Zantel sio UNLIMITED,
Nina package yao ya 10GB nayo huwa inazidi na mwisho wa Mwezi naletewa bill kubwa kweli, almost Tshs 490,000 kila mwezi.
Niliwahi kutumia Benson, nilijuta na sintorudia.
Nimechukua VodaCom pia, ipo kwenye majaribio ya 4months, nimechukua package ya 10GB pia. Uzuri wa VodaCom over Zantel ni kuwa unalipia kadiri unavyotumia packages zote, Zantel hawakupi package hiyo ya 10GB kama huendi Post Paid ambayo nayo lazima uambatanishe na Passport na madude kibao ya identification.
VodaCom iko slow kulinganisha na Zantel, Zain ndo niliitumia kwa wiki mbili tu na kuweka chini modem yao, ovyo tu.
TTCL ni wazuri sana, lakini iwe ni broadband ya ukweli si vile vidude wanavyobebesha watu, tatizo coverage ya TTCL si kwa Dar nzima, maeneo ya Airport hawana mtandao wa internet.
Mengine labda tuendelee kushirikishana, nshajaribu SimbaNet, Raha, AfricaOnline lakini wote hamna kitu! Wana maneno mengi sana ya ushawishi lakini ukishakuwa mteja hawana muda na wewe