Where is God?

Where is God?

SimbaMpole123

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2023
Posts
5,501
Reaction score
4,956
Mi najiuliza maswali mengi. Mungu Ni Nini, anataka Nini na Yuko wapi.

Ukifuatilia historia ya binadamu tokea tukiwa wawindaji maporini miungu ilikuwepo. Wazee walikuwa wanaongoza vijana kwa kuwaambia kuwa Mungu anataka mfanye hivi, na hio miungu ilikuwepo pangoni ambapo wazee tu wanaingia, baadae vijana wakajitoa akili kwenda wakaona wazee ni waongo na hamna kitu mule. Wagiriki wakaja na miungu yao wakasema ipo ya milima ya Olympus.

Leo hii watu wamepanda milima yote ugiriki hawajaona miungu hio. Wakaja wayahudi, wakasema Mungu yupo mawinguni. Ukifuatilia hata Yesu alipaa mawinguni, Mungu alifungua madirisha ya mbinguni kuleta mafuriko, alichungulia kutoka mawinguni kwenye mnara wa babel, etc. Waislamu nao wakaja na mbingu Saba sijui. Anyways wazungu wametengeneza ndege na rocket zimeenda mawinguni, nje ya dunia, mpaka mwezini. Sasa hivi watu wa dini wanasema yupo nje ya ulimwengu.

So nikagundua trend, wanamficha, wanamweka mbali ili watu wasiweze kumfikia, why? Kwa sababu hayupo? Kwa sababu hajasema hizo sheria? Why wanamficha. Afu wanakuambia anataka uamini yupo ndo utapona usipoamini unaunguzwa. Ukiuliza nikimwona afu nikamwamini, anasema no, lazma usimwone ndo uamini. Na wanaweka kifo mwisho wa kumuani ili waweze kuendelea kutunga sheria kwa jina lake na kuweza kuendelea kutawala watu kwa sababu hamna mtu Ashawahi kurudi akasema baada ya kifo kipo hivi. Mwanasayansi mi nauliza Mbinguni Kuna Nini.

Hamna njaa hamna maumivu hamna ndoa hamna chochote zaidi ya kumuabudu Mungu. Watu kanisani na msikitini hawapendi kwenda unategemea watapenda milele ya Ibada. So wakaamua kuanzisha motoni kutishia watu kwamba wataunguzwa milele. Sasa, ukifa unaacha mwili wako hapa, wanasema una roho, roho ni Nini, hoo mawazo sijui pumzi, ukiuliza unajua kazi ya ubongo ni Nini mtu hajui, haya tufanye roho ni ka upepo kanaenda motoni ehe kanaunguaje, hakana nyama, hakana nervous system hakana ngozi, hakana pain receptors, hakana ubongo au spinal cord, maumivu unayasikiaje, na bado hatujauliza huu Moto upo wapi, walisemaga chini kisa mavolcano lakini now hawasemi Tena coz of elimu.

Tukienda kwenye sheria zenyewe sijui usivae nguo tofauti, usile shellfish, usichanganye mazao, usimwage nje, usiabudu sanamu lakini abudu kitu Cha kufikiriwa na myahudi, hivi kwa Nini mtu atengeneze nyota billion 60 na sayari trillion afu aje kujali binadamu wewe ambae ni Kama vumbi kwa huu ulimwengu unamwaga wapi. Na kwa Nini sheria hizi zinaonekana Kama sheria za kabila ya la zamani huko kwenye majangwa na haziendani na sheria za binadamu kuishi na watu vizuri. Na Wanavyosema tumuabudu siku ya Saba.

Siku zimekuja kutengenezewa baadae Sana na zimebadilika badilika Mara kwa Mara katika historia ya Mayans na Romans. Na wamechagua sun day coz ni siku ya pagans kuabudu jua. Ila yote haya tuyaache, why Mungu muweza yote anataka hela, mwisho wa siku wote mnabidi mgundue kuwa binadamu walitengeneza miungu ili kujibu maswali magumu yasiyojibika kipindi kile na kuwatawala watu kwa ujinga na hofu.
 
Mungu siyo kiumbe Bali Ni cheo Kama Cha diwani, mbunge au rais.
Duniani Kuna miungu zaidi ya 10,000 lakini Mungu pekee aliyethibitisha ukuu wake juu ya miungu yote ni yule aliyewatokea Waebrania wakiwa utumwani nchi Misri, akafanya matnendo ya kutisha hadi wakaachiwa na mfalme farao.

Akawafanyia njia katika bahari, mchana akatumia wingu kuwaongoza na usiku nguzo ya Moto Kama compass directory.

Walipohisi njaa aliwashushua mikate na kware kutoka juu. Walipohisi kiu aliwafanyia maji kutoka kwenye jiwe la jangwani. Kwa uweza wake, Punda alizungumza Kama bin'Adam.

Alipoona wanaadamu wanateswa na Nguvu za giza, iliituma pumpzi ya nafsi yake iliyofanyika mtu katika tumbo la mwanamke na baadaye mtu yule alifanyika kafara ya damu kwaajili ya ondoleo la dhambi na ikawa agano kuwa kwa kila aliitiaye jina Hilo ataokolewa kutoka kwenye mateso ya nguvu za giza, na Ile pumzi ya Mungu itaingingia ndani ya mwili wake na kufanyika Mungu pamoja na Wanaadamu (Emmanuel).

Kwa maelezo hayo usimtafute Mungu aliko kwa kutumia ndege na rocket Bali kwa kutubu na kufuata amri zake zilizo katika Biblia Takatifu, naye Mungu atakuwa ndani yako.
 
Ukitoka hapa nenda kasearch google uone if the Bible is historical. Hamna data za kihistoria zinazosupport kitabu Cha Kutoka. Wachimbaji wameona historia nzima ya Misri hawajaona ushahidi wowote kwamba walikuwa na watumwa wayahudi. Hiyo miji waliyoteka sijui hamna uthibitisho wa kihistoria, hamna mifupa au vifaa vilivyopatikana katika Hilo jangwa, hio sehemu watu walitembea siku 9 sio miaka 40 na kipindi hicho Canaan ilikuwa koloni la Misri hence it means wayahudi walitoka Misri kwenda Misri which doesn't make sense. Kingine
Kunatofauti gani ya tamaduni kumtengeneza Mungu, na Mungu kutokea tamaduni fulani. Mungu si yupo ulimwenguni kote, kwa Nini awatokee wayahudi na sio wamasai, la sivyo wametengeneza huyo Mungu ndo maana sheria zake ni za kiyahudi.
 
Mungu Yuko wapi? Basi funua ubongo wako kwani mawazo yanapatikana kwenye ubongo. Wewe mwenyewe umemuumbia kwenye ubongo. Mungu ni wazo tu! Baada ya kushindwa kupata ukweli unaamua kuwa Kuna mwenye uwezo zaidi ambae ni wazo la Mungu. Tusema tu ni mambo ya kufikirika.
 
Bora umeongea ukweli, coz wengine wanaogopa kusema coz wametishiwa.
 
Mungu siyo kiumbe Bali Ni cheo Kama Cha diwani, mbunge au rais.
Duniani Kuna miungu zaidi ya 10,000 lakini Mungu pekee aliyethibitisha ukuu wake juu ya miungu yote ni yule aliyewatokea Waebrania wakiwa utumwani nchi Misri, akafanya matnendo ya kutisha hadi wakaachiwa na mfalme farao.

Akawafanyia njia katika bahari, mchana akatumia wingu kuwaongoza na usiku nguzo ya Moto Kama compass directory.

Walipohisi njaa aliwashushua mikate na kware kutoka juu. Walipohisi kiu aliwafanyia maji kutoka kwenye jiwe la jangwani. Kwa uweza wake, Punda alizungumza Kama bin'Adam.

Alipoona wanaadamu wanateswa na Nguvu za giza, iliituma pumpzi ya nafsi yake iliyofanyika mtu katika tumbo la mwanamke na baadaye mtu yule alifanyika kafara ya damu kwaajili ya ondoleo la dhambi na ikawa agano kuwa kwa kila aliitiaye jina Hilo ataokolewa kutoka kwenye mateso ya nguvu za giza, na Ile pumzi ya Mungu itaingingia ndani ya mwili wake na kufanyika Mungu pamoja na Wanaadamu (Emmanuel).

Kwa maelezo hayo usimtafute Mungu aliko kwa kutumia ndege na rocket Bali kwa kutubu na kufuata amri zake zilizo katika Biblia Takatifu, naye Mungu atakuwa ndani yako.

Mkuu kwani huyo Mungu aliyewatokea waebrania amekwisha kufa? Kwanini hatokei huko Sudan au Gaza au kwingineko watu wanakopata madhila makubwa kuliko waliopata waebrania?

Unaamini hekaya za kutunga za miaka milioni nyuma na hujiulizi kipi kinamfanya huyo mungu asijidhihirishe sasa?

Hakuna Mungu kwasababu hayupo na hana impact yoyote kwenye maisha yetu
 
😁Truth be told
 
We have omnipotent creator ambaye hana Muda wowote na mwanadamu anachokifanya hapa duniani...

Huyu Mungu wa kisasa ni watu walimtengeneza na kumpigania....alianza kufa baada ya science revolution 500 years ago...

Sio mbaya ametawala Kwa miaka zaidi ya 7000 tukirudi mwanzo wa agano la kale...

He is dead and not great anymore.....ili usimuhitaji inabidi uhakikishe haumuhitaji otherwise you will fall into delusional mind
 
Back
Top Bottom