Whistleblower aliyefichua uwanja wa ndege wa Kenya kuuzwa ahofia maisha yake

Whistleblower aliyefichua uwanja wa ndege wa Kenya kuuzwa ahofia maisha yake

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Nelson Amenya, kijana aliyefichua mazungumzo ya siri kati ya serikali ya Kenya na kampuni ya Adani Group ya India kuhusu mpango wa kuchukua usimamizi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa miaka 30, sasa anadai kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na vitisho alivyopokea.

Amenya alitoa taarifa hizo akiwa nje ya nchi akihofia usalama wake, licha ya kuendelea kupokea vitisho zaidi.

AMENYA.jpg

Kulingana na nyaraka zilizowekwa hadharani, mazungumzo hayo ya siri yalikuwa yamefanywa bila kuwashirikisha wazabuni wengine, na kampuni ya Adani ilipendekeza uwekezaji wa dola bilioni 1.85 ili kuimarisha miundombinu ya JKIA.

Soma pia: Kenya: Umeme wakatika nchi nzima na kuacha abiria kwenye uwanja wa ndege wa JKIA wamekwama

Hata hivyo, wakosoaji wameeleza kuwa thamani ya mkataba huo ni ndogo ukilinganishwa na umuhimu wa kimkakati wa uwanja huo, ambao huchangia asilimia tano ya GDP ya Kenya.

Uchunguzi wa bunge umeanzishwa baada ya ufichuzi huo, huku Waziri wa Fedha, John Mbadi, akisema kushtushwa na jinsi Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya (KAA) ilivyokubali pendekezo la Adani haraka.

Serikali na mashirika ya kimataifa sasa yanahimizwa kulinda rasilimali za taifa dhidi ya makundi yanayonufaika kifisadi.

Source: The Standard Media Kenya
 
Hata ivo watapita nae,viongozi wamejipa mamlaka ya umalaika mtoa roho
 
Back
Top Bottom