Whitedent wanatumia Siri gani "kuua" brands nyingine za dawa za meno eg "Aha, AfyaDent na Colgate ?

Price differentiation ndo wanayotumia, volume kubwa wakati price iko chini kuliko Colgate kwa mfano ambao volume ndogo na price iko juu. Pili kidogo ile "home sweet home" ingawa siyo sana ila inasaidia watz kujisikia wanataka chao hata kama ni kiwanda cha muwekezaji kutoka nje!!!
 
Huyu anayesema whitedent ilikuwepo toka zamani kabla ya dawa nyingine za meno!.....napata mashaka...at least ujazo na bei labda ndio pigo analotumia whitedent...nadhani pia wabongo issue ya quality sio deal kwao....kwa mfano kuna moja ya UK inaitwa Sensodyne...kana ujazo mdogo ila price yake disaster!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mm naona cologate ndio ilianza tena kitambo ilikua unaambiwa nenda kanunue cologet kama ilivyokua brand ya rungukatika dawa za kuulia mbu
 
Whitedent haina ubora kihivyo, basi tu ulofa. I am telling you tumia Dabur Herbal, you will never use those substandard brands. Kama mdomo wako unatoa harufu basi hii ndio dawa. try it , you will tell me.
Inaweza kufanya meno kuwa meupe?
 
Colgate ni nzuri zaidi kwa upande wangu. Hii whitedent imekuwa hivyo kwa sababu ya kuwa "cheap" na ofa za miswaki.
 
Whitedent ilikuja miaka mingi sana baada ya Colgate na si kama usemavyo kuwa ilianza kabla ya wengine. Na mpaka leo watu wengi dawa ya meno wanaiita colgate.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Colgate ni brand kubwa ni vile tu price yake iko juu
 
Kumbe Sensodyne iko bongo ?
 
Mkuu ina maana bukta ni brand

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani ni issue ya kibiashara, mfanyabiashara anaweza akauza bidhaa yake bei rahisi ili apate faida kubwa kuliko auze bei kubwa faida ndogo. Sema wabongo tunamentality kwamba bidhaa yenye bei kubwa ndio bora kuliko ya bei ndogo. Mtu anakuta shati mlimani city anasema original ila akilikuta kariakoo ni feki. Kwangu mm sijaona utofauti wa ubora kati ya Colgate na whitedent coz hakuna formula iliyobuniwa tanzania kati ya dawa hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha kiwi.
 
Wanagawa miswaki bure....pia dawa haina harufu au ukakasi kama zingine...pia kasha lake linavutia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…