Whitedent wanatumia Siri gani "kuua" brands nyingine za dawa za meno eg "Aha, AfyaDent na Colgate ?

Whitedent wanatumia Siri gani "kuua" brands nyingine za dawa za meno eg "Aha, AfyaDent na Colgate ?

Kuna kampuni mbili hapa bongo zilikuwa juu sana ila walipo jichanganya tu miaka ya tisini basi wakapigwa bao la ajabu.

1. Back in time Colgate ilikuwa dawa pendwa sana na watz miaka hiyo but waliingia mitini kiaina Whitedent akachukua nafasi.

2. Pepsi alikuwa hana mpinzani Tz hii,lakini alipo zingua tu Coka akampiga bao la uhakika.

"the highest risk shoud give the maximum profit"

Na Mimi nilitaka kukumbushia hili kuhusu Pepsi sijui majanga gani yalimpata mpaka akafunga viwanda kina Mzee Mengi ndo wakatoboa hapo. Miaka ya 90 mapema
 
Bora mie muhenga nimezoea kutumia Mkaa
Hahaaaa

Na kuna ile nyingine yenye virangi vitatu (AquaFresh???) Nilikua naila kama ice cream. Mpaka mzee aliposhituka bajeti inaenda ndivyo sivyo akaninyoosha ndo nikaacha
 
Tanzania zimejaa colgate fake. Lakini Whitedent huwezi linganisha na Colgate.
 
Nadhani sio kama wana mbinu kubwa wanayotumia lakini kinachowapa advantage ni ile kuwa strong brand ambayo ilianza wakati hakuna wengine na ikaendelea ku maintain ubora wake. Wakati tunakua tulikua hatusemi dawa ya meno ulikua ukitumwa dukani unaambiwa kanunue Whitedent so hiyo imekaa vizazi na vizazi. Wengi tunakuja kujua kama kuna dawa nyingine za meno tumeshakua wakubwa. Hii pia ni ipo kwenye dawa za viatu. Tulikua tukitumwa unaambiwa kanunue KIWI na sio dawa ya viatu. Mpaka baade ukikua ndo unajua kumbe KIWI ni brand tu ila ile ni dawa ya viatu. Hivo imechukua muda kidogo hawa watu kuwatoa kwenye hiyo position waliyopo kwenye akili za wateja. But naamini baada ya miaka michache hawawezi kuendelea kuwa hivi. Kumbuka hata simu ziliitwa mobitel wakati ule kwa kuwa ndo ulikua mtandao pekee wa simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
White dent sio kwamba ndio iliyoanza kabla ya Colgate, na signal ...
White dent wamalitawala soko la Tz...
Mipango mikakati yao madhubuti sana ambayo inagusa kila hali Ninavyokuhusudu soko la kitanzania. 7ps zipo njema. Japo ubora wake hauifikii Colgate hata nusu yake.
 
Unamaanisha kama itatoe dawa yenye bei ya chini kidogo kuliko Whitedent inaweza kushindana na Whitedent ?
Ndio.... Sehemu kubwa ya watanzania tunasemaga dawa ya meno.
Ilitokea Dawa ya meno yenye vigezo vyote Kama whitedent ikasambazwa, na kutangazwa kama whitedent ila ikawa na bei pungufu kidogo ya whitedent, ninauhakika watanzania wengi watainunua
 
Nadhani kila mmoja wetu ni mtumiaji wa dawa ya meno, na katika soko letu Whitedent imeteka kabisa soko kiasi kwamba kila BRAND nyingine inayojaribu kujipenyeza inapigwa mweleka, why ?

- Colgate ni brand kubwa duniani lakini hapa kwetu imeshindwa kabisa kufanya vizuri licha ya matangazo wakati Whitedent hata hawana matangazo !!

- Aha ilikufa, AfyaDent haijulikani ilipo, Aloe zinasuasua!

SIRI YA WHITEDENT ni nini ?
Ni hovyo kabisa hii dawa, ila Bei ndogo na kwa ujazo mkubwa



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kwa sababu mtu anatumia whitedent kila siku basi anajua na wengine wanatumia hiyo whitedent. Colgate walikuwepo siku nyingi na bado wpo na kwa taarifa tu mauzo ya colgate yapo juu na ina watumiaji wengi. Zipo familia ambazo hawatumii dawa nyingine tofauti na Colgate
 
Whitedent anachomzidi Colgate ni bei na ujazo ukienda dukani ukinunua Colgate ile ya elfu 3 halafu ukiliinganisha na whitedent ya elfu 3 utaona ujazo wa whitedent ni mkubwa kuliko wa colgate tena na whitedent unakuta na kamswaki chako. Kitu kingine whitedent zipo za size zaidi ya 5 na bei tofauti wakati colgate yeye ana size 3 tu.

G.O.M.D
Well said mkuu
 
Back
Top Bottom