Whitedent wanatumia Siri gani "kuua" brands nyingine za dawa za meno eg "Aha, AfyaDent na Colgate ?

Whitedent wanatumia Siri gani "kuua" brands nyingine za dawa za meno eg "Aha, AfyaDent na Colgate ?

Whitedent anatumia production philosophy- consumers prefer goods which are widely available and affordable
 
.
Sasa utafiti wako wa Whitedent japo wewe ni mtu wao lakini Ukweli ni kwamba inajitahidi kwasababu imeweza kuwa na aina kadhaa ambazo kila mtu anapata ya kwake kama ni Herbal au ingine. Pili size wameweza kuwa na size za kila mtu halafu ofa ya Mswaki ilimaliza kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kwenye ofa ya mswaki tumekamatika wengi. Kilamwezi unakuwa na mswaki mpya.
 
Kitu kikishapendwa na wanawake na watoto lazima kifanye vizuri sokoni..
Wanawake hawapendi kununua vitu vya gharama sana hasa hivi vitu vinavyoonekana kama ni vidogo vidogo !!
Whitedent wanafanya sana promotion
Kuna baadhi ya bidhaa ukinunua unakutana na zawadi ya dawa ya whitedent kama vyombo,bidhaa nyingine wanaweka miswaki yao
 
Nadhani sio kama wana mbinu kubwa wanayotumia lakini kinachowapa advantage ni ile kuwa strong brand ambayo ilianza wakati hakuna wengine na ikaendelea ku maintain ubora wake. Wakati tunakua tulikua hatusemi dawa ya meno ulikua ukitumwa dukani unaambiwa kanunue Whitedent so hiyo imekaa vizazi na vizazi. Wengi tunakuja kujua kama kuna dawa nyingine za meno tumeshakua wakubwa. Hii pia ni ipo kwenye dawa za viatu. Tulikua tukitumwa unaambiwa kanunue KIWI na sio dawa ya viatu. Mpaka baade ukikua ndo unajua kumbe KIWI ni brand tu ila ile ni dawa ya viatu. Hivo imechukua muda kidogo hawa watu kuwatoa kwenye hiyo position waliyopo kwenye akili za wateja. But naamini baada ya miaka michache hawawezi kuendelea kuwa hivi. Kumbuka hata simu ziliitwa mobitel wakati ule kwa kuwa ndo ulikua mtandao pekee wa simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe wa kizazi gani? Sisi tumekuwa tunaambiwa kanunue COLGATE au unamshangaa mbona bibi anapiga mswaki bila Colgate. Whitedent wa juzi tu.
 
Availability na bei iko chini.

Colgate ya 5,000 unanunua whitedent za 15,000
 
Back
Top Bottom