Alafu hii miradi ni ya serikali gatuzi na sio serikali kuu. Naona Sultani Ali Hassan Joho anajitahidi kweli kweli. Hata Gavana Alfred Mutua pia kule Gatuzi la Machokos na Wycliffe Oparanya kule Kakamega wanajitahidi vilivyo. Gatuzi zote 47 zikifanikiwa kuwekeza kwenye miundo mbinu ya aina hii, ya kukuza talanta kwenye michezo kule mashinani itakuwa jambo la maana sana.