mwanzo na mwisho wa maisha yako, Mungu anakuwazia mawazo ya Amani. Hakupendi huyo lakini Mungu anakupenda sana, hakupendi huyo lakini wazazi wako, kaka na dada zako na rafiki zako wanakupenda.

Usihangaike na kiburi chake, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, na siku zote mbio za sakafuni huishia ukingoni. Huyo hakuwa mume wako, hakufai wala usijute kama kaweza kutamka kwa kinywa chake hakupendi Mshukuru Mungu lazima kuna jambo anakuepusha nalo.

Jitahidi kunyamaza wala usijibizane naye, wala usimlaumu kwa sasa, mimina moyo wako kwa Mungu, tulia jipe muda wa kumtafuta Mungu kwa bidii utapona na utapata neema ya kupita salama katika hilo jaribu.

Hebu ona kama hayo yote ni mapito tu, upo wakati wa furaha unakuja kwako, unajua dhahabu haiwezi kuwa dhahabu mpaka imepita kwenye moto, wewe ni dhahabu, ukitulia sasa nina uhakika utakuwa umejifunza mengi utakuwa msaada kwa watu na utaimarika zaidi kiakili na kiroho pia.

Kataa hiyo roho ya mauti kabisa, huo ni mpango wa adui, fikiria hata ukifa unafikiri yy atapata faida? Hapana kwanza hakupendi, mtoto wako, na ndugu zako ndio wataumia. Haijalishi kakupotezea muda kiasi gani, Mungu ni mwenye haki na anahukumu kwa haki. We msamehe, muachie Mungu ashughulike naye mwenyewe, wakati ukifika atajutia maneno yake....wakati yy anajuta ww umeshapona na unaendelea na maisha yako.

Ngoja niishie hapa dada, lakini ninakuombea, najua unachopitia, najua unavyoumia lkn kwa usalama wa afya na akili yako, lia na Mungu tu, utaona neema ya ajabu.
 
Dada pole sana kwa yaliyokukuta

Lakini amini Mungu mtu anaweza kuishi na mwengine miaka kadhaa bila ya kumpenda na akitaka kumwambia akakosa courage. Na siku akimwambia ndio anashindwa kuisema vizuri inatoka kavu kavu.

Na madhali alikuwa akijilazimisha kuishi na wewe japo hakupendi, alikuwa akiumia. Bora sasa utaumia wewe lakini utapona utasonga mbele, kuliko kuendelea kuishi na asiyekupenda.

point ya niongeza: Kama mtu umejua kumbe hukuwa unampenda, unatakiwa umwambie vipi?
 
oooohhhhhh pole sana sweetdada kweli inauma sana lakini ndio ukweli jipe moyo mkabidhi Mungu yote mwite Mungu yeye ndio atakuondolea machungu yote uliyo nayo.
usiwe pekee yako katika wakati huu mgumu machungu yatazidi moyoni kuwa na rafiki yako wa karibu unayejua mnapendana na akutie moyo na kukufariji
Kumbuka kuna watu wanakupenda sana mie mmojawapo
TUNAKUPENDA SANA
 

LD kwa maneno haya naamini yatamliwaza sana umeongea maneno mazuri hata mie nilipata huzuni sana niliposoma hii thread lakini umenifariji sana ulipotoa mchango wako.
 
Pole sana mdada, inauma sana ila muombe tu mungu yatapita tena muombee maisha marefu huyo mtalaka wako maana yatakayokuja kumpata utashangaa na hutoamini. Mbona wapo wengi tu wa hivyo anakupotezea muda halafu baadae anakuacha bila sababu za msingi ila kinachokuja kuwatokeaga yaani muombee tu aishi maisha marefu atakuja kumpata mwanamke ambae atamchezesha kiduku mpaka miguu ipinde niamini, kwa sasa utaona kama nakupoza moyo tu ila ikitokea utanikumbuka atakuja kukoma huyo mpaka akomae wewe msubirie tu mpe miaka miwili tu.
 

:smiling: u made me laugh.thnx
 

Asante LD kwa maneno yako yanatuliza moyo
 


MANENO YAKO YANA FARAJA SANA - SI KWA HUYO MWENYE TATIZO TU ILA KWA WENGI TULIOPITIA MATATIZO AINA MBALI MBALI - NATAMANI NINGEONGEA NAWEWE LIVE - MUNGU AKUBARIKI KWA KUUPONYA MOYO WANGU KWA MANENO YAKO - AM TELLING YOU - YOU DESERVE TO RUN A FAITH COUNSELING CENTRE - AGAIN BE BLESSED ALWAYS :decision:
 

mwenzanguu,ningeyajua mapema basi si kunambia leo baada ya kuachieve wat he wanted in life mxiii
 
Inawezekana akawa keshawahi kukwambia kwa njia nyengine wewe ukawa huamini.

Nazungumza kwa experience hapa, nishamwambia mtu kistaarabu kuwa kwangu naona ni mistake kuwa naye, lakini anatafuta kila sababu za kupinga hiyo kauli na kuzidi kujisogeza karibu na familia yangu.

Hebu jaribu kaa ukumbuke kwenye muda wote huo hukuona dalili au maneno ya kuwa hakupendi?

mwenzanguu,ningeyajua mapema basi si kunambia leo baada ya kuachieve wat he wanted in life mxiii
 
mwenzanguu,ningeyajua mapema basi si kunambia leo baada ya kuachieve wat he wanted in life mxiii
dont give up your life and happiness... but before doing anything, jiangalie 360 degree na ujue pia how many things are said when people are angry and if they really mean what they say

asiyekupenda singeweza kukaa na wewe for six year, especially mwanaume, sisi sio wavumilivu
 
Aya ya ya ya yaya ya aisee nasikia ku....roho ya mtu eti anasemaje???? Wewe ni mvumilivu aise aaahhh anakwambia maneno hayo uwwiiiiii Mungu nisamehe niishie hapa aaiiiiii naweza aaaaa leo ni siku ya wanawake ngoja niache duuhhhh

Dena haya yote he said them kwa kunitext.he did not have guts kunambia face to face.afu alivyo mshenzi anajitilisha huruma na kusema
eti he is confused he doesnt know wat to do anaweza kunywa sumu coz of me and the baby...mxiiii..kufaa..jamani nina hasira tena na wanaume wooote
 

Huwezi amini vetinari hakuna neno kasema ila vitendo ndo kama nilivyosema kwenye ile sred alijiweka distant recemtly kiaina may be ndo ilikuwa jinsi ya kunambia....tena juzijuzi tu hapa last week kanipeleka kwenye sherehe ya ndugu huko he was all over me mpaka watu wanamshangaa..kama si kutiana aibu mi nitapeleka wapi sura yangu..
 
swty dada pole my dia!!

karibia kila msichana ukimuuliza atakwambia nijinsi gani alivyowahi kuumizwa katika maisha yake tena na mwanaume!!

nilijifunza kitu kimoja na mie baada ya kunikuta ya kunikuta " Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana".nidhambi kumpenda mwanadamu mpk akikuacha unatamani kujiua!!

Weka tumaini lako kwa Mungu zaidi, mambo yote yatakwenda sawa my dia!!!
 
Am happy you know the truth.....we advised you to seek the truth....trust me,it will set you free....now:

You may be feeling the pain of negative words spoken over your life, or maybe you've spoken to someone else and you wish you could take back. Maybe there are things in your past that you think can't be forgiven. Or maybe you feel guilt for some past failure or resentment and unforgiveness toward someone who has wronged you.Whatever your need may be, let God meet it! Allow the power of His forgiveness to sweep across your heart and life and make everything new.

God is a good God, and He is at work in your life. Trust Him because He is faithful. His plans are always for your good. His plans are always to prosper you. He delights in seeing you grow and succeed. Make the decision to cooperate with what God is doing. Set aside the wrong questions, set aside complaining, and pick up His peace and joy and move forward with Him in victory and blessing every day of this New Life without him.Happy Womens Day!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…