When one tells you,he didn't love you...uwiiiiiiiiiii

Yote mabaya sana, sijawai au sijakupenda....dah! yote inamaanisha kibuti mbaya!!
 

Thnx Michelle.Happy Womens day to u too :smiling:
 
...haina tofauti na kuwa cheated.

Tatizo, tuna tabia ya ku ignore the signs, mpaka pale inapokuwa too late halafu unatafuta wa kumlaumu.
Kujiua sio suluhisho ni udhaifu, kwamba huwezi kuchukua responsibilities za matendo yako.

Learn mama, deal with it, Life's too precious kuendekeza 'udhaifu' wa roho
...move on!
 
not even i don't love you anymore.hiyo ingekuwa afadhali my dear...he said i did not love you.Nilikutamani

Dont expect too much from men. Mara nyingi wanaume tunaigiza na hizo tenz tunazowaimbia ni usanii tu. Hata nyie wadada mnaodhani mnapendwa, jueni inawezekana tu ni usanii. Upendo wa kweli upo kwa mama, baba, mtoto, au ndugu, at least mna ukoo. Sasa we unategemea miujiza toka kwa mtu hata ukoo hamna!
 
Wasi wasi wangu Mbu ni kuwa keshawahi hata kutamkiwa kuwa hapendwi, lakini akafumbia macho. Mpaka jamaa kaamua kutema kavu kavu.

Wanawake wakipenda wanafikiri na wao wanapendwa kama vile wanavyopenda, na hata wakipewa ukweli wataubadilisha tu.


 

Sweetdada sasa unaanza kunichanganya tena anatia huruma eti yuko confused??? Na nini tena?? Wewe ushampotezea kajua au??

Hebu niweke sawa maana hapa sasa unaanza kunichanganya
 
Sweetdada sasa unaanza kunichanganya tena anatia huruma eti yuko confused??? Na nini tena?? Wewe ushampotezea kajua au??

Hebu niweke sawa maana hapa sasa unaanza kunichanganya

yani ni hivi Dena..kaongea maneno yooote hayo ni mengi hayaelezeki.keshamaliza.anatext tena "am sorry but hapa nilipo nalia naweza hata kunywa sumu nife coz i dont know wat to do on this.."..sasa mie kushangaa iweje unywe sumu na umesema wewe,nikamwmabia aache unafiki
 
Wasi wasi wangu Mbu ni kuwa keshawahi hata kutamkiwa kuwa hapendwi, lakini akafumbia macho. Mpaka jamaa kaamua kutema kavu kavu.

Wanawake wakipenda wanafikiri na wao wanapendwa kama vile wanavyopenda, na hata wakipewa ukweli wataubadilisha tu.

aaa ngoja nipotezee mana naweza kukunyonya hayo macho..mana hatuelewani.read this clearly.HAJAWAHI KUTAMKA HANIPENDI.
 

Wewe kuwa kama mimi "IM a Woman with Principles" Nikisema no its no, nikisema yes it is.

Stand on your own ok?? Asikupotezee muda yaani uniambie ulikuwa hunipendi urudi tena eti im confused to hell kafie hukoooooooo.

Ni afadhali angesema unajua mie siku hizi mapenzi yamepungua kuliko huo upuuzi aliosema.

Piga chini achana nae mtoto mtoto ndo nini bana watu wameolewa na watoto wanne nini mmoja.

Endelea na maisha yako natamani ningekuwa karibu na wewe nikushauri ana kwa ana.
 

usikasirike sana Dena..am done with him.Mungu atanisaidia nitapita haya majaribu salama.
there is a reason for everything,may be nimeepushwa..

Asanteni wote kwa kunipa moyo..i feel much better
 
I am beginning to doubt sasa.... yawezekana matatizo yapo kote
 

Karibu yatima, mimi huwa naamini hakuna kitu kinachopita ktk maisha ya mwanadamu ambacho Mungu hajakiona, ni kila kitu kina kusudi. Lakini tukitambua kuwa mstakabali wa maisha yetu upo mikononi mwa Mungu tukimtegemea kwa unyenyekevu tunavuka!! Nitakutafuta!!

Sijui kwa nn umeamua kutumia jina hili, lakini tutaongea zaidi, sio vizuri kujiita jina linalo reflect wakati mgumu tunaopitia......
 
usikasirike sana Dena..am done with him.Mungu atanisaidia nitapita haya majaribu salama.
there is a reason for everything,may be nimeepushwa..

Asanteni wote kwa kunipa moyo..i feel much better

Unajua kuna wanaume wanajiaminisha wanawake hawana msimamo wala hawajui kitu!! Na kwa bahati mbaya hawa viumbe wamepewa akili ya ajabu ya kucheza na kichwa na moyo wa mwanamke!!

Lakini nakuhakikishia utakaposimama kwa miguu yako, ukaweka Imani yako kwa Mungu, na ukamtangizia kumshukuru Mungu kwa mapito yote na kumwambia naona ushindi ktk mambo yote.

Atajutaaaaa, na litakuwa kinamtesa kila siku. Mpaka hapi atakapokaa amrudie Mungu wake, ampe na yy neema ya kujirekebisha. Amini hivi chochote atakachokuambia sasa hivi ni UONGO. Sio kweli hata kidogo, iweje achukue miaka 6 kutamka sikupendi halafu achukue masaa 2 kusema nilikosea sio kweli hata kidogo.

Dada tunaishi kwa Neema ya Mungu, tunakula kwa sababu Mungu yupo. Mkabidhi mtoto wako mikononi mwa Mungu, amuepushe na magonjwa na hila za adui. Yeye muache kama alivyo kwa sasa. Tulia wala usikubali akupigie pigie hata msg zake usisome ikibidi. Wala usimjibu. Mpe nafasi, jipe nafasi ya kupangua moja baada ya jingine akilini mwako.

JIPANGE SAWA!! Hata kama asipokuheshimu tayari unaye mtu wakukuheshimu, hata dunia ikuite majina gani, ukiishi kwa malengo ukamlea mtoto wako vizuri, yeye atasema huyu ni mama yangu. Mbona aliniacha hai, mbona hakunitupa, mbona amenilea amenisomesha!!!

Daaaah furahi shangilia kabisa, kula ushibe mtukuze Mungu, na utakufanya kuwa mke mwema.

Stay blessed forever!!!
 
kivipi MTM?

Hakuna haja ya kutafuta una tatizo wapi. Swala ni kwamba hakupendi basi!!!! Kwa hiyo matatizo yako sio tatizo tatizo hakupendi, alikuwa anatafuta starehe!! Madhaifu yako yangesaidia kama angesema nachukia tabia yako hii na hii. Lakini Hakupendi.

Mwambie sawa yupo anayenipenda, alikuja kutafuta starehe lakini ipo siku atajutia hiyo starehe. Mtegemee Mungu. Unajua Mungu siku zote anatenda haki. Nakuhakikishia ipo siku atapiga magoti ajutie hiyo starehe yake.

Uzuri naongea kitu ninachokiamini na ninachokijua.
Sio wa kwanza wewe dada, ndo maana nimekwambia unaangaliwa kuwa mwalimu mzuri, haya yapo ktk dunia hii na yataendelea kuwepo. Ni nani atawasaidia watu kama sio mm na wewe???

Tulia usianze kujihukumu bureeeee!!!!
 
Mmmh! Baaaaad,
Pole sana. Njoo huku upendwe mama.
On the second thought, alitaka kutolea pressure zake za sex kwako, wanawake mnatakiwa kufahamu haya mambo.

Juzi niliongelea the very same thing!!www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/115345-i-was-lonely-and-you-were-there.html SweetDada pole mwaya...soma hapo japo sikusema ufanye nini ikitokea ila utajifunza yasikukutd tena mpendwa!Pole tena!
 
haya MTM academia, nimekukubali haraka kabla sijatoa povu

Ila wanasema the best way ya kujua where you stand in anything, ni kujiangalia kwanza wewe... are we sure hayajasemwa na pande zote hayo amneno ya hasira??

Nimesoma sehemu hapahapa anasema ameshachukia wanaume wote, to me hii ni kauli ya hasira na kamwe sitamhukumu kwani najua hamaanishi coz ana ndugu jamaa na marafiki anaowapenda.... in love life we say all nasty stuffs but we end up making it up and move on avoiding all precursors za problems

bado naamini kabisa both had some roles to play to the problem, imagine kama mtu haambiliki, hata kama unataka kumwambia kitu, inakua ngumu and may take year to break the silence

I am still looking for a balanced decision na sio judgemental au principally, normally, categorically, scientifically etc.

Ni hayo tu, ila mdogo wangu sweetdada... solution ya matatizo yako ipo kwako, wengi humu tuna makubwa zaidi na kama tungesikiliza ya humu basi all members wangekua either divorced, separated or single for life

I am done maana naogopa kum-bore sweetheart shem wangu LD, sipendi atoke povu:hand:
 

dah!LD asante sana, una maneno ya faraja..sikuwa mtu wa kumweka Mungu mbele kwa kila jambo,inabidi nimrudie kwa kweli
nashukuru dada umejaliwa kipaji..nasikia moyo wangu u mwepeesi kwa kusoma maneno yako..ubarikiwe.:mwaaah:
 
Pole sana kwa yaliyokukuta, Mungu wetu ni mwaminifu hili litapita na utashangaa. Mtangulize Mungu katika maisha yako, mlee mtoto wako kwa furaha msahau, malipo ni hapahapa duniani, dunia itamfundisha. Soma Zaburi 23
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…