Which engineering field has the best scope?

Soma Civil Engineering

African countries - cuvil engineering.

Civil engineering haiku nivutia sana lakini nitajaribu kupitia Syllabus kwa mara nyingine.
 
kujiajiri ni simple kwan haihitaj kua na mtaj mkubw san,mfano mzur ni maintenance ambazo unaeza kuzifanya kuanzia katik makaz ya watu mpka office kubwa..
Pia ni rahis kua umeajiriwa na uku ukawa unapiga kaz zengne za nje!
Inspection,testing, wiring installation huku zinafanywa na wahitimu wa vocational college. Kama una degree ya EEE na unataka kuwa electrician, ilikupata kazi kirahisi inabidi usome tena vocational courses ambazo employers wengi wanapendelea vyeti vyao kwa sababu wanakuwa wamefuzu zaidi kwenye hayo mambo.
 
Mkuu Chonya Wa Chilonwa kama nlivyotangulia hapo juu kusema, hongera sana kwa kuwa na malengo ya kusoma engineering!!! na hongera pia kwa kutumia muda wako kufanya research kuhusu fields mbali mbali za engineering!!! sijapata hakika sana kama umepanga kusomea huko huko france au utakuja bongo kusoma, whatever the case...haya ni mawazo yangu...
kama nilivyoahidi....
1)Civil engineering
Kwa hapa nyumbani (tanzania) hii kiasi flani ina upana sana katika kujiajiri na kuajiriwa. Ukianzia katika sekta za serikali na binafsi, mashirika mbali mbali ya research yanahitaji hawa watu!! most likely ukisomea hii kozi uta specialize katika moja hizi fields structural,transport engineering na baadhi ya vyuo wameongeza irrigation na water resources!! changamoto kubwa ya hii field ni tenda nyingi kupewa watu wa nje(wachina na wengineo), kuwepo kwa wataalam feki na kutokuwepo kwa capital hasa mainjinia wazawa!! mkuu simaanishi kwamba huwezi ajiriwa au kujiajiri, uwanja upo mkubwa sana!! japo umesema hujai feel ila unaweza ukaifikiria tena hii field...
2) Mechanical engineering
Kwa maoni yangu hii inafwatia kwa ubora hapa kwetu!! kama utasomea hii kozi unaweza specialize kwenye energy production, au general... popote ambapo civil engineer yupo huyu lazima awepo!! kazi zao ni katika ujenzi, migodini bila kusahau secta za binafsi na serikali!! uzalishaji wa mashine mbali mbali na kudesign mara nyingi ndio kazi zao!!
3) Electrical and electonics engineering au electrical engineering.
Sasa hii ntamwomba Maganga Mkweli , Sinziga King'asti Horseshoe Arch Consultant na wengine waje watie neno hapa!! japo wengi wanasema iko so limited nikimaanisha wao waafanya kazi tanesco tu, hii sio kweli!! hakuna project ambayo inaanzishwa bila hawa watu kuwepo!! migodini, ujezi wa nyumba, bara bara, uzaishaji umeme and so forth kote huko wanapatikana!! na kama ukisomea hii most likely unaweza specialize kwenye power generation, micro computer, au general electrical!! kwa hapa tanzania bado sana inalipa na ina future nzuri kama utafaulu na kuipenda!! katika hii kozi kama nlivyosema unaweza pia kusomea mambo ya computer kama ukiambua kuspecilize huko..inawezekana!!
4)Petrolium engineering
Hakuna ubishi kwamba gesi imevumbuliwa hapa nyumbani, na kwa msisitizo hii kozi imeanza fundishwa kwenye vyuo kama UDSM(imeanza mwaka huu) na UDOM!! ni kozi nzuri na future yake ni nzuri, ila kama unataka kujiajiri nadhani haitakua rahisi kiasi flani na mara kwa mara unaweza ajiriwa na serikali!! changamoto nyingine ni kwamba, katika field hii ya gesi hasa hapa bongo makampuni mengi yenye tenda ni ya nje na mara nyingi wanakuja na wataalamu wao(simaanishi wataalam wa ndani hawaajiriwi), sasa hapa mbongo kupata kazi kiasi flani inaweza kua ngumu!!
5)Agriculture engineering
Kwa hapa nyumbani hii kozi inatolewa chuo kimoja tu, nchi sasa imeweka mkazo sana kwenye mambo ya kilimo, na kama unavyoona watu hawa kiasi fulani wapo wachache sana, kama unataka kujiajiri ni rahisi sana na kama kuajiriwa pia haisumbui!! makampuni ya uzalishaji hasa kilimo wanahitaji sana hawa watu, kwenye viwanda nako hawa watu fiti..
6)Chemical engineering
Mara nyingi hawa watu wanabase sana kwenye viwanda na uzalishaji(processing) kwa ujumla. na kwa hapa tanzania inatolewa na vyuo kama viwili kama sikosei(UDSM na SUA), bado hawa watu wanahitajika sana na ni choice nzuri. Kwa mtazamo wangu hawa watu ni ngumu kidogo kujiajiri(simaanishi haiwezekani kijiajiri), labda kama unauwezo ukaanzisha kiwanda chako...
7) Computer engineering, Software engineering
Kuliko ukasomee computer science(kama unataka kusomea engineering) ni bora ukasomea moja ya hizo mbili. kwa hapa bongo inakaugumu flai kupata kazi katika serikali ila ni rahisi sana kujiajiri hasa kama consultant engineer. tukianza na compurer engineering wana deal sana na hardware na kiasi flani computer science imemezwa na hii, na kwa baadh ya vyuo ukifika mwaka wa tatu unaweza ukaspecilize katika software engineering!! software engineering, on the other hand, kwa hapa tz inatolea na UDOM pekee, bado sana watu wake wanahitajika sana katika sekta binafsi na serikali!!
8)Irrigation engineering
Kwa hapa kwetu inatolewa na vyuo vitatu tu (SUA na arusha tech,instutute of water dar), hii kozi ni subset ya civil engineering na kwa baadhi ya vyuo wanaijumisha na water resources engineering!! hamna mtu ambaye hajui mabadiliko ya hali ya hewa duniani!! wataalamu wa umwagiliaji wanahitajika sana duniani hasa na makampuni binafsi, bila kusahau kama unataka kuajiriwa na serikali ni rahisi mno na nirahisi kujiari!!
9)Architecture
Japo inaonekana kama sio field ya engineering, ila believe me hamana project inafanywa bila uwepo wa architect na yeye mara nyingi ndiye anadesign let say nyumba then anamkabidhi structural engineer, wataalamu wake wapo wachache hilo halina ubishi, kama unajiamini ni mbunifu(and ofcoz to be an engineer you must be creative) hii field nzuri sana hasa kwa hapa bongo!! ni rahisi sana kujiajiri na inasemekana hata ukiwa mwanafunzi hasa mwaka wa nne na tano unaweza ukawa unapiga pesa mtaani kama uko smart enough!!!
USHAURI
Hamna kitu kizuri kama kufanya kazi au kitu unachopenda toka moyoni mwako bila kulazimishwa na mtu!! kwa field yoyote utayoenda hakikisha unaenda sio kwa sababu inalipa ua utapata tittle mtaani ila kwa sababu unaipenda toka moyoni!! kumbuka changamoto zipo anzia shuleni(sup) mpaka makazini...ila kama umeenda kwasababu unaipenda kamwe hutatishwa na changamoto hizo!!! Kumbuka hamna kitu kizuri kama kutimiza ndoto zako maishani!! Ukifanikiwa maliza usisahau kujisajili kama proffesional engineer ili utambulike ndani na nje....na kama unaswali usisite kuuliza..

Karibu sana uhandisini mkuu, na kila heri...
 
labda na mimi nitie neno kidogo..na thanks mkuu LORDVILLEkwa kutambua uwepo wangu.... kwa nafasi yangu napenda UMEME/ELECTRICAL POWER ENGINEERING na najivunia vijana wengi niliwashauri wakiwa A LEVEL wasome hii kozi mimi binafsi nilishauriwa pia.. kufanya hivi ...kwa tanzania kwanini usome ELECTRICAL ENGINEERING...
1. energy industry inakuwa sana kwetu kuna fursa nyingi sana ...

2.hii course iko wide sana ..hasa kwenye suala la kuajiri ambayo ndio lengo lako la kwanza ... (kuna miradi mingi sasa especially ya REA-Rural electricafication,construction nyingi zinafanyika sasa ,kuna project nyingi za gesi zinakuja fikria kuhusu hili..

3.kwa ajira bado hii kozi haijasaturate sana .. kuna waajiri wengi wako makampuni ni mengi sana yanahitaji electrical engineers(viwanda vinakuja vingi sana ,makampuni makubwa ya generation of electrical power yanakuja kwa kasi)

4.hata jeshini demand ya wahandisi wa umeme ni kubwa sana..
kifupi power industry iko vizuri brave people wanaenjoy sana...


chaguo la pili CIVIL STUCTURE ENG. la tatu ni MECHANICAL ENG....
petroleum engineering naiona imekaa kuajiriwa sana iko narrow kwa mtazamo wangu..ingawa inaonekana ni hotcake kwa sasa kama ilivyokuwa telecom na computer eng early 2000's ...

NAPENDA ELECTRICAL CIVIL NA MECH sababu naona zina wigo mpana sana.. hasa kwetu third world
UAMUZI NI WAKO...
ASANTE..
 
Last edited by a moderator:

Thank you for your contribution mkuu!!! I believe Chonya Wa Chilonwa he/she may get something from you!! appreciated brother...
 
Last edited by a moderator:
Chonya Wa Chilonwa, kama unataka kuja kujiajiri civil engineering bado ina wigo mpana sana wa kujijenga. Mechanical engineering itakuwa na soko kubwa kama Chuma ya Liganga na Oil& Gas Industry ikisimama vizuri. Naamini Era tuliyonayo sio ya expansion telecomunication industry tena...ni ya infrastructural and industrial expansion, kuanzia barabara mpaka viwanda vya kudhalisha bidhaa.
 
Last edited by a moderator:

Ningekushauri kusoma Electrical Engineering, ina wide career opportunities kwa kweli. Haipo too specific kama kozi nyingine.
 


Nicethread..nimeipenda kwakuwa maoni utakayopewa hapa si kwamba yatakusaidia wewebali yatawasidia pia na wadogo zetu wanaoendelea kusoma A- level


Napendapia nikutoe wasiwasi kwenye suala la ajira, kwa engineering field kuna unafuu(japo kidogo) ukilinganisha na field zingine ( tuliosoma coet tunaziita ‘ngwini’)


kilaengineering field ina soko zuri tu ila mimi ningependa nikushauri ukasomeENVIRONMENTAL ENGINEERING japo hujairodhesha kwenye list yako ila hii ndo thebest na kamwe huwezi kulala nyumbani wala kuzunguka na vibahasha vya kaki kwazaidi ya mwezi..mbali na iyo nenda kasome Chemical engineering. Ukitaka nikuchambulie field moja baada yanyingine kwa undani zaidiI will do that for you coz engineering field zote ninao college mates, so uwa tuna sharechangamoto na kupeana mawazo ya hapa na pale.. karibu sana kwenye ulimwenguhuu.


 
Kama una ideas za kujiajiri, nashauri usome Civil na Software engineering.
Civil mtu anajiajiri vipi...naomba kamfano hata kamoja tu kanatosha
Note:ieleweke kuwa lengo langu ni kujua tu jinsi mtu anavojiajiri na sio kuonesha kuwa mtu hawezi jiajiri na civil..
 
Civil mtu anajiajiri vipi...naomba kamfano hata kamoja tu kanatosha
Note:ieleweke kuwa lengo langu ni kujua tu jinsi mtu anavojiajiri na sio kuonesha kuwa mtu hawezi jiajiri na civil..

Unafungua kampuni yako mkuu, kwan hawa civil engineers wametoka wapi?
 
Mkuu, umemwaga data vizuri sana..greatly appreciated!

Labda soon tutawaona Sinziga King'asti Horseshoe Arch Consultant .


Thanks you.
 
Thank you for your input.
 
Ni kweli mkuu,
Kuna watu kutokana na wameishi nje nchi kwa muda mrefu wanasomea kozi zinaendana na mazingira yaliyopo wakirudi nyumbani wanakuta mabo ni tofauti kabisa.
 
Mkuu hii mimi ilinipa shida sana kufanya maamuzi juu ya kozi ipi ambayo ingefaa kutokana na mfumo wetu wa maisha na mzingira yake..

Mimi nilikuwa muda mrefu nchini Ujeruman kwa kipindi kirefu na mdhamin wangu akawa na nia kubwa kuniendeleza ila sio kwa jinsi ya kuja kuajiliwa,Bali kujiajili.

Alikuja Dar kukagua soko la ajira, kisha akaniambia machenical Eng nzuri ijapo limeshikwa na Wachina, sio kwa ubora wao wa kazi bali vifaa walivyonavyo na mitaji wanayo dhaminiwa na selkari yao.

kikubwa akanishauri nisome hii fani na kweli nimefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana..sasa nipo Dar natafuta wadau kunifahamu.na nimeona inalipa sana ukiwa na mtaji.

Mimi nakushauri sama hii fani kaka tuwe wengi tupate kushauriana, maana huu ni ulimwengu wa machine bhana haswa magari.
 

Mkuu samahani, hivi Mech engineering ndo ufundi makenika? Kama ndio vipi opportunities unazoongelea ni car garages ama??
 
Mimi nimesoma mach Eng ambapo wenzetu wanataka ujue fani zote za mitambo
Mf, nimechomelea zaidi ya miezi 6, nimechonga vyumba muda tu, kisha nikaingia kwenye magari sana sasa kama miaka 4 hivi na nikaingia mtaani kutafuta visent ila muda wa miaka 10 ukwa umekwisha ndio kurudi Dar..
 
Juu ya opportunities za hapa Dar sina uzoefu sana maana ndio nina miezi 2 sasa hapa Dar ila naona pesa ipo hapa nyumbani ukijiajili mwenyewe...

Maana mfumo wa wenzetu ni wa kujiajili sio kwenda kuwa meneja wa kiwanda fulani au mkuu selkari hapana..ngoja nikimbizane nione nitarudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…