Which engineering field has the best scope?

Which engineering field has the best scope?

I'm planning to study engineering this year but I'm stuck between a rock and hard place.

Kwa sasa hivi ninaishi France lakini nina mpango wa kurudi Tanzania baada ya miaka 3-4 na nimeona njia ya kukabiliana na maisha ya nyumbani ni kusoma kozi ambayo ninaweza kujiajiri au kuajiriwa na nimehamua nitasomea Engineering kwa sababu it appeals to me the most and i have a passion for it.

I have done research on a range of engineering fields. I have looked at syllabus, subjects and talked to student course advisors and I’m intrigued by seven disciplines.


1) Mechanical engineer.
2) Electronic/electrical engineering.
3) Computer engineer
4) Software engineer
5) Computer science
6) Chemical engineer
7) Process engineer

Tatizo langu lipo kwenye "employment and business opportunies" baada ya graduate.Nimeondoka Tanzania muda mrefu kidogo, therefore I’m behind the curve na imenifanya nishindwe kudecided nikozi ipi ni jiunge nayo.

However, I’m leaning towards Mechanical engineering due to its broadness, to have wider opportunities.

I know,it doesn't sound good to start looking at “career/market scenarios” especially if you want to be engineer. But,
i have seen here (France), graduates kama wa computer science,some of them are confused after their plans didn't materialized. They are doing menial jobs such as stacking shelves in supermarkets.

I’m trying to avoid the same path but i’m aware the worst thing is to corner myself into something which i wont be happy with.

WAKUU, Ninaomba msaada ni kozi gani,nikichangia na jitihada zangu inaweza kunisaidi Tanzania baada ya miaka 3-4?


It’s my first time to post here...

Merci beaucoup (Thank you very much).

Watu wengine kwani ukisema unaishi chumbageni utadharauliwa? Njoo tu ukasome unachotaka huwezi kuamuliwa na mtu kuhusu maisha yako
 
Mkuu hii mimi ilinipa shida sana kufanya maamuzi juu ya kozi ipi ambayo ingefaa kutokana na mfumo wetu wa maisha na mzingira yake..Mimi nilikuwa muda mrefu nchini Ujeruman kwa kipindi kirefu na mdhamin wangu akawa na nia kubwa kuniendeleza ila sio kwa jinsi ya kuja kuajiliwa,Bali kujiajili. Alikuja Dar kukagua soko la ajira, kisha akaniambia machenical Eng nzuri ijapo limeshikwa na Wachina, sio kwa ubora wao wa kazi bali vifaa walivyonavyo na mitaji wanayo dhaminiwa na selkari yao.kikubwa akanishauri nisome hii fani na kweli nimefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana..sasa nipo Dar natafuta wadau kunifahamu.na nimeona inalipa sana ukiwa na mtaji.Mimi nakushauri sama hii fani kaka tuwe wengi tupate kushauriana, maana huu ni ulimwengu wa machine bhana haswa magari.
Hivi hakuna visas restriction kwenye employments?! Ni kitu gani kinawashinda uhamiaji kuweka vikwazo kwenye kazi zinazoweza kufanywa na watanzania wenyewe? Rate of unemployment is very high Tanzania, vijana wenzangu wamemaliza chuo kikuu lakini wapo vijiweni kutokana na uhaba wa ajira, halafu wageni wanakuja kufanya hizo kazi kwa viwango duni...inasikitisha!
 
Mkuu samahani, hivi Mech engineering ndo ufundi makenika? Kama ndio vipi opportunities unazoongelea ni car garages ama??
ME sio machines na magari, ni very broad field, ukiangalia karibu vitu vingi ninavyokuzunguka mechanical engineer wamehusika kwa kiasi fulani kudesign.Kwa mfano switch ya umeme "on and off" button ni ME, robot, injection molding systems,computer keyboard ni ME hata kwenye Oil and gas wana play part kubwa.Lakini tatizo letu Bongo hatuko kwenye kudesign, huko tumewaachia wazungu, sisi tupo kwenye spanner zaidi.
 
Mkuu Chonya Wa Chilonwa kama nlivyotangulia hapo juu kusema, hongera sana kwa kuwa na malengo ya kusoma engineering!!! na hongera pia kwa kutumia muda wako kufanya research kuhusu fields mbali mbali za engineering!!! sijapata hakika sana kama umepanga kusomea huko huko france au utakuja bongo kusoma, whatever the case...haya ni mawazo yangu...
kama nilivyoahidi....
1)Civil engineering
Kwa hapa nyumbani (tanzania) hii kiasi flani ina upana sana katika kujiajiri na kuajiriwa. Ukianzia katika sekta za serikali na binafsi, mashirika mbali mbali ya research yanahitaji hawa watu!! most likely ukisomea hii kozi uta specialize katika moja hizi fields structural,transport engineering na baadhi ya vyuo wameongeza irrigation na water resources!! changamoto kubwa ya hii field ni tenda nyingi kupewa watu wa nje(wachina na wengineo), kuwepo kwa wataalam feki na kutokuwepo kwa capital hasa mainjinia wazawa!! mkuu simaanishi kwamba huwezi ajiriwa au kujiajiri, uwanja upo mkubwa sana!! japo umesema hujai feel ila unaweza ukaifikiria tena hii field...
2) Mechanical engineering
Kwa maoni yangu hii inafwatia kwa ubora hapa kwetu!! kama utasomea hii kozi unaweza specialize kwenye energy production, au general... popote ambapo civil engineer yupo huyu lazima awepo!! kazi zao ni katika ujenzi, migodini bila kusahau secta za binafsi na serikali!! uzalishaji wa mashine mbali mbali na kudesign mara nyingi ndio kazi zao!!
3) Electrical and electonics engineering au electrical engineering.
Sasa hii ntamwomba Maganga Mkweli , Sinziga King'asti Horseshoe Arch Consultant na wengine waje watie neno hapa!! japo wengi wanasema iko so limited nikimaanisha wao waafanya kazi tanesco tu, hii sio kweli!! hakuna project ambayo inaanzishwa bila hawa watu kuwepo!! migodini, ujezi wa nyumba, bara bara, uzaishaji umeme and so forth kote huko wanapatikana!! na kama ukisomea hii most likely unaweza specialize kwenye power generation, micro computer, au general electrical!! kwa hapa tanzania bado sana inalipa na ina future nzuri kama utafaulu na kuipenda!! katika hii kozi kama nlivyosema unaweza pia kusomea mambo ya computer kama ukiambua kuspecilize huko..inawezekana!!
4)Petrolium engineering
Hakuna ubishi kwamba gesi imevumbuliwa hapa nyumbani, na kwa msisitizo hii kozi imeanza fundishwa kwenye vyuo kama UDSM(imeanza mwaka huu) na UDOM!! ni kozi nzuri na future yake ni nzuri, ila kama unataka kujiajiri nadhani haitakua rahisi kiasi flani na mara kwa mara unaweza ajiriwa na serikali!! changamoto nyingine ni kwamba, katika field hii ya gesi hasa hapa bongo makampuni mengi yenye tenda ni ya nje na mara nyingi wanakuja na wataalamu wao(simaanishi wataalam wa ndani hawaajiriwi), sasa hapa mbongo kupata kazi kiasi flani inaweza kua ngumu!!
5)Agriculture engineering
Kwa hapa nyumbani hii kozi inatolewa chuo kimoja tu, nchi sasa imeweka mkazo sana kwenye mambo ya kilimo, na kama unavyoona watu hawa kiasi fulani wapo wachache sana, kama unataka kujiajiri ni rahisi sana na kama kuajiriwa pia haisumbui!! makampuni ya uzalishaji hasa kilimo wanahitaji sana hawa watu, kwenye viwanda nako hawa watu fiti..
6)Chemical engineering
Mara nyingi hawa watu wanabase sana kwenye viwanda na uzalishaji(processing) kwa ujumla. na kwa hapa tanzania inatolewa na vyuo kama viwili kama sikosei(UDSM na SUA), bado hawa watu wanahitajika sana na ni choice nzuri. Kwa mtazamo wangu hawa watu ni ngumu kidogo kujiajiri(simaanishi haiwezekani kijiajiri), labda kama unauwezo ukaanzisha kiwanda chako...
7) Computer engineering, Software engineering
Kuliko ukasomee computer science(kama unataka kusomea engineering) ni bora ukasomea moja ya hizo mbili. kwa hapa bongo inakaugumu flai kupata kazi katika serikali ila ni rahisi sana kujiajiri hasa kama consultant engineer. tukianza na compurer engineering wana deal sana na hardware na kiasi flani computer science imemezwa na hii, na kwa baadh ya vyuo ukifika mwaka wa tatu unaweza ukaspecilize katika software engineering!! software engineering, on the other hand, kwa hapa tz inatolea na UDOM pekee, bado sana watu wake wanahitajika sana katika sekta binafsi na serikali!!
8)Irrigation engineering
Kwa hapa kwetu inatolewa na vyuo vitatu tu (SUA na arusha tech,instutute of water dar), hii kozi ni subset ya civil engineering na kwa baadhi ya vyuo wanaijumisha na water resources engineering!! hamna mtu ambaye hajui mabadiliko ya hali ya hewa duniani!! wataalamu wa umwagiliaji wanahitajika sana duniani hasa na makampuni binafsi, bila kusahau kama unataka kuajiriwa na serikali ni rahisi mno na nirahisi kujiari!!
9)Architecture
Japo inaonekana kama sio field ya engineering, ila believe me hamana project inafanywa bila uwepo wa architect na yeye mara nyingi ndiye anadesign let say nyumba then anamkabidhi structural engineer, wataalamu wake wapo wachache hilo halina ubishi, kama unajiamini ni mbunifu(and ofcoz to be an engineer you must be creative) hii field nzuri sana hasa kwa hapa bongo!! ni rahisi sana kujiajiri na inasemekana hata ukiwa mwanafunzi hasa mwaka wa nne na tano unaweza ukawa unapiga pesa mtaani kama uko smart enough!!!
USHAURI
Hamna kitu kizuri kama kufanya kazi au kitu unachopenda toka moyoni mwako bila kulazimishwa na mtu!! kwa field yoyote utayoenda hakikisha unaenda sio kwa sababu inalipa ua utapata tittle mtaani ila kwa sababu unaipenda toka moyoni!! kumbuka changamoto zipo anzia shuleni(sup) mpaka makazini...ila kama umeenda kwasababu unaipenda kamwe hutatishwa na changamoto hizo!!! Kumbuka hamna kitu kizuri kama kutimiza ndoto zako maishani!! Ukifanikiwa maliza usisahau kujisajili kama proffesional engineer ili utambulike ndani na nje....na kama unaswali usisite kuuliza..

Karibu sana uhandisini mkuu, na kila heri...

Mungu akubariki, hasa kwa kuitumia elimu yako kwa ajili ya kuelimisha na wengine, Nice job brother
 
Watu wengine kwani ukisema unaishi chumbageni utadharauliwa?
hawezi dharauliwa, ila hii ni sehemu ambayo amtu ana uhuru wa kusema anachojiskia ila asivunje sheria na katika hili sidhani kama mleta mada kakosea!!
Njoo tu ukasome unachotaka huwezi kuamuliwa na mtu kuhusu maisha yako
naamini hata wewe kuna kipindi uliomba ushauri, nadhani ungetofautisha kati ya USHAURI na KUAMULIWA MAISHA mkuu!!
 
Hivi hakuna visas restriction kwenye employments?! Ni kitu gani kinawashinda uhamiaji kuweka vikwazo kwenye kazi zinazoweza kufanywa na watanzania wenyewe?
kisha akaniambia machenical Eng nzuri ijapo limeshikwa na Wachina, sio kwa ubora wao wa kazi bali vifaa walivyonavyo na mitaji wanayo dhaminiwa na selkari yao.
haya ni maneno yaliyotajwa na mdau hapo juu... you have a good observation!! cha kwanza kujua ni kwamba sisi(tanzania) ni nci inayohitaji misaada toka kwa nchi washirika...nikupe mfano, kuna project labda ya kujenga mabwawa na china ikafadhili hiyo project, je unadhani hiyo tenda watapewa wachina au wazawa? jibu unalo...

Kuna factor nyingine ya capital hapa naongelea mitambo ya ujenzi, kwa hapa nyumbani tuna project inaefanywa kule bagamoyo, na hii project inahitaji contractor mwenye vifaa vya kisasa kitu ambacho kwa mainjia au makampuni ya ndani kiasi flani ni ngumu kupata, na wageni mara nyingi huwaga wanafadhiliwa na serikali zao in terms of capital!! na hii kiasi flani inawasaidia kuwin tenda mbali mbali!! na kuhusu swala la visa restrictions kwa nchi kama yetu ni ngumu ku-impliment sheria kama hizo hasa kwa wageni wa mataifa makubwa!!
Rate of unemployment is very high Tanzania, vijana wenzangu wamemaliza chuo kikuu lakini wapo vijiweni kutokana na uhaba wa ajira, halafu wageni wanakuja kufanya hizo kazi kwa viwango duni...inasikitisha!
I concur with you, but this is our home land and that is the reality ..ila sio kigezo cha kutopambana!!
 
Watu wengine kwani ukisema unaishi chumbageni utadharauliwa? Njoo tu ukasome unachotaka huwezi kuamuliwa na mtu kuhusu maisha yako
Ni sehemu gani kwenye posts zangu zimekupa impression nipo Chumbageni? Kama ningekuwa Chumbageni isingenipa tatizo kuandika hivyo kwa sababu sidhani watu hapa wanachangia kwa sababu mwanzisha thread yupo sehemu fulani. Angalia thread nyingine na utaelewa ninachosema.
 
haya ni maneno yaliyotajwa na mdau hapo juu... you have a good observation!! cha kwanza kujua ni kwamba sisi(tanzania) ni nci inayohitaji misaada toka kwa nchi washirika...nikupe mfano, kuna project labda ya kujenga mabwawa na china ikafadhili hiyo project, je unadhani hiyo tenda watapewa wachina au wazawa? jibu unalo...Kuna factor nyingine ya capital hapa naongelea mitambo ya ujenzi, kwa hapa nyumbani tuna project inaefanywa kule bagamoyo, na hii project inahitaji contractor mwenye vifaa vya kisasa kitu ambacho kwa mainjia au makampuni ya ndani kiasi flani ni ngumu kupata, na wageni mara nyingi huwaga wanafadhiliwa na serikali zao in terms of capital!! na hii kiasi flani inawasaidia kuwin tenda mbali mbali!! na kuhusu swala la visa restrictions kwa nchi kama yetu ni ngumu ku-impliment sheria kama hizo hasa kwa wageni wa mataifa makubwa!!I concur with you, but this is our home land and that is the reality ..ila sio kigezo cha kutopambana!!
Haya makampuni ya barabara and the like ni sawa, hata Membe akiwafuata uko China kwenye maofisi yao kuwapa viza ni sawa tu. Tatizo langu ni hawa wawekezaji wadogo wadogo wa kichina,kwa mafano wamachinga au kama "NI MTAZAMO TU" alivyosema mention hapo juu, wapo pia kwenye biashara ya garages.Sidhani biashara kama hizi sisi wabongo hatuna ujuzi au mtaji.Serikali wangeweka kipengele cha kiasi cha mtaji kwenye maombi ya viza za biashara.Lakini ili alinitatizi kutimiza ndoto yangu, kama wazungu wanavyosema " If you can't stand the heat, get out of the kitchen", nipo tayari kupambana.
 
Nimetolea mfano tu wa makazi sikumaanisha kuwa unakaa huko nilipokusema.

hawezi dharauliwa, ila hii ni sehemu ambayo amtu ana uhuru wa kusema anachojiskia ila asivunje sheria na katika hili sidhani kama mleta mada kakosea!!

naamini hata wewe kuna kipindi uliomba ushauri, nadhani ungetofautisha kati ya USHAURI na KUAMULIWA MAISHA mkuu!!
 
I hope I am not late to advise you, lakini kama uko nje ya Tanzania na unataka kurudi bongo, usisome any of the field ulizoweka hapo. Soma Petroleum Engineering.
 
Civil mtu anajiajiri vipi...naomba kamfano hata kamoja tu kanatosha
Note:ieleweke kuwa lengo langu ni kujua tu jinsi mtu anavojiajiri na sio kuonesha kuwa mtu hawezi jiajiri na civil..

unafungua kampuni inaitwa hardman general supplies&civil engineering, hapo utapewa tenda kujenga hadi barabara za mtaani, nyumba za serikali, na za wananchi
 
Back
Top Bottom