Tena wewe ndo hutatoa hata talaka moja,
Hivi unajua kuwa hakuna kitu kigumu kama talaka??
Kuna dogo wangu, mke wake anapigiwa simu na mzinzi mwenzake hata saa 6 usiku...Juzi kaja kwenye familia, watu wakamshauri aanze upya maisha yake..Alikubali vizuri tu utadhani ni dume mwenye akili. Akaamua kumrudisha mke kwao. Haikupita hata week 2, nasikia kesharudisha mke wake eti anampenda sana kiasi kwamba hataki kuona watoto wake wanaishi bila mama yao!!
Unacheza na talaka wewe?? Ni rahisi sana kuandika na kutamka hayo maneno kwa watu wengine...Ila asikwambie mtu kwamba rusha vitendo hapa....!
Ngoja niishie hapa.
Dunia imekuwa hivyo toka imeumbwa na hakuna jipya!
Babu DC!!